Monday, March 25, 2013

CHID BENZ " AMTANDIKA MAKOFI " NGWAIR


Mkali wa vina na mashairi kutoka pande za Ilala anayefahamika kwa jina maarufu la 'Chid Benz' ameanza kupata sifa mbaya baada ya kumpiga mwanamuziki mwenzake 'Ngwea' nje ya ukumbi wa Ambassador Lounge ulioko kwenye jengo la Benjamini Mkapa tower Posta usiku wa kuamkia Machi 22.

Kupigwa kwa 'Ngwea' kulikuja baada ya 'Chid' kumzingua 'Dully' alipokua akiingia ambapo mwisho wake aliamua kuondoka.

Alipoondoka 'Dully', 'Ngwea' akamuuliza inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo 'Chid' alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza 'Ngwea', inasemekana 'Ngwea' aliamua kukaa kimya lakini 'Chid' aliendelea kungea kwa hasira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia 'Ngwea'.

'Ngwea' aliamua kuondoka kwenye ukumbi huo lakini alipofika chini ya ghorofa ndipo 'Chid' alipomfuata na kuanza kumshambulia mwanamuziki mwenzake huyo na baadaye kumjeruhi kwa chupa mkononi.


Lakini baada ya hapo 'Ngwea' aliweza kufika hospitali na kuweza kupatiwa matibabu ya jeraha hilo la chupa.

WEMA SEPETU AJITOLEA KUTOA MILIONI 13 KUMUOKOA KAJALA ALIEHUKUMIWA MIAKA MITANO ....









Leo imesomwa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili mcheza filamu za Kitanzania anayefahamika kwa jina la 'Kajala Masanja' na mumewe mbele ya Hakimu 'Sundi Fimbo' kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam.


Katika hukumu hiyo 'Kajala' amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.

Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe 'Faraji Agustino' kukumbwa na makosa ya kutakatisha fedha haramu.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolea mahakamani hapa, mwanadada mwenye michejo mingi hapa Bongo anayefahamika kwa jina la Wema Sepetu' aliweza kujitolea yeye mwenyewe kiasi cha Tsh. milioni 13 kutoka mfukoni mwake kwa ajili ya kumlipia msanii mwenzake wa filamu 'Kajala' asiweze kutumikia adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5 jela.



Hii ni mara ya pili kwa msanii 'Wema Sepetu' kujitolea kiasi kikubwa cha fedha kusaidia msanii mwenzake.!

Thursday, March 21, 2013

NEY WA MITEGO AMNYESHEA MVUA YA MATUSI KWA NIKKI MBISHI


Katika kile kinachoonesha bifu ya Ney wa Mitego na Nikki Mbishi kufikia pabaya, Ney amemmwagia matusi ya nguoni rapper huyo wa ‘Kill Yo Self’ kupitia BBM.

 Bifu la wasanii hao lilianza baada ya Nikki kudaiwa kurekodi wimbo uitwao Ney wa Mitego ambayo anamzungumzia msichana mwenye jina hilo na ambaye ana tabia za ukicheche.
“Nikki Mbishi acha us***ge k***m*yako utaf***a siku si nyingi kwa ambao huyu shoga ni rafiki yao BBM mtajua kwanini naongea hivi. Serious Nikki utaf**ika muda si mrefu unatambia za kike we m***nge nimekuvumilia sana kumbe una tabia sawa na dada yako …!! Jipange,” ameandika Ney.

HUU NDIYO MUONEKANO MPYA WA AGNES MASOGANGE


Mwanadada ambaye ni Video Queen wa bongo na alifanya poa sana katika video ya Belle 9 ya Masogage,na kupewa jina la Agnes Masogange,
huu ndiyo muonekano wake mpya kwa sasa.... check picha zake akiwa katika pozi tofauti tofauti.



Angnes katika poziiii




Agnes Maso gange katika pozi.

MWANAMKE ACHINJWA KAMA MBUZI HUKO KAHAMA



Marehemu Martha Charles baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake. 
 
HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Asack Nzolela (29), mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.

Afande Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja mkewe wakiwa wamelala chumbani kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo alikimbia.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe afanye kazi.

Habari zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.


Marehemu Martha Charles (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake.
 
Edward alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika kutoa msaada.

Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana.

Nao majirani waliokwenda kutoa msaada ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema walikuta mwili wa Martha ukiwa kitandani huku amekatwa na kitu chenye ncha kali katika eneo lote la shingo, ndipo walipomchukua na kumkimbiza hospitali lakini tayari alikuwa ameshakata roho.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Noel Mkisi alisema baada ya muuaji huyo kutoroka usiku huohuo jitihada za kumsaka zilianza.


Isack Nzwalile aliyemchinja mkewe, Martha Charles.

Tukio la kuchinjwa kinyama kwa mwanamke huyo limetokea siku chache baada ya hivi karibuni, mchuna ng’ombe Musa Petro (27) naye kumuua kwa kumchinja kwa kisu mpenzi wake, Jessica Elialinga (19).

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Maduka ya Nyama Kahama, Faraji Mohamed akiongea na mwandishi wetu alisema Petro ni mfanyakazi wa Nzolela katika duka lake la nyama (bucha) ambapo alishangaa kusikia Nzolela amemchinja mke wake kama alivyofanya mfanyakazi wake, Petro.

Wakati tunakwenda mitamboni habari zilizopatikana kutoka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kahama na kudhibitishwa na OCD George Simba zilisema mtuhumiwa huyo amekamatwa.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...