Wednesday, February 22, 2012

PEDESHEE WEMA ATUA  BONGO BAADA YA KUFANYA  SHOPPING YA MILIONI 45 DUBAI

 Wema Sepetu akiwa kwenye pozi siku chache alipokuwa ameenda kufanya shopping  Dubai

Msanii machachali ndani ya chimbo la filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu 'Pedeshee Wema,' ambaye pia ni miss Tanzania 2006/007, mapema jana alitua nchini akitokea katika falme za kiarabu mjini Dubai alikoenda kwaajili ya mapumziko ya siku ya wapendanao 'Valentine Day' na kufanikisha mahemezi ya mavazi yake ya kila siku na vitu vingine vidogo vidogo vya familia yake.
Wema anadai kuteketeza zaidi ya milioni 41, katika shopping hiyo na sasa amelejea kujenga heshi yake kama ilivyo ada.
Gazeti la risasi lilibahatika kupata baadhi ya vifaa na ngu alizonunua akiwa huko Dubai, so kwa picha na habari zaidi tembelea mtandao wa www.globalpublishers.info

 
Wema Sepetu wa enzi hizo...


SHOPPING YA GHARIMU ZAIDI YA SHILINGI MIL. 45
Habari zilizosambaa kwenye mitandao mingi ya burudani na kijamii ndani na nje ya Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, zilisema kuwa Wema siyo wa bei ndogo tena baada ya kumwaga mamilioni ya fedha kwa ajili ya shopping iliyodaiwa kugharimu dola za Kimarekani 40,000 (zaidi ya Sh. milioni 45 za madafu).
AFIKIA HOTELI YA NYOTA TANO
Katika habari hiyo, Wema aliyefikia katika hoteli ya nyota tano ya DXB mjini humo, alipiga picha akiwa kwenye moja ya maduka ya kistaa akinunua bidhaa za bei mbaya zikiwemo pafyumu, dhahabu, viatu na mazagazaga mengine.
MSHANGAO
“Inavyoonekana mwanadafada Wema siku hizi baada ya kuachana na Almasi (msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’), amekuwa akijiachia na kufanya matanuzi ambayo duh! Amekuwa mtu wa shopping hapa home na sasa yuko zake Dubai kwa ajili ya shopping na matembezi kidogo,” ilisomeka sehemu ya habari hiyo ikiambatanishwa na picha.

MASWALI TATA
“Najaribu kutafakari ni kazi gani anayofanya Wema siku hizi ambayo imekuwa ikimlipa hadi anafuja fedha kiasi hiki? Maana zile pesa ni zaidi ya milioni 45, tena ni kama milioni sitini na pesa hivi...ni hela nyingi sana! Je, ni filamu tu au kuna kingine?” alihoji mmoja wa watu aliyesoma habari hiyo ambapo maswali ya sampuli hiyo yalikuwa mengi.

WEMA PEDESHEE?
Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ulibaini kuwa, mbali na gari la Sh. milioni 35, aina ya Toyota Lexus Hybrid Harrier analosukuma mnyange huyo baada ya kusota na teksi kwa muda mrefu, pia amekuwa akituza wanamuziki wanapokuwa stejini katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar es Salaam.
Katika utetezi wake, Wema aliliambia gazeti pacha na hili, Risasi Jumamosi kuwa, gari analoendesha alinunuliwa na familia yake kama zawadi baada ya kuachana na Diamond.
Achilia mbali gari na shopping za kufuru, pia Wema anaishi kwenye nyumba ya kifahari aliyopangisha maeneo ya Makumbusho Mwanayamala jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...