Thursday, November 29, 2012

MAMA RAY C AKANUSHA UVUMI ULISAMBAA KUWA RAY C AMEFARIKI......



Usiku wa novemba 27 2012 zilisambaa habari za msanii Ray c zikidai kuwa amefariki dunia.....

Habari hizi ziliwagusa wengi ambao walitaka kujua undani na ukweli wa habari hizo.Ukweli ni kwamba, Ray c ni mzima na anaendelea vizuri na matibabu

Mama Ray c ameamua kuvunja ukimya na kuueleza umma kuwa mwanae ni mzima.Wanaosambaza habari hizo ni adui zake tu.....

“inasikitisha sana kusikia taarifa hizo, Ray C ni mzima kabisa namshukuru Mungu anaendelea vizuri na matibabu tuko nae, anakula vizuri anapata usingizi vizuri, hizo habari zimetoka wapi? nazikanusha kabisa kwa jina la Yesu nalikataa hilo neno” MAMA RAY C


Hivi karibuni, hali ya Msanii Ray c ilibadilika na kuwa tete kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya hali iliyomfanya mama yake aombe msaada kwa wasamalia wema ili kugharamia matibabu yake

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...