Washiriki Miss Dar Inter College, nani ataibuka mshindi leo? Twendeni tukashuhudie

Dina 'Dodo'
HAYAWI hayawi, hatimaye yamekuwa- shindano la Miss Dar Inter College 2012 linatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa Makumbusho, katikati ya Jiji karibu kabisa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), likisindikizwa na burudani ya Mfalme wa
Bongo Fleva, Nassib Abdul au Diamond Platinum.
Diamond ambaye imeelezwa leo atatinga na mkoko wake mpya wa ‘bei chafu’ alioununua hivi karibuni katika shoo hiyo, ili mashabiki wake wauone kwa macho yao makavu, amepania kufanya mambo baab kubwa leo Miss Dar Inter College 2012.
Shindano hilo, litakaloshirikisha mabinti wenye upeo wa hali ya juu kutokana na ukweli kwamba wanatoka vyuoni, mbali na burudani ya Mfalme wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, pia litapambwa na burudani ya bendi mpya ya muziki wa dansi inayokuja juu hivi sasa, Skylight.

Diamond atatinga na mkoko huu leo; umewahi kuuona live?
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail Mkingiye ‘Dodo’, amesema maandalizi kwa ujumla yanaendelea vizuri na warembo 14 watakaoshiriki shindano hilo leo watafanyiwa usaili
Dar es Salaam
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Inter College anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania,” alisema.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati taji la Miss Inter College linashikiliwa na binti kutoka IFM, Rose Msuya.
Warembo wawili wa Inter College walishiriki fainali za Miss Tanzania mwaka jana na kufanya vizuri, mbali na Rose mwingine ni mshindi wake wa pili, Blessing Ngowi.
Dina aliyewahi kuandikia pia magazeti ya Majira, Spoti Starehe na kutangazia Radio Times, aliwataja warembo wanaoshiriki shindano hilo kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacqueline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Redd’s Premium, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Clouds Media Group blog za Michuzi, Dina Ismail, BIN ZUBEIRY, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
Moja ya vitu watavayoonyesha jukwaani leo ni shoo hii; kwa nini ukose?

No comments:
Post a Comment