Thursday, July 2, 2015

DIAMOND AKIRI KUMPENDA OMOTOLA

Mwandishi wetu
KING wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametengeneza kichwa cha habari nchini Nigeria baada ya kufunguka kuwa anampenda ‘vibaya’ staa wa filamu nchini humo, Omotola Jalade Ekeinde, Ijumaa lina stori kamili.
King wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond katika ziara ya kimuziki iitwayo ‘Nana Tour’ nchini humo, staa huyo ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mjasiamali maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekuwa akiumizwa na penzi la Omotola kitambo sana lakini hakuwahi kuzungumza katika vyombo vya habari.

OMOTOLA_NdaniTV_Daniel-Sync-PHOTOS-13-Edited-1Staa wa Nollywood nchini Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde ‘Omotola’.
“Diamond ana maumbo yake flani hivi amazing ambayo huwa anayapenda, siku nyingi sana kabla hata hajakutana na Zari, alikuwa akituambia watu wake wa karibu kwamba miongoni mwa wanawake mastaa ambao anawatamani awaweke kwenye himaya ya penzi lake ni Omotola.
“Alisema anampenda kwa kila kitu kuanzia ufanyaji kazi wake, umbo lake na hata umaarufu mkubwa alionao ndani na nje ya Bara la Afrika,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kueleza habari hiyo, mapema wiki hii, mtandao wa nigeriafilms.com ulithibitisha maneno hayo kwa kuposti habari iliyobainisha Diamond anampenda Omotola sanjari na mastaa wengine wawili wa Nigeria anaovutiwa nao kimapenzi.
Akiwa hewani alipokuwa akihojiwa na redio moja jijini Lagos, Diamond aliweka bayana kuwa anateswa na penzi la mastaa watatu Nigeria, Omotola, Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji.
“Jamaa kitambo sana anateswa na penzi la Omotola sasa leo kaongeza na wengine wawili na ninavyomjua hashindwi kufanya kweli ingawa nina wasiwasi kwa Omotola na Tonto maana wana waume zao labda ajiweke kwa Genevieve ambaye hajaolewa,” kilikazia chanzo chetu.Diamond hakupatikana ili kusikia kauli yake juu ya ishu hiyo.

LULU AMWAGA MINOTI KWENYE PATI!

