Marehemu steven kanumba
WASANII wa filamu Tanzania wapo katika harakati za mwisho wa mchakato wao katika maandalizi ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni moja ya jambo walilokusudia kuhakikisha wanamuenzi na kuthamini mchango aliouacha kwenye tasnia ya filamu
Akizungumzia maandalizi hayo jijini Dar es Salaam rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba alisema kuwa baadhi ya maandalizi yameanza kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba, huku wakishirikiana na familia ya marehemu ili kuweka mipango ya nini kifanyike katika harakati za kutimiza lengo
Alisema kuwa lengo lao lazima litimie kwa sababu walikusudia kufanya kitu kwa ajili ya kumuenzi marehemu kutokana na mchango wake aliouacha kwenye filamu na ili kudhihirisha hilo wanaamua kumenzi katika hali ya kiupekee
"Lazima tufanye kitu cha tofauti katika kumuenzi marehemu na ili tuonyeshe upendo wetu lazima tuheshimu kile alichokiacha kwa kuendeleza" alisema Mwakifwamba
Aliongozea kuwa muda ukifika na maazimio yakipitishwa ndipo ataweka wazi ni jambo gani lililokusudiwa kufanyika
Akizungumza na sisi maeneo ya hotel ya lamada msanii ambaye anasifika kwakuwa baba wa wasanii JB amesema kuwa si jambo la kufikiria kwa mtu kama Kanumba kumfanyia siku ya kumbukumbu kwani mchango wake kwa tasinia hii ni mkubwa sana pengine kuliko mtu yeyote kwani alitufanikishia kutafuta masoko ya nje na hata hapa ndani hakuna ubishi kuwa Kanumba na Ray wana mashabiki wengi sana so kwetu kama wasanii tutaungana na kuweka kila kitu pembeni kwa ajili ya kumuenzi mwenzetu aliyetangulia mbele ya haki .
Kwa upande wa Vicent Kigosi(Ray) alisema siku hiyo ni muhimu sana na ni siku ambayo kwake haitamtoka akilini mwake na mkumbuka kwa mengi sana nachoweza kusema Mungu ampe pumziko la amani,Ray ameyaongea hayo kwa uchungu sana na kuwaasa wasanii kumrudia Mungu kwani hakuna ajuae siku wala saa.
Marehemu Steven Kanumba amefariki april 7 mwaka 2012 ambapo chanzo cha kifo chake kinadaiwa kuwa ni ugomvi wa mapenzi, na aliyekuwa mpenzi wake msanii mwenzie wa filamu Lulu ambae bado anakabiliwa na kesi hiyo licha ya kuwa nnje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment