Saturday, January 30, 2016

YANGA SC.YACHEZEA KICHAPO CHA MABAO 2-0 DHIDI YA COASTAL UNION TANGA!

Kikosi cha timu ya Yanga SC, kikiwa katika picha ya pamoja mapema kabla ya mchezo huo kuanza, ambapo wamechezea kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa timu ya Coastal Union ndani ya uwanja wa Mkwakwani Tanga jioni ya leo.
Wachezaji wa timu ya Coastal Union wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mchezo wao dhidi ya Yanga kuanza.
Beki wa kushoto wa timu ya Yanga, Oscar Joshua, akipambana na mmoja wa walinzi wa timu ya Coastal Union.
Mashabiki wa timu ya Coasta Union ya Tanga wakishangilia bao lao la pili.

SIMBA YAIKANDAMIZA 4-0 AFRICAN SPORTS YA TANGA


Klabu ya Simba imeendelea kuzikimbiza Yanga na Azam katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu baada ya kufanikiwa kuichapa African Sports kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya ligi hiyo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Hamisi Kiiza ameibuka shujaa wa mchezo huo akifanikiwa kuweka bao mbili kambani ndani ya kipindi cha kwanza huku bao la tatu ndani ya kipindi cha kwanza likifungwa na Hasan Kessy.Beki wa African Sports (kushoto) akimdhibiti Ibrahim Ajib wakati wa mchezo wa Simba vs African Sports
Bao la ushindi la mnyama wa Msimbazi limekwamishwa wavuni na Haji Ugando na kukamilisha kalamu ya mabao kwa siku ya leo.
Matumaini ya Simba kuibuka kidedea kwa kutwaa ndoo ya ligi msimu huu yameibuka baada ya mtani wao Yanga kukwama jijini Tanga mbele ya Coastal Union kwa kipigo cha bao 2-0. Azam ambao leo wangecheza na Tanzania Prisons hawapo nchini hivyo mchezo huo umeahirishwa hadi hapo watakaporejea nchini.
Yanga bado wanaongoza ligi wakiwa na pointi 36, Azam wako nafasi ya pili kwa pointi 36 sawa na Yanga lakini wao wanafaida ya mchezo mmoja mkononi ambao walitakiwa wacheze leo.
Matokeo hayo yanaiingiza Simba kwenye orodha ya timu ambazo zinawania ubingwa msimu huu kutokana na tofauti ya pointi lakini bado kuna mechi nyingi ambazo zinaweza zikaamua nani ataibuka bingwa wa msimu huu.
Jackson Mayanja ambaye anashikilia nafasi ya kocha mkuu kwa muda tangu kutimuliwa kwa Dylan Kerr ameendelea kufurahia ushindi ndani ya klabu hiyo kwani ameshinda mechi zote ambazo ameingoza Simba.

Friday, January 29, 2016

MBWANA SAMATTA AKABIDHIWA JEZI ATAKAYOITUMIA RASMI KATIKA KLABU YA KRC GENK UBELGIJI


Viongozi wa Klabu ya KRC Genk wakimtambulisha Samatta.

BOSI wa TP Mazembe, Moise Katumbi, amemfuata straika wake, Mbwana Samatta nchini Ubelgiji ili kuweka mambo sawa ili mchezaji huyo ajiunge na Klabu ya KRC Genk.
Samatta alitangulia kwenda Ubelgiji ambako alifika juzi Alhamisi na kukutana na wakala wake ambaye walianza kukamilisha taratibu za mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo, lakini Samatta, jana alitambulishwa rasmi klabuni hapo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na nusu.
Katumbi yeye anawasili Ubelgiji, leo Jumamosi kuungana na Samatta na wakala wake kukamilisha baadhi ya mambo licha usajili wa mchezaji huyo kuwa umekamilika.
“Katumbi amefika leo (jana) na alijiunga na Samatta kukamilisha mambo ya msingi na viongozi wa Genk na mambo yapo sawa, yaani Samatta ni mali ya Genk,” alisema ofisa huyo.
Tovuti ya Genk pia iliandika jana kuwa, Samatta tayari ni mchezaji wao na anaweza kutumika muda wowote.
Awali Katumbi alionekana hataki Samatta ajiunge na Genk kutokana na klabu hiyo kutotumia njia sahihi katika kumsainisha mkataba wa awali bila kuwasiliana na TP Mazembe.

