Monday, March 11, 2013

PICHA ZA UHURU KENYATTA NA RUTO KANISANI JANA BAADA YA USHINDI, RUTO ALISHINDWA KUJIZUIA NA IKAWA HIVI



Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Urais nchini Kenya jumamosi iliyopita, jana jumapili march 10 2013 Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria ibada ya kumshukuru Mungu.

Standard Media wameripoti kwamba Rais huyu wa awamu ya nne aliwasili Kanisani huko Gatundu akiwa na ulinzi mkali ambao unalingana na levo yake ya Urais.

 
Vilevile William Ruto ambae ni mgombea mwenza na Uhuru alihudhuria ibada ya kumshukuru Mungu kanisani anakosali jijini Nairobi.

Ruto alimwaga machozi na kushindwa kuongea wakati aliposimama mara ya kwanza mbele ya umati kutoa ushuhuda wa ushindi wao pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuwapigania.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...