Saturday, June 27, 2015

WEMA KUBADILI WANAUME CHANZO NI HIKI


1Wema Sepetu na Nangari.
Mwandishi wetu
IMEBAINIKA! Kufuatia tabia yake ya kubadili wanaume, mrembo asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Isaac Sepetu imefahamika kuwa chanzo cha yote ni kusumbuliwa na ugonjwa ujulikanao kitaalamu kwa jina la Sex Maniac.
Wema-na-Diamond (1)Wema Sepetu na Diamond.
Akizungumza na gazeti hili, mtaalam wa masuala ya utabiri na nyota, Maalim Hassan Yahya alisema kwamba suala la Wema kubadili wanaume kila mara si kulogwa bali anasumbuliwa na ugonjwa huo ambao mtu akiwa nao kila wakati anawaza mapenzi na raha yake ni kufanya tendo la ndoa.
wemanacharlesbabaWema Sepetu na Chaz Baba.
Maalim alidadavua kwamba, ugonjwa huo hautibiwa na dawa za hospitali kama magonjwa mengine ila kama mtu anahitaji kuondokana na tatizo hilo anatakiwa kumtafuta mwanasaikolojia ambaye mara kwa mara atakuwa anamjenga kwa ushauri hadi atakapoona amekuwa sawa kwa kuacha kuwaza mambo hayo.
TBT-Wema-na-KanumbaWema Sepetu na Steven Kanumba.
“Watu wanashindwa kuelewa, unakuta mtu anakuwa na wanaume wengi, anabadili kila mara alafu watu wanamsema bila kujua kwamba ni ugonjwa ambao mtu anajikuta akipenda ngono kila wakati na kwenye mawazo yake anatawaliwa na kutamani tendo la ndoa tu.
IMG_0131Wema Sepetu  na Bob Juniour.
“Lakini wapo wengine wanabadili mabwana maarufu ili nao wawe maarufu,” alisema Maalim.
WemaJumbeWema Sepetu na Jumbe.
Wema aliwahi kutoka kimapenzi na wanaume tofauti akiwemo, Herry Samir ‘Mr. Blue’, Khaleed Mohamed ‘TID’, marehemu Steven Kanumba, Yusuf Jumbe, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, CK na Nagari Kombo.
Jitihada za kumpata Wema ili kuzungumzia hali hiyo ziligonga mwamba baada ya simu yake kutokuwa hewani na kukosekana nyumbani kwake hivyo jitihada zinaendelea.

Thursday, June 25, 2015

BANZA: MNANIUA SANA JAMANI

banza Mwanamuziki nguli wa dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
Gladness Mallya
BAADA ya uvumi kuzagaa mtaani kwamba mwanamuziki wa dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefariki dunia, Banza amesema amechoshwa na watu kumuua sana.
Baada ya uvumi huo, ndugu zake wamesema watu waache kumuua kwa maneno kwani bado yupo hai.
BANZA2‘Banza Stone’ akiwa katika ofisi za Global Publishers (Picha na Maktaba).
Ndungu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Hamis, alisema uzushi wa kifo cha Banza umewasumbua sana kwani watu mbalimbali walikuwa wakipiga simu na wengine kufika nyumbani jambo ambalo lilimuumiza sana Banza japokuwa anaumwa lakini akawa analalamika kwa nini watu wanamuua kwa maneno na si mara moja kutokea.
“Jamani yupo hai japokuwa anaumwa lakini anaongea tatizo lipo kwenye kusimama na kula, watu waache uzushi kwani wanamuumiza zaidi kwa uzushi wao huo,” alisema Hamis.

MSANII BONGO MUVI AIKIMBIA NYUMBA

Bozii (1) Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu `Bozi’ akihamisha vitu vyake.
Mayasa Mariwata na Gladness Mallya
MAJANGA! Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu `Bozi’ amejikuta akifungasha virago na kuhama kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Kinondoni jijini Dar kutokana na mjengo huo kutawaliwa na mauzauza yanayosadikiwa kuwa ya kishirikina.
Bozii (4)….Akiendelea kutoa vitu vyake.
Chanzo makini kilicho jirani na nyumba aliyokuwa akiishi mwanadada huyo kilieleza kuwa, baada ya kuvumilia vimbwanga vya kishirikina ameamua kuondoka.
Bozii (2)“Hii nyumba wapangaji huwa hawadumu kwa kushindwa kustahimili wanayoyaona sijui ina balaa gani, tunashangaa yeye ameweza kukaa kwa mwaka mzima na kuvumilia majanga yote, inataka moyo.

LINAH AJIWEKA KWA KAKA’AKE ZARI

LinahStaa wa Muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga ‘Linah’ akiwa ameketi na William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.
Musa Mateja
MREMBO anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’ kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.IMG-20150602-WA0025 Ndani ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, paparazi wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini hapo.
Linah1Linah na Boss Mtoto katika pozi la kimahaba.Mbali na kunaswa siku hiyo, pia paparazi wetu amekuwa akiwashuhudia mara kadhaa wawili hao wakiwa pamoja katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar.

VIFO MASTAA KUTIKISA UPYA!

MSHTUKO! Wakati wimbi la wasanii Bongo likizidi kuwa kubwa katika kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, mtabiri maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein amefunguka mazito juu ya vifo vya mastaa hao kutikisa upya huku wale watakaosalia wakipata nafasi za uongozi.
steveveeStaa wa bongo movie Steven Mangele ‘Steve Nyerere’.
TUJIUNGE MAGOMENI-MWEMBECHAI
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Magomeni-Mwembechai jijini Dar, mapema wiki hii, mtabiri huyo alisema kuwa, mwaka huu kinyota ni wa mafanikio makubwa kwa wasanii lakini pia vifo navyo vitakuwa vingi kwao.
Wema-SepetuMiss tanzania 2006 na muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu.
NI MWAKA WAO KINYOTA
Alisema kwamba, kwa wale watakaosalimika huku wakiwa wamejiingiza kwenye kinyang’anyiro cha kugombea uongozi wa kisiasa, wote watafanikiwa kwa kuwa mwaka huu ni wao.
Maalim alisema kuwa, mwaka huu kinyota ni wao ndiyo maana wamejitokeza wengi kwenye kuwania nafasi hizo tofauti na vipindi vingine vya uchaguzi vilivyopita.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...