MKONGWE wa miondoko ya muziki wa dansi nchini,…
MKONGWE wa miondoko ya muziki wa dansi nchini, Hamza Kalala ‘Komandoo Kalala’, hatimaye amebeba jukumu la kukifua kikundi cha Twanga Academy, ambacho kilianzishwa hivi karibuni na uongozi wa ASET. Kikundi hicho kwa sasa kinafanyia mazoezi yake katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Asha Baraka alisema walikaa kama kamati ya Ofisi za ASET na kuona mtu pekee anayeweza kuwafundisha vijana hao ni Komandoo Kalala hivyo wakamuita na kumpatia jukumu hilo.
“Tulikaa na tukapendekeza kwa pamoja kuwa Komandoo Kalala ndiye mwanamuziki pekee anayeweza kutukuzia vipaji hivi kutokana na uzoefu wake wa siku nyingi katika muziki huu”, alisema Asha Baraka.
No comments:
Post a Comment