Tuesday, March 5, 2013

DStv REWARDS YAENDELEA KUIBUA MAMILIONEA: AHMED SALIM SALEH ASHINDA Tshs.5,000,000‏



Ahmed Salim Saleh, mshindi wa Tshs, 5,000,000 za DStv Rewards akiwa na uso wa furaha huku ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa.


Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, akiwa na mshindi wa DStv Rewards kwa wiki ya tatu, Ahmed Salim Saleh, baada ya kumkabidhi mfano wa hundi ya kitita cha Tshs. 5,000,000 alichojishindia.


Mshindi wa DStv Rewards, Ahmed Salim Saleh, akisaidiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake kushangilia kwa kuibuka mshindi wa Tshs, 5,000,000 alizoshinda.

Katika muendelezo wa kampeni ya DStv Rewards kampuni ya MultiChoice Tanzania inayo furaha kumtangaza rasmi mshindi wake wa tatu. Mshindi huyo ni Ahmed Salim Saleh, mfanyakazi wa Access Bank ya jijini Dar-es-Salaam.

Kupitia droo ya DStv Rewards, MultiChoice Tanzania inaibua baadhi ya wateja wao kuwa “mamilionea” ambapo katika kila wiki mteja mmoja huibuka mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 5. (Tshs 5,000,000)

DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao.

Kampeni hiyo maalumu ilianza tarehe 5 February, 2013 na inaendelea mpaka tarehe 10 April, 2013. Wateja ambao wanakuwa na nafasi ya kuibuka “mamilionea” ni wale ambao hulipia akaunti zao za DStv kabla hazitajakatwa kwa kulipia kifurushi chochote kati ya DStv Access, DStv Family, DStv Compact, DStv Compact Plus na DStv Premium.

UHURU KENYATTA BADO ANAONGOZA.....



Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia.

Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa!

Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi.

Ukifuatilia mwenendo wa Uchaguzi wa Kenya kuna dalili kuwa Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai anaelekea kwenye kupata ushindi.

Moja ya tafsiri ya jambo hili ni ilivyo kwenye fikra za wapiga kura ambao ni wengi ni watu wa kawaida- kuwa Uhuru anaonewa, hata na mataifa ya nje. Kwamba mambo ya Kenya yao yanaingiliwa pia na wasio Wakenya, tena Wazungu.

Wakenya wana historia ya mapambano magumu ya kudai uhuru kutoka kwa ' Wazungu'- ni tangu enzi za Mau Mau.

Pamoja na utajiri wake, bado Wakenya wengi wa kawaida wanamwona Uhuru kama mtu wanayefanana naye. Ni mwanadamu kama wengine. Huko nyuma Uhuru amekuwa na historia ya matatizo binafsi pia ya kimaisha, ikiwamo matatizo ya pombe, hivyo ya kifamilia pia. Wakenya wengi wanaishi wakijisikia kuwa wananyanyaswa na kuonewa. Wanamwona Uhuru Kenyatta kuwa ni mtu anayeonewa pia.

Hivyo, yawezekana kuna kura za ' kuonewa huruma' ambazo Uhuru Kenyatta anaweza kuzipata, hata kutoka kwa watu wa kabila la Wajaluo. Wanaojiona ' wanafanana naye'.

Na lingine ambalo laweza kutokea ni ukweli, kuwa katika matatizo mengi wanayoyakabili Wakenya kwa sasa, kuna ambao wanaikumbuka ' Bora ya jana' ya Mzee Jommo Kenyatta. Wanaikumbuka historia. hivyo, kuna Wakenya waliopiga kura za ' nostalgie'- Kura za ' Zilipendwa'.

Kuna Wakenya wengi walimpenda Mzee Jommo Kenyatta. Bado wanakumbukumbu za ' Fuata Nyayo'. Na Uhuru naye anaitwa ' Kenyatta'- Jina lake la pili. Ni mwana wa Mzee wa ' Fuata Nyayo.

Naam, Nyayo zilishapotea. Kuna wenye hamu ya kuzitafuta. Wanaamini Uhuru atawasaidia kuziona. Na tusubiri tuone.

"HAZIPITI SIKU MBILI BILA KULIZWA NA KERO ZA WAANDISHI WA HABARI:.....MAMA KANUMBA



Mama  mzazi wa marehemu Steven Kanumba amesema maswali anayoulizwa kila mara na waandishi wa habari hasa za udaku humfanya asipitishe siku mbili bila kulia kutokana na kumkumbuka mwanae kipenzi.

Akiongea na kipindi cha The Avenue cha TBC 1, mama huyo ambaye hivi karibuni amejiingiza kwenye uigizaji wa filamu pia amesema mara nyingi anapofuatwa na waandishi wa habari kumuuliza maswali kuhusiana na mwanae hubaki akilia na waandishi wa habari huishia kuandika habari za uongo tofauti na alivyoongea.

“Kupoteza mtoto wa miaka 28 sio mchezo, inauma,” alisema Mama Kanumba.

Aliongeza kuwa hawezi kuangalia filamu za mwanae kwakuwa humfanya ajisikie vibaya japo nguo zake bado zipo na huziona kila siku.

MTOTO ALIYEZALIWA NA VIRUSI VYA UKIMWI APONA...



Wanasayansi wametangaza kuwa mtoto aliyekuwa amezaliwa na virusi vinavyosababisha Ukimwi amepona na hana tena virusi hivyo.

Mtoto huyo wa huko Mississippi nchini Marekani amekuwa akitumia dawa kwa mwaka sasa na haoneshi kuwa na maambukizi hayo tena.

Hata hivyo hakuna uhakika asilimia 100 kuwa mtoto huyo amepona kabisa lakini vipimo vya hali ya juu vimetoka kumpima na haoneshi kuwa na virusi tena.

Habari hii inaweza kuwa mwanzo wa kupatikana tiba ya ugonjwa huo unaosababisha vifo vya watu wengi hususan barani Afrika.

Saturday, March 2, 2013

BETHIDEI YA LADNAA YAVUTIA MASTAA KIBAO

Jacqueline Wolper (kushoto), akimlisha keki Ladnaa kwenye Bethidei yake.
Ladnaa akiwa na keki yake.
Steve Nyerere akilishwa keki.
Mama mzazi wa Diamond (kushoto), akilishwa keki hiyo.
Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule (kushoto), akilishwa keki.
Ladnaa akimwagiwa Shampeni na mmoja wa wageni wake.
Snura akinogesha sherehe hiyo kuchezesha makalio.
Snura akitimua mbio baada ya kumaliza kutoa burudani mahali hapo.
Nay wa Mitego akiwa katika pozi na Ladnaa.
Beny Kinyaiya pia alikuwepo.
Yussuf Mlela akiwa katika pozi na Ladnaa.
Wasanii wa kundi la Makomandoo wakiwa katika pozi na Ladnaa.
Baaadhi ya waalikwa wakipiga makofi wakati wa kuimba wimbo wa bethidei hiyo. BETHIDEI ya aliyewahi kuwa mtangazaji wa EATV katika kipindi cha Friday Night Live, Ladnaa, ilifana vya kutosha juzi ilipofanyika
ndani ya Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na mastaa kibao.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...