Saturday, March 9, 2013

NAKWENDA KUPUMZIKA UARABUNI – STARA.

Stara mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa baada ya muda mwingi wa mihangaiko ya kuuguza na hata kumpoteza mumewe anahitaji kupumzika na kujenga akili upya, katika kulifanya hilo ameamua kwenda kupumzika Uarabuni kwa ajili ya kutuliza akili na kujipanga upya, akiongea na FC amesema kwa sasa anahitaji kupumzika kwa muda.

Stara akiwa na mtoto wake.

Stara akiwa katika pozi

“Nina safari wiki ijayo na kwenda Uarabuni kwa ajili ya kupumzika kisha baadae kuangalia nafanyaje kazi katika staili ipi, kwa sasa itakuwa ngumu kuwepo bila kufanya kazi lakini pia familia imeamua niende huko kama ni sehemu ya kunifariji zaidi kutokana na kipindi hiki kigumu,”anasema Stara.

Lakini mwanadada huyo asiye na makuu ameamua kwenda huko kupmzika kutokana na hali ya filamu ilivyo sasa ambapo watayarishaji wanajikuta wakikikaa kwa muda mrefu wakisotea kazi zao kutoka pasipo na wakati maalum, soko la filamu kwa sasa inasemekana ni gumu kuliko ambavyo jamii inaliona ukiona kazi imetoka sokoni ujue watu wametabika kwa kiwango kikubwa.
.

Stara akiwa katika pozi.

Blog hii inakutakia mapumziko mema na safari yenye Baraka na baadae akirudi arudi na nguvu mpya kwa ajili ya kuendeleza sanaa yetu Bongo

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...