Mwaka 1990, mwezi na siku kama ya leo Mrs. Abraham Sepetu ama (Mama Sepetu) alipata bahati ya kujifungua mtoto wa kike ambae alimtunuku jina la Wema Abraham Sepetu, Mtoto ambae Nyota yake ilianza kama masihara tu pale aliposhinda taji la Miss Tanzania 2006, kisha baadae kuingia katika Muvie Industry kama utaniutani vile na ghafla kuwa DIVA wa Tasnia hiyo, na licha tu ya udiva pia kuwa ICON wa Tanzania.Siku hii ya leo ya tarehe 28/09/ anazaliwa upya na kutimiza miaka 22.
Saturday, September 29, 2012
RAIS KIKWETE AAGANA NA MABALOZI WA CUBA NA IRAN.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania aliyemaliza muda wake
AWAMU YA KWANZA YA TANZANIA LIVE MUSIC FESTIVAL YAFANANA
MC wa Tamasha hilo Ben Kinyaiya akiwa jukwaani
AWAMU ya kwanza ya Tamasha la muziki wa dansi lililobatizwa jina la Tanzania Music Festival lililoanza jana katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni limefana baada ya wapenzi wengi wa muziki huo wa kufika kwa wingi kujionea wenyewe burudani hiyo.
Akizungumza na mtandao huu mmoja wa watangazaji wa redio Times ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Sinda Madadi ‘Cnda King’ alisema kuwa amefarjika kuona watu kufika kuwaunga mkono katika juhudi zao hizo za kukuza muziki wa dansi.
Cnda King amewaomba wale ambao hawakufika jana wafike leo Jumamosi kwa ili nao wapate burudani hiyo.
“Naomba nitumie nafasi hii kuwaomba wapenzi wote wa muziki huu kufika kwa wingi leo Jumamosi September 29, 2012 kwa sababu ndiyo siku ya mwisho ya kuazimisha Tamasha hili” alisema Cnda King.
Mtangazaji wa kituo cha Redio One, Salma Dacota mwenye njano akiweka pozi mbele ya kamera huku pembeni akiwa na ‘shostito’ wake
Mtangazaji wa kituo cha Redio One, Salma Dacota mwenye njano akiweka pozi mbele ya kamera huku pembeni akiwa na ‘shostito’ wake
Isha Mashauzi akiwajibika jukwaani
Njemba hii ilibambwa ikizungurusha nyonga kwenda sambamba na mirindimo ya taarabu
Wacha weeeeeee! Mzungu naye hakuwa nyuma kuzungurusha nyonga baada ya kupagawa na burudani ya Mashauzi
Friday, September 28, 2012
Zitto: Asema Ubunge sasa basiiii....!!!!!
MH:ZITTO KABWE
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais.
Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma.
Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.
“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi.
“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.
“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.
“Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.”
Atangaza kugombea urais
Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
“Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.
Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”
“Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto
Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46.
Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.
“Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.
“CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto.
Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.
Habari na Mwananchi
Thursday, September 27, 2012
Jumuiya ya Uingereza- Tanzania yasherekea miaka 50
Siku ya jumanne tarehe 25.9.12 Jumuiya ya Uingereza- Tanzania ( BRITAIN- TANZANIA SOCIETY) iliandaa hafla fupi ya kusherekea miaka 50 ya Utaifa kati ya Nchi ya Uingereza na Tanzania katika ukumbi wa The Royal Commonwealth Club, London. Wageni mbalimbali pamoja na wanachama walijitokeza kwa wingi kuhudhuria hafla hii fupi ilioandaliwa hususani kwa ajili ya kuchangia nchi ya Tanzania. Mojawapo ya wageni waliohudhuria ni pamoja na balozi wetu Peter Kallaghe pamoja na mkewe Mama balozi Joyce Kallaghe, Mwenyekiti wa Britain- Tanzania Society William Fulton JP DL.
Mgeni rasmi katika shughuli hii alikua ni Balozi wa Ubelgiji Mh Dr Diodorus Kamala aliyetoa mada maalum kuhusu mafanikio, maendeleo na changamoto katika nchi ya Tanzania na jumuiya nzima ya Afrika mashariki. Aidha Mh Dr Kamala alifafanua jinsi uchumi wa Tanzania unavyokua kwa kasi kutokana na takwimu kutoka Benki ya Dunia pia aliongelea kuhusu masuala ya utalii, mioundo mbinu, hali ya amani na usalama ambazo zimepelekea wawekezaji wengi kuwekeza katika nchi ya Tanzania. Nchi ya Uingereza ndio nchi pekee inayoongoza katika uwekezaji katika nchi ya Tanzania Ikifuatiwa na India pamoja na Kenya
Pamoja na hayo Mh Dr Kamala aliwashukuru wana jumuiya wa Uingereza- Tanzania kwa kuendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali ili kupambana na hali ya umaskini. Baada ya kutoa mada yake kulikuwa na kipindi kifupi cha maswali na majibu kutoka kwa wanajumuiya pamoja na wadau waliohudhuria.