Q-CHILLAH KUTAMBULISHA BENDI YAKE KESHO NDANI YA BILICANAS

Q-Chillah akicheza na mashabiki zake kwenye moja ya maonesho yake ya nyuma.
BAADA ya kuutumikia Muziki wa Bongo Fleva kwa muda mrefu, mkongwe Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ ametangaza kuibuka na bendi itakayofahamika kwa jina la QS International.
Akizungumza na gazeti hili, Januari 26, mwaka huu, Chillah alisema Jumapili hii ametangaza hali ya hatari kwa wasanii wote kwa kuzindua bendi hiyo katika Ukumbi wa Bilcanas, Posta jijini Dar ambapo itakuwa ikipiga muziki mchanganyiko kila wiki kwa ratiba itakayotangazwa hapo baadaye.

Msanii wa Bongo Fleva ‘Q-Chillah akiwa katika pozi’.
“Nimejipanga sana kuja kivingine kwani hapo mwanzo nimekuwa nikijitahidi kadiri ya uwezo wangu ili nirudi katika Bongo Fleva lakini mambo yalikuwa magumu, namshukuru Mungu kwa sasa nimepata kampuni mpya ya kusimamia kazi zangu za muziki ya QS Mhonda J Group of Company ambayo imenipa vifaa vya bendi.

“Kwenye bendi hii nitakuwa na M-Dog na wanamuziki wengine kibao yaani jumla na wapiga vyombo tunaweza kufikia hata kumi, nimejipanga kufanya vitu vizuri kwani nimefanya uchunguzi wa kina katika bendi nyingi maarufu za hapa nchini kuna upungufu mkubwa hivyo nitaufanyia kazi,” alisema Q-Chillah.
Q-Chillah anayetamba na Wimbo wa Mkungu wa Ndizi, kwenye utambulisho wake huo anatarajia kusindikizwa na wasanii kama Chaz Baba, Juma Nature, Bushoke, Abdul Misambano na Banana Zorro.

VOGUE LAMTOKEA PUANI WEMA SEPETU,TRA WAMTAITI ALIONA CHUNGU!


Wema Sepetu (wa pili kutoka kulia), akipekuliwa na baadhi ya maafisa wa TRA baada ya kumkamata akiwa na gari lake jipya na kumhitaji aonyeshe vibari vya gari hilo jambo lililozua kizaa zaa.


MAMA Coming Soon  Wema Isaac Sepetu  kwa mara nyingine ametengeneza kichwa cha habari, safari hii amewekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kuendesha gari aina ya Range Rover Evogue bila kuwa na vibali, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.

Tukio hilo lililodumu kwa takriban saa tatu lilijiri Jumanne iliyopita maeneo ya Aficana, Mbezi Beach jijini Dar wakati mrembo huyo alipokuwa ‘kiguu na njia’ kwenda kwenye bethidei ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Kibadude.
Gari lake lililokamatwa na  maofisa wa TRA
NI LILE ALILODAI KUJIZAWADIA

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichokuwepo eneo la tukio, gari hilo alilokamatwa nalo Madam ni lile alilojizawadia kwa mbwembwe nyingi mwishoni mwa mwaka jana katika siku yake ya kuzaliwa ambalo lina thamani ya shilingi milioni 200 za Kibongo.

“Nimepiga picha. Wamemtaiti hapa Mbezi Africana, naona maofisa wa TRA wanamhoji. Lina tatizo katika uhalali wa kuingia nchini. Hapa sasa naona wanaomhenyesha ile mbaya. Si kawaida.”
Wema akiwashuhudia kwa pepembeni maafisa hao baada ya kumng'ang'ania.

