Washiriki wa shindano la Miss Utalii Tanzania Fainali za Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Ukumbi wa Dar Live.
Shindano la Taifa la Miss Utalii Vipaji 2012/13 linafanyika kesho katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, ambapo Warembo 40 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Kanda Maalum vyuo Vikuu Tanzania , watapanda stejini kushindana kucheza Ngoma za asili kutoka Mikoa ambayo wanawakirisha,watapita na mavazi mbalimbali.
Katika shindano hilo mbali na Burudani kutoka kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutakuwa na Burudani zaidi za Ngoma za Asili, Muziki wa kizazi Kipya pamoja na Burudani kutoka kwa Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao, Atakuwepo pia mwanamuziki chipukizi wa Bongo Flava Dogo Genius ambeye ametokea kuwa mpinzani mkubwa wa Dogo Janja na Asley.
Shindano hili ni la awali ambalo litapata Mshindi wa Vipaji kabla ya kufanyika fainali kuu ambalo litampata Miss Utalii Tanzania litakalo Fanyika Tarehe 17.03.2013 katika ukumbi wa Dar Live. Mshindi wa Tuzo hilo la Vipaji atajipatia zawadi ya Kusomeshwa Bure katika ngazi ya Cheti au Diploma kulingana na Sifa zake. Mshindi wa Mwaka jana na ambaye anashikiria taji Hilo kwa sasa ni Daisy Msumbusi Miss Utalii Kutoka Mkoa wa Kagera.
Katika Shindano hilo , ulinzi utakuwa umeimarishwa ambapo kutakuwa na Polisi na Ninja, usalama wa Magari pamoja na vitu vyote utakuwa ni wakutosha, kutakuwa na eneo la kutosha la kuegesha Magari na walinzi muda wote watakuwepo katika eneo hilo.
Viingilio katika Shindano hilo itakuwa kama ifuatavyo, Viti vya kawaida Tsh 5,000 na Viti Maalum 10,000
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Michuzi Media Group,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA)
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Fainali za Taifa 2012/13 wakiwa katika mazoezi ya nguvu ya kujiandaa na Shindano lao la Vipaji ndani ya Ukumbi wa Dar Live.

No comments:
Post a Comment