Nae mwenyekiti wa Computer 4 Afrika ndg Aseri katanga alitoa risala fupi ya kumshukuru mgeni rasmi kwa kujitolea kwake kuja kujumuika na wanajumuiya pamoja na hotuba yake nzuri kuhusu Tanzania.
Vile vile halfa hii ilijumuisha uoneshwaji wa picha zilizochorwa na wachoraji kutoka Tanzania ambazo zilinadiwa ili kuchangisha pesa za kuwasaidia kuwainua wadau wa tasnia ya uchoraji Tanzania. Baadhi ya wachoraji ambazo picha zao zilionyeshwa ni Mmadi Ausiy, Haji Chilonga, Hassan Kadudu, Florian Ludovick Kaija, James Haule na Aggrey Mwasha.
KUMEKUCHA TANZANIA LIVE MUSIC FESTIVAL KESHO.
Mkurugenzi wa Edge Entertainment, waandaaji wa Tanzania Live Music Festival, Edwin John Ngeh akizungumza na Waandishi wa Habari leo asubuhi, viwanja vya Leaders kuhusu tamasha hilo kesho. Wengine kulia kwake ni Charles Baba, kushoto wake, Jacqueline Wolper, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ na Tarcise Masela.
Tamasha la muziki Tanzania, (Tanzania Live Music Festival) linafanyika kesho katika viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam, likishirikisha bendi zaidi ya saba na wasanii wengine mbalimbali.
Bendi hizo ni Sikinde, Msondo, B. Band, Mashujaa Band, Akudo Impact, FM Academia, Mashauzi Classic na Wazee Sugu. Malkia wa mipasho, Khadija Kopa pia atakuwepo.
Timu ya Tamasha kesho
Mwandishi Vicky Kimaro akichukua habari
Timu
Jacqueline Wolper akizungumza na Chalz Baba, wote wakuwepo kesho
Mkurugenzi wa Edge Entertainment, waandaaji wa Tanzania Live Music Festival, Edwin John Ngeh akizungumza na Baba na Jacqueline Wolper
King Kiki akiwa na Bin Zubeiry
Tarcise Masela kushoto akizungumza na Waandishi. kulia King Kiki
Baby Lucas wa Msondo kushoto akizungumza na Waandishi. Kulia kwake ni Ally Jamwaka wa Msondo na Masela
Thabit Abdul wa Mashauzi Classic (kushoto) akizungumza na Waandishi
Banana Zahir Ally Zoro wa B. Band kulia akikzungumza. Kushoto ni Jacque Wolper
King Kiki akizungumza kwa hisia kali. Kushoto ni Masela.
Jamwaka kushoto na Masela kulia
DIMBA TEAM ENZI HIZO; Kutoka kulia Timzo Kalugiwa sasa yupo Habari Leo, Mahmoud Zubeiry, sasa yupo bongostaz.blogspot.com, Elizabeth Mayemba, sasa yupo Majira na Said Makala sasa yupi Channel Ten na Magic FM
Wasanii mbalimbali watakaoshiriki tamasha hilo, leo wamezungumza na Waandishi wa Habari Leaders asubuhi na kuahidi kufanya mambo makubwa kesho.
AIRTEL YAZINDUA MINARA YA MAWASILIANO INAYOTUMIA UMEME WA JUA
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana zaidi imezindua minara yake inayotumia Umeme unao tumia nguvu za nishati ya Jua katika kijiji cha kimande kata ya itunguru mkoani Iringa. Uzinduzi huo ni moja kati ya mikakati ya Airtel kuhakikisha inaendeleza mipango yake ya kupanua upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini kirahisi, kupunguza gharama za uendeshaji na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye minara yake nchini.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande kata ya Itunungu Tarafa ya Pawaga Iringa Vijijini Bw, Andason Mpululu ameushukuuru uongozi wa Airtel kwa kuweza kukabili changamoto za mawasiliano kijijini hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji wa uendeshaji wa biashara mbalimbali hasa za kilimo cha mpunga ambapo hapo awali upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu sana kutokana na kutokua na mawasiliano thabiti kama ilivyo sasa.
