Saturday, December 15, 2012

MWANAMUZIKI KOFII OLOMIDE AWAKUNA VILIVYO MASHABIKI NA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI JIJINI DAR ES ES SALAAM LEADERS CLUB USIKU WA KUAMKIA LEO



Mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani na kundi lake katika Onesho linalofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo wageni waalikwa na mashabiki mbalimbali walifurika katika viwanja hivvyo , ili waweze kushuhudia shughuli pevu ya mwanamuziki huyo nguli wa muziki Barani Afrika.


Mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide akifanya vitu vyake jukwaani kama anavyoonekana katika picha.
Kofii Olomide akiimba na mmoja wa waimbaji wake Cindy.Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa na mmoja wa waimbaji wake wa kike wakipagawisha mashabiki wa bendi hiyo waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Leaders ili kushuhudia kile anachokifanya jukwaani.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Group akizungumza kumshukuru mwanamuziki Kofii Olomide na mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika onesho hilo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Vimwana wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakimwaga mauno kwa kwenda mbele jukwaani katika onesho hilo.


Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa amezungukwa na vimwana hao ambao ni wanenguajia wa bendi yake huku akiwa katikati yao kama mfalme.

Hapa ni Burudani ya mauno tu kama inavyoonekana madau.
Mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki Kofii Olomide wakifuatilia kwa makini wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
Mashabiki wa mwanamziki Kofii Olomide wakishangilia kwa furaha wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru pamoja na wafanyakazi wengine.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...