Tuesday, March 13, 2012

ZIJUWE FAIDA NA HASARA ZA KUTAIRIWA...


Je ni muhimu kutahiriwa? (samahani kwa wale ambao nitakuwa nawakwaza kwa hili somo)

Ukianza kujadili issue ya wanaume kutahiriwa huwa ngumu kama vile kujadili mambo ya siasa na dini.
Wapo watu wenye kukereketwa sana na suala la kutahiriwa na wengine hawana maoni kabisa na hawaoni umuhimu wowote.
Ukweli ni kwamba suala la kutahiriwa ni maamuzi ya wawili mke na mume waliokubaliana kuoana na kuishi pamoja na kufurahia maisha ya ndoa yao, iwe kutahiriwa au kutotahiriwa.
Kwani suala la kutahiriwa limeweka misingi zaidi katika dini na tamaduni za watu kuliko masuala ya Medical.
Kutahiriwa ni nini?
Kutahiri (circumcision) ni neno la kilatini linalotokana na maneno mawili yaani circum (lenye maana ya mzunguko) na ccedere (lenye maana ya kukata)
Hivyo basi kutahiri ni kukata mzunguko wa ngozi iliyo mbele ya uume.
Kutahiri ni suala la mila na dini na hakuna ubaya wa kutahiriwa na hakuna ubaya wa kutotahiriwa.
Ni lini mwanaume hutahiriwa?
Kutahiri kwa kawaida kunafanyika wakati watoto wa kiume wakiwa na umri mdogo.
Katika baadhi ya mila za Kiafrika, kutahiriwa kunafanyika mvulana anapobalehe na inakuwa kama sehemu ya mafunzo ya jandoni, anapokuwa mwanamume halisi, yaani mtu mzima.
Wanaume wengine huja kutahiriwa baada ya kushauriana na wachumba zao kabla ya kuoana.

Zipi ni baadhi ya faida za kutahiriwa

Usafi na kuepuka magonjwa ya kuambukiza kama vile urinary tract infections (UTI).
Pia inaaminika wanaume ambao wametahiriwa huweza kupunguza maambukizo ya HIV/AIDS (asilimia ndogo sana kama, kutahiriwa si kinga ya kuambukizwa UKIMWI)
Pia wanaume waliotahiriwa huweza kupunguza uwezekano wa kuugua aina ya cancer (penile)
Hupunguza uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa.
Faida za kuwa na uume usiotahiriwa.
Uume huonekana mrefu zaidi kuliko ule ambao umetahiriwa hivyo kujisikia raha hasa katika suala zima la kumsisimua mwanamke (penetrative sex).
Katika asili, ngozi inayofunika uume (gomvi) husaidia kuzuia sehemu ya ndani ya uume kupata michubuko na kukauka na kupata contamination na kutahiriwa hupunguza hisia (sexual sensation, pleasure, fulfilment) wakati wa sex.
Ngozi inayoondolewa (govi) husaidia kupisha damu kuzunguka vizuri kwenye uume hasa wakati wa sex hivyo kuiondoa ni kuharibu utendaji wa uume.
Je, mwanaume kutahiriwa husababisha kuchelewa kufika kileleni?
Utafiti unaonesha mwanaume aliyetahiriwa uume wake haupo sensitive sana hivyo huweza kuchelewa kufika mapema (ejaculation) ukilinganisha na yule ambaye hajatahiriwa.
Pia mwanaume aliyetahiriwa huweza kumkuna vizuri mwanamke kwa kuwa rim (mzunguko ulio chini ya kichwa cha uume) hutoa msuguano mzuri wakati wa tendo la ndoa.
NA: MKUBWA KAMBI

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...