Monday, September 3, 2012

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LAITIKISA SHINYANGA, WAKAZI WAKE WAKIRI WAZI HAKUNAGA KAMA FIESTA

Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop kutoka Serengeti Super Nyota, Young Killer, akiwajibika jukwaani, katika tamasha la Serengeti Fiesta, 2012, katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere juzi, mjini Shinyanga.


Mashabiki wakifuatilia kwa ukaribu tamasha la Serengeti Fiesta, Shinyanga usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Kambarage.

Mwimbaji Winfirda Josephat Recho akiwajibika jukwaani usiku wa kuamkia leo, katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani Shinyanga, katika Uwanja wa Kambarage.

Mwimbaji wa muziki wa mduara, IT akionyesha manjonjo yake katika tamasha la Serengeti Fiesta, lililofanyika mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo.

Mashabiki wakifurahia burudani kutoka katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani Shinyanga.

Profesa Jay akifanya vitu vyake katika uwanja wa Kambarage, mkoani Shinyanga, katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Msanii Ommy Dimpozi, akicheza na shabiki wake.

Msanii Ney wa Mitego akikamua katika tamasha la Serengeti Fiesta.

Msanii Barnabas akijibu mapigo kwa shabiki wake, kwenye tamasha la Serengeti Fiesta, lililofanyika usiku wa kuamkia leo, mkoani Shinyanga.

Mh Temba akiwapa mikono mashabiki wake katika tamasha la Serengeti Fiesta.

Mtangazaji wa Clouds TV, Antonio Nugaz, akitangaza washindi wawili wa pikipiki zinazotolewa na kamuni ya Push Mobile.

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma akifanya vitu vyake uwanjani hapo, katika tamasha la Serengeti Fiesta.

Waimbaji wa kundi la Wanaume Family, Mh Temba, Chege na Bibi Cheka wakifanya vitu vyao katika tamasha la Serengeti Fiesta.

Msanii Ommy Dimpozi akiimba mbele ya mashabiki wake.

Mashabiki wakifurahia burudani za Serengeti Fiesta mkoaani Shinyanga.

Mashabki wakipata burudani za Serengetu Fiesta mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa kambarage.

SIMBA KUKIPIGA NA SOFAPAKA ALHAMISI DAR ES SALAAM.


Simba SC

BAADA ya mwezi na zaidi wa kuwa kambini nje ya Dar es Salaam, Alhamisi wiki hii wapenzi wa Simba SC watapata fursa ya kuiona tena timu yao ikicheza mbele ya mechi yao, itakapomenyana na waliowahi kuwa mabingwa wa Kenya, Sofapaka FC Uwanja wa Taifa.
Msemaji wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga ‘Mr. Liverpool’ amesema leo kwamba, mechi hiyo itakuwa ya mwisho kabla ya kucheza na Azam FC, Septemba 11, mwaka huu katika mechi ya Ngao ya Jamii.
Kamwaga alisema kwamba Simba itarejea kesho Dar es Salaam na kuendelea na mazoezi katika Uwanja wa Sigara, Chang’ombe ikisubiri kukipiga na Azam FC.
Kwa sasa kiwango cha Simba, inayofundishwa na Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick, akisaidiwa na Mganda, Richard Hamatre, kipo vizuri na timu inaonekana iko tayari kwa Ligi Kuu. Pamoja na jana kulazimishwa sare ya 1-1 na Sony Sugar ya Kenya, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, lakini Simba ilicheza soka safi na washambuliaji wake walikosa mabao ya wazi zaidi ya matano.
Lakini hata hali mbaya ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika eneo la kuchezea inachangia kupunguza idadi ya mabao kwa Simba.
Katika mechi tatu ambazo Simba imecheza kwenye Uwanja huo, imevuna mabao matano na kufungwa matatu, na kikwazo kimekuwa kikionekana ni hali ya eneo la kuchezea.
Katika mchezo wa jana, bao la Simba lilifungwa na Daniel Akuffo, wakati Komabil Keita alijifunga katika jitihada za kuokoa na kuwapa Wakenya bao la kusawazisha.
Awali, Simba ilicheza mechi mbili Arusha, dhidi ya Mathare United ya Kenya na JKT Oljoro ya Arusha, ambazo zote ilishinda 2-1, mshambuliaji mpya Daniel Akuffo kutoka Ghana akifunga bao moja kila mechi, Kiggi Makaasy na Mrisho Ngassa wakifunga mabao mengine.
Kitu moja tu ambacho Milovan anapaswa kuendelea kufanyia kazi ni makosa ya safu ya ulinzi na mawasiliano duni na makipa wao.
Ilivyo sasa kipa yeyote anayesimama kwenye lango la Simba SC, kabla ya kuchunga wachezaji wa timu pinzani, anakuwa na jukumu la kwanza la kujihadhari na mabeki wake wasimfunge, kwani mabeki wote wa kati wa timu hiyo wamekwishaonyesha ‘kipaji cha kujifunga’ katika mechi za karibuni, Juma Nyosso, Paschal Ochieng na Komabil Keita.
Simba inajiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambayo kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kukutanisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0.


MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI AFARIKI DUNIA KWENYE VURUGU ZA BAINA YA WAFUASI WA CHADEMA NA POLISI KATIKA KIJIJI CHA NYOLOLO, MUFINDI IRINGA


Daudi Mwangosi
  Daud Mwangosi ameuwawa jana katika vurugu za Polisi na wafuasi wa CHADEMA katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa.

Mwangosi aliuawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za CHADEMA Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.

Kabla ya kuuawa kwa mwanahabari huyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadaye mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini.

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa CHADEMA kurushiana mawe kwa mabomu, zaidi ya magari matano ya CHADEMA na ya wananchi yameharibiwa, huku watu kadhaa wakiachwa wamejeruhiwa hali mwanahabari mmoja, Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya. 

  
Marehemu Daud Mwangosi (kulia) akiwa kazini dakika 20 kabla ya mauti kumfika.
 
Mwandosi akiwa katikati ya polisi kabla ya kifo chake.



Saturday, September 1, 2012

WAKAZI WA MUSOMA WAKUNWA VILIVYO NA UJIO WA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012

Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma. 
Kati ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma. 
Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mwasiti akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
Mmoja wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Rachel (kushoto), akionyesha uwezo wake katika uwanja wa Karume mjini Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 na wanenguaji wake.
Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AKIWA KWENYE MKUTANO IRAN


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Dk. Mohammad Reza Rahimi, walipokutana jana mjini Tehran na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliohudhuri Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na Upande wowote uliomalizika jana mjini Tehran, Iran.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...