Wednesday, February 27, 2013

*MSD YAWEKA WAZI WANAOWALINDA WANAOTOROSHA DAWA NJE YA NCHI


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti z\ilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini.

Meneja wa Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi ikiwemo Cameroon.
Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati ya usajili wa maduka ya dawa baridi vijijini wakati wa kongamano hilo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO

Monday, February 25, 2013

PICHA: PENZI LA DIAMOND NA PENNY SIO SIRI TENA!








tagazo

MCHUNGAJI ALIYEKUBALI KUWATAHIRI WATOTO WAKE ARUSHA AVULIWA NGUO ZOTE NA KUCHAPWA VIBOKO



Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo katika kata ya Ngusero mkoani Arusha aliyedhalilishwa na vijana wa jamii ya kifugaji kwa kuvuliwa nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na kisha kutandikwa viboko amesema atanunua bunduki na kuitumia kuua endapo Serikali haitachukua hatua.

Mchungaji huyo alifanyiwa udhalilishaji huo hivi karibuni baada ya kuwatahiri wanawe katika hospitali ya Kiteto, jambo ambalo vijana wa jamii hiyo walisema ni kosa kwa kwenda kinyume na mila na desturi ya kuwatahiri kimila, na hivyo kumvua nguo, kumchapa, kumpiga na kumjeruhi.

Mchungaji huyo anasema aliripoti shambulio hilo katika kituo cha polisi na amekuwa akifuatilia lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya vijana hao wala kuulinda usalama wake ikiwa ni pamoja na kuenedelea kupewa vitisho. 
habari/picha:mpekuzi blog

ODAMA ASEMA ,,,,SITEGEMEI MWANAUME KAZI NDIO KILA KITU KWANGU



Jenifa kyaka (Odama)



Mwanadada nyota kutoka bongo movie Jenifa Kyaka Odama amefunguka na kusema katika maisha yake hategemei wanaume na ndio siri ya mafanikio aliyo nayo kwa sasa

Mwanadada huyo amesema anashukuru Mungu kwa kila hatua anayopiga na kwa sasa amejipanga kuhakikisha anafanya vizuri sana katika tasnia hii ya filamu hapa nchini.


Odama amekanusha vikali uvumi uliozagaa kuwa mambo yote anayofananya ni msaada kutoka kwa pedeshee flan hapa mjini na badala amesema kila kinachoonekana ni juhudi zake binafsi na hakuna mkono wa mwanaume unajua watu wakimuona mwanamke kafanikiwa wanadhani ni nguvu ya mwanaume kiukweli hili huwa linaniumiza sana na ndio sababu tosha inayonifanya nisonge kila kukicha.


Hapa akikagua camera

Mwana dada Odama ameendelea kusema kuwa anajua anachokifanya hivyo haoni sababu ya kuongozwa na mtu mwingine,
Amesema anafanya kazi kwa bidii sana na ndio maana alisafiri kwenda china kwa ajili ya mahitaji ya kampuni yake ya J-FILIM 4 LIFE Ambayo imeshatengeza filamu kibao zinazofanya vyema sana dukani kwa sasa


Odama ametoa wito kwa wasanii wachanga na hata mastaa kuwa hakuna kitu kizuri kama kujituma kwani unapofanya kazi kwa bidii basi jua pesa zitamiminika tu ila ukikaa na kupiga domo basi utaishia domo kwani pesa zinatafutwa na hazitutafuti sisi..Nachoshauri kina dada wenzangu tufanye kazi tukikaa na kusema bila vitendo tutabaki kilalamika kila siku maana hakuna kitu kibaya na adui wa pesa kama uvivu.Odama alizidi kutiririka na kusema kama kuna wanawake haswa mastaa wenye tabia za kuwa tegemezi waache kwani siku wakigombana wajue ndio mwisho wa kupata pesa ila ukiwa na chako huwezi kuteseka.


Akiendelea kununua

Kwa sasa mwanadada huyu amesema anajipanga na atafanya fila kubwa na ya historia ambayo itakayotumia gharama kubwa sana kwa wengi wawatakaoshiriki watatoka nje ya nchi bila kufafanua nchi gani na wanaotoka nje wanakuja kama wasanii au crew.

Kwasasa Odama anamiliki biashara zake na ana mipango kibao ambayo itakamilika muda si mrefu kama mungu akitujalia na kila mtu atajua Odama anataka kufanya
Wakizungumza na sisi kwa nyakati tofauti mashabiki wa filamu wamesema wanamkubali sana mwandada huyu kwani anakwepa sana kuandikwa kwa habari za uwongo pili wanamkubali kwani ni mwanadada mpiganaji mwenye ndoto kubwa sana za maisha bora.


Hapa akikagua stick ya boom

Odama amefunguka kuwa ana amini filamu aliyoifanya na kuwashirikisha Riyama Ally, Cath na wasanii wengine wengi itafanya vizuri sana sokoni kwani ni filamu nzuri na ina mafunzo na ana amini itapendwa sana kwani watu waliocheza wamefanya vizuri sana

SIMBA YAKATWA MKIA NA MTIBWA SUGAR, YAFUNGWA 1-0



Kikosi cha Simba kilichoanza katika mchezo wa leo.

Kikosi cha Mtibwa Sugar.

Mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba akichuana na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaban Nditi.


Wachezaji wa akiba wa Simba wakiwa hawaamini macho yao wakati jahazi la timu hiyo likiwa linazama

Golikipa wa Mtibwa Sugar, Hussein Shariff akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mtibwa imeshinda bao 1-0.

Waamuzi wa mchezo wa jana wakitoka uwanjani
Kocha wa Simba, Patrick Liewig akitoka uwanjani baada ya mchezo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...