AMWAGA CHOZI

“Sasa namuona Madam machozi yanamtoka yenyewe… anahaha, mara aende huku mara kule. Nahisi so litakuwa limemkalia vibaya maana kila simu anayopiga hapati msaada,” kilinyetisha chanzo hicho.
Ukaguzi ukiendelea
TRA WABAINI FIGISUFIGISU

Gazeti hili lilizungumza na ofisa mmoja wa TRA ambaye alikuwepo kwenye tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa mamlaka hiyo aliweka wazi kuwa, walibaini figisufigisu katika gari hilo.

“Hili gari ni moja kati ya magari ambayo yanaingia nchini kutokea nchi ya Msumbiji. Hata namba zake za usajili zinaonesha hivyo. Sasa huwa yanakatiwa vibali vya miezi mitatu au kulipiwa ushuru na kununuliwa. Liliingia nchini tangu mwaka jana.

“Tumekuta halina vibali maana vibali vya miezi mitatu vimeisha, tumemuuliza atoe nyaraka za gari, anasema zipo nyumbani, tukamwambia twende huko nyumbani ukazitoe, akabadili lugha, akasema anazo Steve (Nyerere). Inaonekana hili gari lina matatizo makubwa ya ushuru,” alisema ofisa huyo.

FIGISU NYINGINE

Kumbukumbu zinaonesha gari hilohilo la Wema ambalo alisema amejinunulia kwa fedha zake, ndilo alilodaiwa kununuliwa na mbunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye aliwahi pia kutajwa kuwa ndiye baba kijacho wake kabla ya Idris Sultan kuibuka na kujinadi kuwa ndiye ‘mmiliki’ halali wa tumbo hilo.

KIGOGO SERIKALINI AMUOKOA

Paparazi wetu alimtafuta mtu wa karibu kabisa na Wema ambaye alieleza kuwa, Madam baada ya kuhaha kwa muda mrefu eneo hilo huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenye bunduki, alipata wazo la kumpigia kigogo mmoja serikalini (jina tunalo) ambaye alimpa msaada kwa masharti.

“Alimpigia simu… (anataja jina la kigogo), akamweleza matatizo yaliyomkuta, naye akazungumza na maofisa wa TRA, wakakubaliana kwa masharti kwamba asilitumie gari hilo ndani ya wiki moja mpaka apeleke vibali vya gari hilo,” alisema mtu huyo wa karibu na Wema.

HUENDA LIKATAIFISHWA KAMA LA WOLPER

Kwa mujibu wa taratibu na sheria za TRA, endapo Wema atashindwa kutoa nyaraka muhimu za gari hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa gari hilo kama ilivyomtokea mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye mwaka 2014, gari lake aina ya BMW X6 lilikamatwa na kutaifishwa kwa kushindwa kulipia ushuru na kukosa vibali halali.

WEMA ASAKWA

Baada ya kupewa taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Wema kwenye simu yake ya mkononi lakini muda wote iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

MENEJA WA WEMA ANENA

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, meneja wa msanii huyo, Martin Kadinda alisema yeye alisikia kwa watu kuhusu taarifa za Madam kukamatwa na gari hilo lakini alipomuuliza alimwambia si kweli, ni uzushi tu na hata gari hilo lipo nyumbani aende kuliona jambo ambalo alilifanya na kweli akajionea gari hilo.

“Ni uzushi tu. Nimeongea na Madam, akanihakikishia kwamba hamna kitu kama hicho. Nikaenda kulitazama gari, nikalikuta nyumbani kwake Ununio, shwari kabisa,” alisema Martin.

Gazeti ndugu na hili, Amani, toleo la Alhamisi iliyopita, ukurasa wa nyuma kulikuwa na habari yenye kichwa; Range la Wema layeyuka. Msingi wa habari hiyo ni taarifa kuwa, Wema haonekani akiwa na gari hilo licha ya kujinadi kuwa ni lake. Amekuwa akitumia kigari kidogo ‘ki-kirikuu’ kuendea kwenye shughuli zake.