Waandishi wetu
ULE msemo wa ‘pata pesa tuone tabia yako’ huenda ni kweli, kufuatia staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ambaye siku hizi anaitwa ‘tajiri mtoto’ kutokana na kuwa na fedha na kumwaga ‘minoti’ (pesa) kwenye pati, Ijumaa ‘Kubwa’ lilikuwepo.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa shushushu wetu, ishu nzima ilijiri usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye pati ya ‘bethidei’ ya mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Hamza ‘Kalala Junior’ iliyofanyika ndani ya ukumbi wa hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano iliyopo Masaki jijini Dar ambapo mastaa na mapedeshee kibao wa ‘mujini’ walihudhuria.
LULU AMWAGA MINOTI
Ilielezwa kwamba, Lulu alifanya ‘kufuru’ hiyo baada ya waalikwa wa pati hiyo kumaliza kula na kunywa ambapo ikafika wakati ratiba ikaelekeza watu kutoa zawadi kwa kadiri watakavyojisikia au kujaliwa nacho.
Ndipo Lulu ambaye siku hizi amekuwa hapendi kujitokeza kwenye shughuli, alipita mbele na kuanza kumpa noti nyekundu ‘Msimbazi’ aliyekuwa akizikusanya kwa niaba ya Kalala Junior kwa staili ya moja-moja.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akihesabu minoti.
Shuhuda wetu alidadavua kuwa, kila aliponyoosha mkono kutoa Msimbazi mmoja, watu walimkodolea macho wakiamini hawezi kufika ‘kilo moja’ (Sh. 100,000).
MANENO YA WATU
“Lulu bwana, anajitutumua tu. Hawezi kumpa laki moja Kalala Junior. Kwanza sidhani kama siku hizi ana pesa za kufanyia fujo,” alisema mwalikwa mmoja, mwenzake akampinga.“Wee! Lulu siku hizi ana pesa. Wenzake wanamuita tajiri mtoto. Ndiyo maana ana jeuri ile,” alisema mwingine miongoni mwa waalikwa hao.
Hata hivyo, Ijumaa halikuweza kufuatilia noti hizo katika mtiririko wa kutoka ili kujua ni shilingi ngapi bali baada ya kumaliza, lilimfuata Lulu ili kumuuliza ambapo hakuwa tayari kutoa ushirikiano.
Mtu wa karibu na Lulu ambaye aliomba jina lihifadhiwe, aliliambia Ijumaa kuwa, Lulu siku hiyo alitenga shilingi milioni moja na laki nne (1,400,000) kwa ajili ya kumtuza Kalala Junior tu.“Hawezi kusema, lakini mimi ninavyojua alitenga milioni moja na laki nne. Lulu kwa sasa yuko vizuri kipesa,” alisema mtu huyo na kuachana na Ijumaa.
KWA NINI LULU ALITOA KIASI HICHO CHA PESA KWA KALALA JUNIOR?
Habari za ndani zinasema kuwa, Lulu aliamua kumwaga mkwanja huo kwa vile, mwanamuziki huyo kwa sasa ni mpenzi wa shoga kipenzi wa Lulu, Rose Alphonce ‘Muna’.
Wakati wa matatizo ya Lulu kuswekwa Magereza ya Segerea, Dar kwa madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Muna ndiye aliyebeba jukumu la kumpelekea chakula mahabusu huyo kila siku.
Lakini pia, Lulu alipotoka gerezani kwa dhamana, alikwenda kuishi kwa muda nyumbani kwa Muna, Mwananyamala jijini Dar.
MAPEDESHEE NAO
Baada ya Lulu kumaliza kutuza minoti yake, mapedeshee waliokuwa ukumbini humo nao walicharuka ambapo walichomoa minoti yao na kuimwaga kwenye maboksi mawili na kutolewa ukumbini hapo na wapambe.
KUMBE KALALA ALIFANYIWA SAPRAIZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya ukumbi huo, Kalala Junior akiwa hajui chochote, mpenzi wake huyo ambaye pia ni msanii wa filamu, alimtaka watoke kwa ajili ya kupata chakula cha jioni ambapo walikwenda kwenye hoteli hiyo.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Kalala Hamza ‘Kalala Junior’.
Baada ya kufika, Kalala alipokelewa na watu waliokuwa ukumbini hapo huku wakimmwagia maji, bia na soda hadi akawa chapachapa huku wakimwimbia nyimbo za ‘hepi bethidei tu yuuu…’ jambo ambalo hakulitegemea.
Kutokana na kulowa chapachapa, Muna alimchukua hadi kwenye chumba alichochukua mapema ndani ya hoteli hiyo ambapo alimbadilisha nguo.
Muna alimvalisha Kalala suti yenye gharama ya shilingi 2,800,000, viatu vya shilingi 800,000 (inadaiwa ni vya kutoka Italia), vyote hivyo alivinunua mwanadada huyo ikiwa ni zawadi kwa mpenzi wake.
Wawili hao walirudi ukumbini ambako walipokelewa kwa shangwe huku mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ akiwa ni mshehereshaji (MC) wa shughuli hiyo ambayo kwa kuangalia tu iligharimu mamilioni ya shilingi.
KALALA AMFUNGUKIA MUNA
Kufuatia mbwembwe hizo za Muna, Kalala alitumia nafasi hiyo kumtambulisha rasmi kwamba ndiye mchumba’ke wa sasa na kumshukuru kwa kumwandalia sherehe kubwa na ya gharama kwani hakuwahi kufanyiwa hapo awali.
MAIMARTHA ATIA NENO
Naye mshereheshaji wa shughuli hiyo, Maimatha aliliambia gazeti hili kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ya aina yake na yeye alilipwa zaidi ya shilingi milioni moja.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS

WASTARA: NAMPA BOND NAFASI YA KUNIOA

WASTARA Juma Issa Abeid amekiri kuzidiwa na hisia za kuwa na mwenza kutokana na ukweli kwamba damu yake bado changa, hivyo suala la kuolewa halikwepeki huku akimpa nafasi kubwa msanii mwenzake, Bond Bin Sinan endapo atakidhi vigezo na masharti.

Wastara Juma Issa Abeid akiwa na Bond.
Akifungulia ‘koki’ ya maneno mbele ya paparazi wetu kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii, Wastara ambaye kwa sasa yuko bize kusaka ubunge nyumbani kwao Morogoro Vijijini, alisema hawezi kudanganya kwamba ataishi bila kuwa na mume kwa kuwa amekamilika kimaumbile.
“Mimi ni mwanamke, nimekamilika tena nakula na ninashiba. Damu bado changa. Nikisema siwezi kuolewa, nitakuwa nadanganya. Nimekaa muda mrefu kwa sababu kila mwanaume anayenihitaji ananitamani tu.

