Friday, March 16, 2012

MKAZI WA MUHEZA TANGA ARAMBISHWA MIL.30 ZA NANI MKALI WA AIRTEL


Mshindi wa millioni 30 wa droo ya Nani Mkali wa Airtel, Abdi Mohamed akiongea mara baada ya kukabidhiwa shillingi millioni 30 muda mfupi baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa promosheni ya Nani Mkali (kutoka kushoto), ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na Afisa Mahusiano wa Airtel Dangio Kaniki.

Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akimkabidhi mshindi wa milioni 30 wa promosheni ya Nani Mkali Bwana Abdi Mohamed muda mfupi baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa mwenzi katika promosheni ya Nani mkali inayoendelea kuwapa wateja wa Airtel nafasi ya kujishindia pesa taslim.

Ofisi Mawasiliano wa Airtel  Dangio Kaniki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa kumkabidhi mshindi wa promosheni ya Nani Mkali ambapo Abdi Ibrahim Mohamed wa Muheza Tanga aliibuka mshindi wa kitita cha milioni 30.

 
KAMPUNI  ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imemzawadia mshindi wa kwanza wa mwenzi wa promosheni ya "Nani Mkali" Bwana Mkali Abdi Ibrahim Mohamed mkazi wa Muheza Tanga pesa taslimu shilling milioni 30.

Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Ofisa Mawasiliano wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema" leo tunayofuraha kumtangaza mshindi wa mwenzi wa shilingi million 30 bwana Mkali Abdi Ibrahim Mohamed ambaye amejishindia katika promsheni yetu inayoendelea ya nani Mkali. Kama mnavyofahamu tumekuwa tukitangaza washindi wa siku na wa wiki, Airtel bado inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali".

Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, ili kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu
sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.aliongeza Kaniki.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo Bwana Abdi Ibrahim Mohamed alisema" nachukua fulsa hii kuwashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuanzisha promosheni hii na najisikia furaha kuibuka Mkali wa Airtel na kujishindia pesa taslimu shilling milion30 leo hii.

Napenda kutoa wito kwa wateja wa Airtel kushiriki na wale ambao hawajajiunga kushiriki na kuibuka washindi kama nilivyojishindia leo, kila mmoja ananafasi ya kushiriki na Kushinda kama mimi nimeshinda toka Tanga wilayani muheza hii inaonyesha wazi kuwa nafasi ipo kubwa
kwa kila mtanzania Kushinda awe wa mjini au vijijini.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...