“Kwa kupitia Mtandao na huduma ya Airtel money huduma za kifedha zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na kuwawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama nafuu na bila usumbufu wowote. Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola gharama za mawasiliano ya simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa zaidi na kuleta tija kwa wananchi hasa wenye kipato kidogo” alisema bwa Mpululu
Naye mkazi wa kata ya Itunungu bwana Jumanne Zuberi alisema “tunashukuru sana serikali kuwawezesha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel. Hapo zamani upatikanaji wa mawasiliano ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo kuwafanya wakazi wa kijiji hapa kutembea umbali mrefu kupata mawasiliano. Tunashukuru kwa sasa huduma za simu kijini hapa zimeweza kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kuboresha usalama wa raia na mali zetu”.
Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano bw, Jackson Mmbando alisema” nia yetu ni kubadili matumizi ya mafuta ya diesel na generator kuendesha mitambo yetu ya mawasiliano na kutumia umeme wa nishati ya jua ambao utasaidia katika kutunza mazingira na kupunguza gharama za uendeshaji ambazo zitatuwezasha kutoa huduma kwa ufanisi Zaidi na kwa gharama nafuu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi na kusogeza huduma mbambali za kijamii karibu na wananchi zikiwemo huduma za Elimu, Afya na Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi nikulinda huduma hizi na kuzitumia vizuri kwa shughuli za maendeleo vijijini”.
Mawasiliano ndio chachu ya maendeleo hivyo tunaamini kwa kutumia umeme wa jua hata gharama za uendeshaji zitapungua hivyo kuwezesha ktoa huduma zenye viwango vya juu kwa gharama nafuu kwa watumiaji na wateja wa Airtel nchini nzima aliongeza Mmbando”
Kampuni ya Airtel katika kurahisisha mawasiliano nchini inaendelea kufunga mitambo ya umeme wa sola katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya Tanga, Sumbawanga, Kigoma na mikoa mengine mingi. Mpaka sasa Airtel imefanikiwa kufunga mitambo minne inayotumia nguvu za jua katika mkoa wa iringa Iringa vijijini.Mpaka sasa Airtel inaongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana na ina vijiji na miji 50 zaidi.
Wa kwanza ni injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege akitoa ufafafanuzi kwa mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu jinsi mtambo wa mawasiliano uliowekwa na Airtel kijiji hapo unavyofanya kazi ili kurahisisha mawasiliano katika kijiji hicho.Airtel imeanza kufunga mitambo ya mawasiliano itakayotumia nguvu za Nishati ya jua (solar) ili kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijijini, kati ni meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania bw Jackson Mmbando wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na bw Beda Kinunda Meneja wa Mauzo wa airtel Mkoani Iringa wakiwa nje ya Mnara wa Airtel unaotumia nguvu ya Nishati ya jua (solar) wakizungumza na Mwenyekiti wa kijiji cha Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu (shoto) mara baada ya Airtel kuzindua rasmi mnara wa mawasiliano unaotumia nguvu za Solar katika kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani, Airtel imezindua mnara huo unaotumia nishati ya jua kwa lengo la kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijiji ambapo bado hakujafikiwa na umeme wa taifa.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu kuhakikisha wanaweka ulinzi shirikishi kulinda mtambo mpya wa mawasiliano unaotumia nishati ya jua uliowekwa na Airtel ili kufikisha huduma bora ya mawasiliano kijijini hapo, wakwanza kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel Nyanda za juu kusini Bw, Beda Kinunda na kushoto ni Injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege. Hafla ya uzinduzi ilifanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia ni Injinia wa airtel mkoani Iringa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu anaedadisi ili kupata ufafanuzi wa jinsi mnara wa Airtel unaotumia Nishati ya jua (solar) unavyofanya kazi mara baada ya Airtel kuzindua mnara huo kijijini hapo jana.
Wednesday, September 26, 2012
RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAOFISA WA JWTZ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO.
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na walioapishwa leo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa leo mara baada ya hafla fupi ya kuwaapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati).
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa waandamizi wanawake wa JWTZ leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali Lilian Kingazi (Kulia) na Meja Jenerali Grace Mwakipunda (kulia).
Subscribe to:
Posts (Atom)