Mwana muziki ambae anafanya poa sana kwenye game ya Bongo fleva hapa nchini Tanzania muite Ney wa mitego a.k.a True boy leo ameamua kufunguka kwa wasanii wenzake ambao wametokea kudis wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Diamond unaitwa "Muziki Gani" Ney amewachana hiviii "Najua ni kwanini wanasema hivyo mimi huwa naongea ukweli siku zote, wana hip hop sikuzote ni wanafiki na wanamajungu, iko hivyo na ndiyo wasanii siku zote wako na shida hawana maendeleo. kwa sababu ya majungu yao, mimi sitaki kubishananao kwanza najua hawajielewi, hawajui huu ni muziki na hii ni biashara, mwisho wa siku mtu ambae upeo wake ni mfupi kiasi hicho inabidi tuachanenae, Wasanii wa Hip hop hivyo na wao ndo wamejenga matabaka ya Bongo fleva na Hip hop, kwa sababu muziki wetu ulikuwa ni Bongo fleva, wooote ni Bongo fleva haijalishi huu ukiwa unaiba, huu ni wanini mladi ukiwa unatumia tu kiswahili ni wa bongo fleva, angalia hao wasanii wanobisha wako na maisha gani wako na maendeleo gani, soo me sina time nao wajipange tuu" alisema Ney wamitego.

Filamu ya Ray of Hope iliyoshinda tuzo za Africa Magic. Filamu ya Kitanzania ijulikanayo kwa jina la “The Ray of Hope” iliyotengenezwa na kampuni ya Pilipili Entertainment imeshinda tuzo ya filamu bora iliyotumia lugha asili ya Kiswahili katika tamasha la Tuzo za Watazamaji wa Afrika Magic “Africa Magic Viewer’s Award.” .
Pastor Myamba mmoja ya washiriki filamu ya Ray of Hope.
Joyce Fisoo Katibu wa Bodi ya Filamu alikuwa jaji katika tuzo hizo. Akizungumza wakati wa mahojiano jana jijini Dar es salaam Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Bi.Joyce Fissoo amesema ushindi wa tuzo hiyo ni Heshima kwa nchi na inatoa hamasa kwa waigizaji wa filamu nchi. “Tuzo hii ni heshima kwa nchi kwa sababu inaonyesha filamu zetu zinaweza kufikia kiwango cha kimataifa,na filamu zote zilikuwa zimekaguliwa nakupewa madaraja.”Alisema Bi. Fissoo. Aidha Bi.Fissoo amesema tuzo hizo ni changamoto kwa wasanii na watengeneza filamu nchini kutumia fursa zinazojitokeza kushiriki katika matamasha makubwa na tuzo mbalimbali za kimataifa ili kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine jinsi wanavyoweza kutengeneza filamu zenye ubora. .
Filamu ya Ray of hope iliyoshinda tuzo.
Hashim Kambi mshiriki katika filamu ya Ray of Hope iliyoshinda tuzo. Tuzo hizo zilifanyika hivi karibuni jijini Lagos, nchini Nigeria ambapo filamu 110 zilizotengenezwa na makampuni 43 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ziliingia kwenye kinyanganyiro na tuzo 28 zilitolewa kutoka makundi 26. Aidha filamu hizo zilikaguliwa na majaji tisa kutoka nchi za Ghana, Cameroon, Kenya ,Nigeria, Afrika kusini, Uganda na Zambia pamoja na Tanzania iliyowakilishwa na Katibu wa bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo. Bi Fissoo amesema Tuzo hizo ni za kwanza kufanyika na zilifunguliwa na Waziri wa Gesi na Mafuta wa nchini Nigeria aliyemwakilisha rais Goodluck Jonathan ,viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Uwekezaji na Waziri wa Utamaduni na Utalii. Vilevile tuzo hizo zilipambwa na bendi za muziki na waimbaji mbalimbali kama Femi Kuti, Tiwa Savage , Iyanya pamoja na kundi la Sauti Soul kutoka Kenya.
KATIKA kile kilichoonekana ni kuikomalia ndoa ya msanii wa filamu Bongo Irene Uwoya, baadhi ya wadau nchini Rwanda wameendelea kutambua kuwa yeye ni mke halali wa msakata kabumbu, Hamad Ndikumana ‘Kataut’. Hayo yalibainika hivi karibuni baada ya Uwoya, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Jacob ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ kutua nchini humo kuhudhuria utoaji wa tuzo za filamu zilizopewa jina la Rwanda Movies Awards. Wakiwa Rwanda, matangazo yaliyokuwa yakirushwa kupitia redio na televisheni yaliainisha kuwa Uwoya ni mke wa Ndikumana, kitendo kilichowashangaza wasanii hao.
Akizungumza na hivi karibuni, mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, inavyoonekana Wanyarwanda wengi hawataki kuamini kuwa ndoa ya Uwoya na Ndiku haipo na ndiyo maana wameikomalia. “Katika matangazo yaliyokuwa yakisikika katika redio na televisheni, jina lililokuwa linatajwa ni Oprah umugore wa Kataut, wakimaanisha Oprah mke wa Kataut. “Jina la Oprah kwa Uwoya limekuwa maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha yeye, Ray na marehemu Kanumba,” kilieleza chanzo hicho.
MSANII wa filamu na muziki mwenye mvuto wa aina yake Snura Mushi ‘Snura’, ameamua kutoa la moyoni kwa madai kuwa sasa anatafuta mwanaume wa kuweza kufunga naye pingu za maisha lakini kwanza kabisa akubali kumpa muda mrefu wa kutafuta pesa ili asiwe tegemezi baada ya kuingia ndani ya ndoa hiyo. Kauli ya msanii huyu imekuja mara baada ya mwandishi wetu kumswalika maswali kadhaa kuhusiana na mikakati ya maisha yake ya muziki na mahusiano ..... Akiongea kwa mbwembwe, Snura alidai si kwamba hataki kuolewa bali hataki kuishi ndani ya ndoa na kuwa tegemezi kwa mwanaume. “Sitaki kuishi na mwanaume kabla hajakubali kunipa muda wa mimi kutafuta pesa... Najua anaweza kuwa na uwezo wa kila kitu lakini hivyo vyote vitakuwa vya kwake na mimi natakiwa kuwa na mali zangu, lakini bila hivyo nitazeekea kwangu,” alisema.