Saturday, March 9, 2013

UWOYA USO KWA USO NA NDIKUMANA LEO NCHINI RWANDA


Irene Uwoya

Msanii mwenye tittle bubwa kunako tasnia ya filamu Tanzania Irene Uwoya leo atakutana uso kwa uso na mumewe Ndikumana nchini Rwanda ambapo amepata mualiko maalum wa utoaji tuzo za filamu zilizoandaliwa nchini humo, Katika msafara huo Uwoya maongozana na wasanii wengine kama Mzee Majuto,Jb na Ray.

Uwoya pamoja na kundi hilo watakuwa moja kati ya watoaji wa tuzo hizo kwa washindi watakaotangazwa kama washindi wa Tuzo zinazojulikana kama Rwanda movie Awards, wasanii waliondoka jijini Dar es salaam siku ya jumatano kwa ajili ya utoaji wa tuzo ambazo zimezidi kujichukulia umaarufu Rwanda na Afrika Mashariki.


Wasanii hao wakiwa nchini Rwanda wataonana na mke wa nchi hiyo Paul Kagame mama Jeannette Kagame na kubadilishana mawili matatu kisha kurudi nchini Tanzania, pia kampuni ya Steps Entertainment ambayo ndio wasambazaji wakubwa wa filamu Swahiliwood itapata fursa ya kutangaza filamu zake katika tamasha hilo siku ya utoaji wa tuzo.

Tamasha hilo linafanyika leo tarehe 9. March. 2013.

Ndikumana

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...