“Bond namuona ni mwelewa. Lakini nimempa sharti la kutonigusa hadi siku ya ndoa. Kama atakidhi na hayo mengine ambayo ni siri yetu, niko tayari kuolewa naye,” alisema Wastara.

HOFU MTOTO WA ZARI KUFIA TUMBONI

zariMpenzi wa sasa wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ .
STORI: MWANDISHI WETU
HABARI ya mjini kwa sasa ni mjadala mzito mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba, mpenzi wa sasa wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anaweza kumuua motto aliye tumboni kutokana na tabia yake ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu (high hills) katika kipindi hiki cha ujauzito.
PhotoGrid_1429005202683Diamond Platnumz akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.
WALICHOKISEMA MASHABIKI
Baadhi ya mashabiki, hasa watoto wa mjini wanaosadikiwa kuwa na mapenzi makubwa na Miss Tanzania 2006 aliye pia nyota wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu (Team Wema), ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond, wamemnanga Zari wakisema kuvaa kwake high hills ‘kokoko’ kunaweza kumminya tumbo wakati wa kutembea hivyo kukifanya kitoto hicho kufia tumboni.
DOKTA AZUNGUMZA, AFAFANUA
Kufuatia madai hayo mazito, juzi Amani lilizungumza na daktari maarufu jijini Dar, Godfrey Chale ‘Dokta Chale’ ambaye alilazimika kueleza kuhusu madai hayo.
Amani: “Samahani dokta, tumelazimika kukutafuta kutokana na maneno yaliyosambaa kwa sasa hapa mjini. Diamond ana mpenzi wake ni mjamzito. Sasa pamoja na ujauzito wake, anavaa viatu virefu.
“Kwa hiyo wanamnanga kwamba anaweza kukiua kitoto kilichopo tumboni kwa sababu anapovaa viatu hivyo, misuli ya
miguu inakaza na anabana tumbo. Kuna ukweli?”
Dokta: “Kwanza kabisa siyo kweli. Mwanamke anapovaa viatu virefu wakati wa ujauzito hakusababishi mtoto tumboni kufa.
“Ila, inashauriwa wajawazito
wasiwe wanavaa viatu virefu kwa sababu, wanapovaa, wanatanua misuli na kujiongezea uzito. Kwa hiyo inakuwa kama mtu aliyebeba mzigo kichwani huku akiwa na mimba.”
ATAJA MAGONJWA YANAYOMKABILI ZARI
Dokta Chale aliendelea kuweka wazi kuwa, mjamzito anapopendelea kuvaa viatu virefu, akishajifungua na mwili ukapoa, atakabiliwa na magonjwa manne.
“Kwanza ataugua miguu. Pili, atasumbuliwa na matatizo kwenye visigino. Tatu atapata matatizo ya magoti na nne ataugua mgongo. Ndiyo maana unaweza kukuta mwanamke anakuwa mrembo, miguu mizuri lakini kama alikuwa akibeba mizigo au kuvaa viatu virefu wakati wa mimba, miguu inaota nyama kwa nyuma ‘kiazi’.”
AONDOA HOFU
“Kwa hiyo, kama jamii ina hofu kwamba huyo mjamzito atamuua mtoto aliye tumboni kwa sababu ya kuvaa viatu virefu, hofu hiyo iondoke bali yazingatiwe hayo matatizo manne niliyoyasema,” alisema daktari huyo.
KWA WANAWAKE WOTE
“Lakini madhara haya si kwa wajawazito tu. Utafiti wa kitaalam umegundua kuwa, mwanamke ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku. Kwa hiyo kuvaa viatu vyenye visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa zaidi. Sasa utaona madhara ya kutembea hatua 10,000. Hii haijalishi anayetumia gari.
“Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya kwenye miguu, kiuno, mgongo na shingoni kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito. Kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino,” alimalizia dokta huyo.
DIAMOND ALIVYOSEMA
Amani, juzi lilimtafuta Diamond kwa njia ya mtandao wake wa WhatsApp na kumuuliza anachukuliaje madai ya ‘wabaya’ wa Zari:
“Hao wapo tu. Unajua dunia hii ukishakuwa maarufu kila jambo litakuandama. Lakini mimi naangalia mbele zaidi, nini nafanya na nini nitafanya. Kama maneno hata kwenye kanga yapo.”

TUWAONEE HURUMA - LAKE ZONE ALL STARS (NEW AUDIO)

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...