Thursday, September 27, 2012

AIRTEL YAZINDUA MINARA YA MAWASILIANO INAYOTUMIA UMEME WA JUA



Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana zaidi imezindua minara yake inayotumia Umeme unao tumia nguvu za nishati ya Jua katika kijiji cha kimande kata ya itunguru mkoani Iringa. Uzinduzi huo ni moja kati ya mikakati ya Airtel kuhakikisha inaendeleza mipango yake ya kupanua upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini kirahisi, kupunguza gharama za uendeshaji na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye minara yake nchini.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande kata ya Itunungu Tarafa ya Pawaga Iringa Vijijini Bw, Andason Mpululu ameushukuuru uongozi wa Airtel kwa kuweza kukabili changamoto za mawasiliano kijijini hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji wa uendeshaji wa biashara mbalimbali hasa za kilimo cha mpunga ambapo hapo awali upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu sana kutokana na kutokua na mawasiliano thabiti kama ilivyo sasa.
“Kwa kupitia Mtandao na huduma ya Airtel money huduma za kifedha zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na kuwawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama nafuu na bila usumbufu wowote. Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola gharama za mawasiliano ya simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa zaidi na kuleta tija kwa wananchi hasa wenye kipato kidogo” alisema bwa Mpululu
Naye mkazi wa kata ya Itunungu bwana Jumanne Zuberi alisema “tunashukuru sana serikali kuwawezesha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel. Hapo zamani upatikanaji wa mawasiliano ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo kuwafanya wakazi wa kijiji hapa kutembea umbali mrefu kupata mawasiliano. Tunashukuru kwa sasa huduma za simu kijini hapa zimeweza kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kuboresha usalama wa raia na mali zetu”.
Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano bw, Jackson Mmbando alisema” nia yetu ni kubadili matumizi ya mafuta ya diesel na generator kuendesha mitambo yetu ya mawasiliano na kutumia umeme wa nishati ya jua ambao utasaidia katika kutunza mazingira na kupunguza gharama za uendeshaji ambazo zitatuwezasha kutoa huduma kwa ufanisi Zaidi na kwa gharama nafuu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi na kusogeza huduma mbambali za kijamii karibu na wananchi zikiwemo huduma za Elimu, Afya na Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi nikulinda huduma hizi na kuzitumia vizuri kwa shughuli za maendeleo vijijini”.
Mawasiliano ndio chachu ya maendeleo hivyo tunaamini kwa kutumia umeme wa jua hata gharama za uendeshaji zitapungua hivyo kuwezesha ktoa huduma zenye viwango vya juu kwa gharama nafuu kwa watumiaji na wateja wa Airtel nchini nzima aliongeza Mmbando”
Kampuni ya Airtel katika kurahisisha mawasiliano nchini inaendelea kufunga mitambo ya umeme wa sola katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya Tanga, Sumbawanga, Kigoma na mikoa mengine mingi. Mpaka sasa Airtel imefanikiwa kufunga mitambo minne inayotumia nguvu za jua katika mkoa wa iringa Iringa vijijini.Mpaka sasa Airtel inaongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana na ina vijiji na miji 50 zaidi.
Wa kwanza ni injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege akitoa ufafafanuzi kwa mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu jinsi mtambo wa mawasiliano uliowekwa na Airtel kijiji hapo unavyofanya kazi ili kurahisisha mawasiliano katika kijiji hicho.Airtel imeanza kufunga mitambo ya mawasiliano itakayotumia nguvu za Nishati ya jua (solar) ili kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijijini, kati ni meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania bw Jackson Mmbando wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na bw Beda Kinunda Meneja wa Mauzo wa airtel Mkoani Iringa wakiwa nje ya Mnara wa Airtel unaotumia nguvu ya Nishati ya jua (solar) wakizungumza na Mwenyekiti wa kijiji cha Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu (shoto) mara baada ya Airtel kuzindua rasmi mnara wa mawasiliano unaotumia nguvu za Solar katika kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani, Airtel imezindua mnara huo unaotumia nishati ya jua kwa lengo la kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijiji ambapo bado hakujafikiwa na umeme wa taifa.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu kuhakikisha wanaweka ulinzi shirikishi kulinda mtambo mpya wa mawasiliano unaotumia nishati ya jua uliowekwa na Airtel ili kufikisha huduma bora ya mawasiliano kijijini hapo, wakwanza kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel Nyanda za juu kusini Bw, Beda Kinunda na kushoto ni Injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege. Hafla ya uzinduzi ilifanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia ni Injinia wa airtel mkoani Iringa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu anaedadisi ili kupata ufafanuzi wa jinsi mnara wa Airtel unaotumia Nishati ya jua (solar) unavyofanya kazi mara baada ya Airtel kuzindua mnara huo kijijini hapo jana. 



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...