Monday, June 24, 2013

IKULU YA MAREKANI YAWEKA NJE RATIBA YA OBAMA KUJA TANZANIA



Rais Barrack Obama
IKULU ya Marekani na Idara ya Habari (Maelezo), wametangaza ratiba ya Rais Barrack Obama atakapozuru Tanzania huku ikionyesha kuwa atakaa siku mbili tu, kuanzia Julai Mosi na kuondoka kesho yake.

Tanzania itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika kutembelewa na Obama baada ya Senegal na Afrika Kusini. Mara atakapowasili na ndege yake kubwa ya Air Force One, Rais Obama atazindua barabara mpya katika upande wa Mashariki wa geti la kuingia Ikulu.
Rais Obama, ambaye atafuatana mkewe Michelle pia siku hiyohiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika na Marekani kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam. “Pia amepanga kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,” ilisema taarifa ya Maelezo.
Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa atakayoandaliwa Ikulu na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete. Siku itakayofuata ataweka shada la maua kwenye sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu waliofariki katika shambulizi la bomu mwaka 1998. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion na atatoa hotuba akizungumzia mikakati ya Marekani ya kulisaidia Bara la Afrika kuzalisha nishati ya umeme.

“Tanzania ni mshirika muhimu wa Marekani,” alisema Ofisa wa Ikulu ya Marekani, Ben Rhodes wakati alipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki katika Ikulu ya Marekani kuhusu ratiba ya ziara ya Obama barani Afrika.
Pia mke wa Obama atakuwa na ratiba yake. Julai Mosi, atapata staftahi na mwenyeji wake, Salma Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Dar es Salaam.
Pia atatembelea sehemu ubalozi wa zamani wa Marekani na baadaye atashuhudia onyesho la utamaduni la Kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho kinajumuisha watoto wa mitaani wenye umri kuanzia miaka mitano hadi 18 kwenye Makumbusho ya Taifa. Julai 2, atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.

NGONO KINYUME NA MAUMBILE ZAONGEZEKA TANZANIA ....WENGI WAO WANAFANYA KUONDOA MIKOSI



Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Nchini (Tacaids) imesema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa vitendo vya ngono kinyume na maumbile vinazidi kuongezeka.

Hayo yalisemwa jana na Dk. William Kafura, katika mkutano wa sita wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (Tapac).

Alisema hiyo inatokana na imani za kishirikina kwamba wakifanya vitendo hivyo watapata bahati kwa kupandishwa vyeo.

“Lazima tukubali tatizo lipo na tulitafutie suluhisho, utafiti upo umefanywa na Muhimbili, umefanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam, umefanywa na Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,”alisema.

Alisema pia wafanyabiashara wanaamini kwa kufanya vitendo hivyo watajirika wakati wanawake wanaamini kuwa watazidi kupendwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho, alisema utafiti uliofanyika nchini unabainisha kuwa wanawake hawana uelewa wa kutosha juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi.

Akizungumzia suala la kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho alisema kuwa wanaume wana uelewa mkubwa zaidi kuhusu ugonjwa huo kuliko wanawake.Hata hivyo, alisema kwa sasa ipo kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kuwataka wabunge na viongozi mbalimbali kutoa elimu juu ya kujikinga na gonjwa hatari la ukimwi.

Aidha Mrisho alisema kuwa kwa sasa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa asilimia 14.8 ambapo Unguja Kaskazini inamaambukizi madogo kwa asilimia 0.1.

Hata hivyo alisema kuwa kuna changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo ni pamoja na rasilimali za ukimwi kwa serikali, mashirika ya Dini na sekta binafsi kuwa pungufu kuliko mahitaji.

Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto lakini nia ni kufikia sifuri tatu ifikapo mwaka 2015 na hiyo hipo katika ulimwenguni, Afrika hapa hapa Tanzania.

MAAJABU: MTOTO AZALIWA NA MAKALIO MATATU, MAMA YAKE ALIA AKIOMBA MSAADA



Maajabu ya uumbaji yamemfanya mama mzazi wa Xiao Wei ambaye ni mchina amwage machozi akiomba msaada wa kunusuru maisha ya mwanae mwenye umri wa miezi 7 aliyezaliwa na makalio matatu...
Kalio la tatu lipo kama mkia mfupi, wenye urefu wa sentimita 8 ( 8 cm ), katikati ya makalio mengine mawili.

Akiongea kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo amedai kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiwaomba madaktari wafanye upasuaji wa tako hilo lakini wao wamekuwa wakimjibu kuwa hiyo si kazi nyepesi kama anavyodhani....

"Tukilikata litaota tena, hivyo hatutakiwi kukurupuka na badala yake tutakiwa kupata muda wa kupitia vitu vingi ukiwemo mrija wa uti wa mgongo ambapo kalio hilo limejiegesha"...Alisema daktari mmoja akimjibu mama huyo

OMMY DIMPOZI ALIVYOPIGWA CHUPA NA MAWE AKIWA STEJINI NA KUKATISHA SHOW YAKE MJINI DODOMA


JuziA DODOMA katika show ya Kilimanjaro Ommy Dimpoz na madansa wake wamejikuta wakiambulia kupigwa mawe na chupa jukwaani, hali iliyowafanya walikimbie jukwaa...
Pamoja na kupigwa mawe na makopo, jamaa walijikaza kisabuni mpaka baunsa akaamua kuwatoa jukwaani ili kunusuru roho zao.
Kisa cha kupigwa mawe nkinatokana na tusi la Ommy Dimpoz kwa marehem Ngwea...

MAKUBWA HAYA, HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYE OA WANAUME WAWILI. SOMA HAPA



MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia blog hii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.
Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa kwenye blog. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...