KATIBU
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa
amesema Rais Jakaya Kikwete ndiye analiyeliangamiza Taifa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa
Alibainisha kuwa kitendo cha Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Kikwete kushindwa kuchukua uamuzi makini katika masuala muhimu kwa taifa ndiko kunakoliangamiza na kuliteketeza.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo katika mikutano yake miwili aliyoifanya katika wilaya za Momba na Mbozi zilizopo mkoani Mbeya.
Alisema mgogoro wa uchinjaji wa nyama baina ya Waislamu na Wakristo iliyotokea hivi karibuni ni miongoni mwa masuala yanayoliweka taifa kubaya, lakini imechangiwa na serikali dhaifu ya CCM.
Aliongeza kuwa Rais Kikwete amekuwa na tabia ya kuchelewa kuchukua uamuzi sahihi na kwa wakati yanapojitokeza matatizo yanayotishia umoja, amani na mshikamano uliopo kwa muda mrefu hapa nchini.
Alibainisha kuwa migogoro mingi inayotokea hapa nchini inajengwa au kutengenezwa na serikali iliyojikita kusambaza sumu ya udini katika misikiti wakati wa kampeni za urais mwaka 2010.

No comments:
Post a Comment