Ilidaiwa kuwa, Wema alilipeleka gereji au yadi ya kuuzia magari, gari hilo hali iliyowafanya mapaparazi wa OFM kulisaka bila mafanikio huku ikielezwa kuwa, gari hilo si lake bali huwa anapepewa kwa muda kujiachia nalo.

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMETEUA MAKATIBU TAWALA WAPYA 2

HATIMAYE TIMU YA GENK YA UBELIGIJI IMEMALIZANA RASMI NA SAMATTA


Mbwana Samatta akipasha viungo vyake.
Katika dakika ya mwisho KRC Genk hatimaye imemnasa mshambuliaji iliyotumia muda na maarifa kuinasa saini yake kutoka katika klabu yake ya TP Mazembe. Samatta aliwasili jana Brussels na alisafiri moja kwa moja kuelekea Genk .

Aly Mbwana Samatta (° aliyezaliwa Dar es Salam 23 Desemba 1992 , 1.80 m na 75 kg) ni mchezaji anayeweza kutumia miguu yake yote kwa ufasaha na mshambuliaji ambaye pia anaweza kucheza kama winga wa kulia. Ametoka Kongo katika klabu ya TP Mazembe.
Samatta (kushoto), akiwania mpira.


Akiwa pamoja na klabu hii alishinda taji la klabu bingwa Afrika 2015, alikuwa mshindi mara nne mfululizo wa ubingwa wa Kongo na mshindi wa Supercup mara mbili. Samatta amefanikiwa kuchaguliwa mara ishirini kwa timu ya taifa ya nchi yake nyumbani Tanzania . Katika michezo hiyo, alifunga mabao saba.

Katika msimu wa 2015 alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwa wale wanaocheza ligi za ndani za bara la Afrika . Amekubali kusaini mkataba hadi mwisho wa msimu 2019-2020.


Q-CHILLAH KUONGOZA VICHWA ZAIDI YA 10 JUMAPILI HII KWENYE UTAMBULISHO WA BENDI YAKE


Jumapili hii katika Ukumbi wa Billicanaz wasanii, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah, Mb Dog, Khadja Nito, Amo Genius, Shalvin, Med na Udsm Xband watakinukisha ile mbaya katika utambulisho wa bendi yao mpya ya Qs International Music.

Wasananii wengine watakaosindikiza utambulisho huo ni Chaz Baba, Juma Nature, Bushoke, Abdul Misambano na Banana Zorro.

KHAAAA....KUMBE WEMA,NAJMA WANASHEA TENA PENZI KWA IDRIS!

Wema Sepetu na baba kijacho wake, Idris Sultan.


Ubuyu mpya kabisa uliotua kwenye meza ya dawati hili unadai kuwa, Mshindi wa Shindano la Big Brother 2014 ambaye anatajwa kuwa ndiye ubavu wa Wema Sepetu kwa sasa, Idris Sultan, anatoka pia na msanii anayefahamika kwa jina la Najma Dattan ‘Naj’.

Najma ni msanii wa muziki aliyewahi kuwa na uhusiano na Mr Blue kabla ya kuhamia kwa Diamond miaka kadhaa iliyopita.

Najma Dattan.

Kisikie chanzo
Chanzo chetu kilicho karibu na Najma kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, Idris na Najma wamekuwa wakitoka kwa muda mrefu na kwa ndugu wa binti huyo wala siyo siri.

“Unajua watu hawajui kuwa Idris yuko na Najma na mara kwa mara amekuwa akienda nyumbani kwao na hata ndugu wa Najma wanamjua.
“Kilichoibua taharuki ni juzikati Idris kudai ile mimba ya Wema ni yake, unaambiwa Najma anashangazwa na taarifa hizo,” kilidai chanzo hicho.

Wanaswa pamoja
Wakati madai hayo yakitua kwenye meza ya gazeti hili, mmoja wa mapaparazi wa Ijumaa hivi karibuni aliripoti tukio la Idris na Najma kunaswa pamoja kwenye hafla ya Clouds TV iliyofanyika pale Escape One, Mikocheni jijini Dar ambapo alisema:

“Mimi niliwaona pale Escape One, Idris alifika na kumchukua Najma na kumuingiza kwenye gari lake na kuondoka, alishuhudia Martin Kadinda, Steve Nyerere na mastaa wengine,” alisema paparazi huyo na kudai alikuwa akifuatilia ili kujua uhusiano wao.

Najma asakwa
Baada ya madai hayo kutua kwenye dawati la Ijumaa, jitihada za kumtafuta Najma kwa njia ya simu zilifanyika na alipopatikana alikiri kujuana vilivyo na Idris ila akagoma kuzungumzia uhusiano wao.

Ijumaa: Najma habari yako, unafahamiana na Idris? Je, ni mpenzi wako kwani kuna madai kuwa wewe unatoka na yeye kimapenzi na kwamba jamaa kakuzimia ile mbaya licha ya yeye kudai kampa mimba Wema, unalizungumziaje hilo?

Najma: Mh! Yaani nyie mmekosa la kuandika na udaku wenu, naomba nisiongelee lolote juu ya hilo.

Ijumaa: Tunachotaka kujua ni kama wewe na Idris ni wapenzi kweli, hilo tu.Najma: Niacheni jamani.

(Akakata simu)
Alipopigiwa tena hakupokea. Kwa upande wa Idris simu yake iliita weee, haikupokelewa, alipotumiwa sms pia hakujibu.

Ijumaa linaendelea kuwawekea mitego kwani kuna msemo wa Kiswahili usemao, mapenzi ni kikohozi, hawawezi kuficha uhusiano wao milele.

Thursday, January 28, 2016

MBWANA SAMATTA AWASILI UBELIGIJI TAYARI KWA KUITUMIKIA TIMU YAKE MPYA YA GENK

 Mbwana Samatta
STAA wa soka la Bongo Mbwana Samatta ‘Popa’ ameondoka usiku wa January 27 kuelekea Ubeligiji kujiunga rasmi na klabu ya Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubeligiji maarufu kama Belgian Pro League.
Akiwa tayari amesaini mkataba na klabu hiyo, Samatta alikuwa anasubiri ‘taa ya kijani’ kutoka kwa bosi wa TP Mazembe Moise Katumbi ambaye mwanzoni alikuwa anaweka ‘kauzibe’ kutoa ruhusa kwa mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika kwenda kujiunga na klabu ya Genk.
Samatta anatarajia kuanza maisha mapya kwenye klabu ya Genk baada ya kuipa mafanikio makubwa klabu ya Mazembe tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2011 akitokea Simba SC.
Atakumbukwa na wana-Lubumbashi kwa kuisaidia timu yao kutwaa taji la ubingwa wa Afrika mwaka 2015 pamoja na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kuifungia timu yao mabao saba kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.
Samatta 

Samatta ameshawasili nchini Ubeligiji tayari kwa ajili ya kuanza majukumu mapya kwenye klabu hiyo ya barani Ulaya.
Klabu ya Genk imeshawahi kuwatoa mastar wakubwa barani Ulaya wanaotamba kwenye vilabu vikubwa vya ligi maarufu duniani. Christian Benteke (Liverpool), Kelvin De Bruyne (Manchester City), Thibaut Courtois (Chelsea) ni baadhi ya majina ya mastar ambao wamewahi kupita kwenye klabu ya Genk.

Wednesday, January 27, 2016

BELLE 9: KOLABO YANGU NA CHRIS BROWN,AUGUST ALSINA INAWEZEKANA!

Staa wa Ngoma ya Shauri Zao, Abednego Damian ‘ Belle 9’
STAA anayetamba kwa sasa na wimbo wa  Shauri Zao, Abednego Damian ‘ Belle 9’ amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa na shauku ya kutaka kufanya kolabo na mastaa wa muziki wa Marekani, August Alsina pamoja na Chris Brown na kwamba jambo hilo linawezekana kufanyika soon.

Akichonga na mwandishi wetu, Belle9 anayebamba pia na Ngoma ya Burger Movie Selfie, alisema kuwa mastaa hao ni kati ya wasanii ambao amekuwa akiwakubali sana.

“Muziki wetu kwa sasa unakubalika kimataifa na wasanii wameamka sana. Ndoto zangu kubwa si kukimbilia Nigeria wala Sauz kufanya kolabo ila ni kukamilisha ndoto ya kufanya ngoma na Chris pamoja na Alsina,” alisema Belle 9.
 Belle 9


MGOGORO WA MATANGAZO YA BUNGE KURUSHWA HEWANI LAIVU MENGI YAIBUKA!



Baadhi ya picha zikionyesha matukio ya Askali Polisi baada ya kuingia ndani ya Ukumbi wa Buunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari kwa kutuliza fujo zilizotokana na mabishano makali baina ya chama tawala na uapande wa upinzani, mara baada  ya mswaada wa kusitishwa urushaji wa matangazo ya Bunge laivu kuwasilishwa na Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo Nape Nnauye.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo Nape Nnauye akitoa mswaada unaohusiana na kusitishwa kurushwa laivu  baadhi ya matangazo ya runinga Bungeni mjini Dodoma 



Waziri Mkuu, Kassim Majalliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama Buneni mjini Dodoma.


Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akimwapisha Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Joyce Ndarichako, bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo Nape Nnauye akitoa kauli Bungeni mjini Dodoma .Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Bungeni mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bunge, Mtemi Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge mjini Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma.
 Kutoka kushoto ni Ruth Mollel wa Viti Maalu Chadema, Hawa Mwinga wa Viti Maalum Cahdema na Ali Saleh wa Malindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Baadhi ya wabunge wametolewa nje kwa kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ya Zitto Kabwe juu ya tamko la serikali la kusimamisha kurushwa matangazo ya moja kwa moja ya bunge kwenye TV taifa.

Serikali Yatoa Ufafanuzi Juu Ya Kutorusha Matangazo Ya Bunge


PROFESA JAY AGOMEA KUITWA MHESHIMIWA, AWATAKA WANANCHI WA MIKUMI WAMUITE MTUMISHI!

Mbunge wa jimbo la  Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay’. katika pozi.
Mbunge mpya wa Mikumi (Chadema) ambaye ni msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amewaambia wapiga kura wake kumuita Mtumishi badala ya Mheshimiwa, kwa sababu kazi yake ni kuwatumikia wananchi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Dodoma, Profesa Jay alisema alipoomba kura aliahidi kuwatumikia wapiga kura wake ili kufikia ndoto zao za maisha bora kwa kuondoa kero mbalimbali, hivyo hawezi kuifanya kazi hiyo kama atakubali uheshimiwa badala ya utumishi.
Mbunge mpya wa Mikumi (Chadema) Profesa Jay.
“Tuliahidi utumishi uliotukuka kwa wapiga kura, tumekuja hapa kuifanya kazi hiyo kwa kuisimamia serikali ili iondoe kero zote zinazowakabili wananchi, sasa ukiruhusu uheshimiwa, unaweza kujikuta unasahau wajibu wako, lakini kama kila mara utajikumbusha kuwa wewe ni mtumishi wao, hakika hautakuwa na muda wa kupoteza,” alisema mbunge huyo na msanii wa pili wa Hip Hop kuingia bungeni baada ya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ wa Mbeya mjini (2010).

MAKUBWA!..ETI MIMBA YA KAJALA NI YA DIAMOND


Muigizaji wa Filamu Bongo Kajala Masanja akiwa katika pozi.

 Hee! Huu ni ubuyu mpyaaa! Mwigizaji Kajala Masanja amekiri kuwa ni mjamzito huku taarifa zikidai kuwa huenda mhusika wa kiumbe alichonacho ni staa nambari moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Risasi Mchanganyiko limeichimba habari kamili.

ISHU ILIVYOIBULIWA
Hivi karibuni, gazeti ndugu na hili la Risasi Jumamosi ndilo lilikuwa gazeti la kwanza kuripoti habari za madai kuwa Kajala ana ujauzito wa kigogo mmoja serikalini (jina tunalihifadhi) lakini mashosti wa karibu wa Kajala wameibuka na kudai kuna asilimia nyingi mimba aliyonayo ni ya Diamond na si kigogo huyo.

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

TUJIUNGE NA SHOSTI WA KAJALA
Akizungumza kwa sharti la kuomba hifadhi ya jina, rafiki mmoja wa Kajala alisema ana imani mimba hiyo itakuwa ni ya Diamond kwani kuna kipindi shosti yake huyo aliwahi kuanguka dhambini na staa huyo wa Bongo Fleva.“K (Kajala) kweli alikuwa na yule kigogo (anamtaja jina) lakini sasa waligombana.

DIAMOND ALIPITA?
“Wakiwa wamegombana, Diamond naye alipita si unajua tena zile za kumalizana leo leo tu, sasa nikijaribu kufanya mahesabu tangu Kajala aniambie ana mimba na tangu wagombane na kigogo, naona kabisa Diamond ndiye mwenye asilimia nyingi kuwa baba kijacho,” alisema rafiki huyo.

DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond ili aweze kuzungumzia kuhusishwa kwake na mimba hiyo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

TIMU WEMA WASHANGAA
Baadhi ya mashabiki wa Wema ambao walipenyezewa habari ya Diamond kutajwa kuwa mhusika, walimshangaa mwigizaji huyo kwani anazidi kujijengea sifa mbaya.
“Mh! Inashangaza kwa kweli kama ni kweli. Kajala huyohuyo si ndiyo alimuibia Wema yule CK sasa tena ambebee mimba Diamond ambaye alikuwa mpenzi wa Wema!” alisema mmoja wa mashabiki wa Wema.

KAJALA SASA
Gazeti hili lilifunga safari hadi kwa muigizaji huyo na kutaka kujua ukweli wake. Awali, mwanahabari wetu alitaka kujua kama ni kweli Kajala ni mjamzito, akafunguka:
“Ni kweli mimi ni mjamzito na tena ujauzito huu unanisumbua sana, si unajua tena mimi ni mwanamke na ninamshukuru Mungu kwa kunijaalia zawadi hiyo.”

NI MZIGO WA NANI?
Kuhusu mhusika hasa wa ujauzito huo, Kajala hakutaka kuweka wazi, badala yake alisema kila kitu kitakuwa wazi baada ya kiumbe kuzaliwa, wakati wowote mwaka huu.
“Subiri mtoto azaliwe mbona una presha sana? Kila kitu kitakuwa wazi mwaka huuhuu tu, kuwa mpole.”

Kwa nyakati tofauti, Kajala ametajwa kuhusishwa na wanaume kadhaa, akiwemo kigogo huyo wa serikali ambaye hata hivyo, alipoulizwa kama ndiye mhusika halali, alishindwa kukubali au kukataa, ingawa ‘data’ zinaonyesha kuwa wakati akinasa ujauzito huo, alikuwa katika mzozo mkubwa na kigogo huyo.

“Hamna kitu kama hicho, huyo mtu anatapatapa tu, mimi nilifanya naye (Kajala) tu shughuli za kikazi zilipoisha, kila mtu anaendelea na maisha yake, halafu hawa wasanii ni watu wa kuwa nao makini, wana mambo ya kuzusha na kuzushiana mambo ya ajabu kiasi ambacho wanaweza kukosa mambo mengi ya kikazi,” alisema kigogo huyo.

SAMATTA AZAWADIWA HEKA TANO ZA VIWANJA

Baadhi ya wapenzi wa soka wakimkabidhi maua mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza barani Afrika, Mbwana Samatta mara alipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa kuamkia jana. (Picha na Bin Zubeiry).
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeamua kumpa uanachama wa heshima mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta pamoja na kumzawadia ekari tano za ardhi katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga kwa ajili ya kuanzisha Chuo cha Mafunzo ya soka.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa kikao cha Kamati ya Utendaji ya Mtandao huo kilichoketi juzi kilifikia uamuzi huo baada ya kufuatilia kwa karibu mafanikio ya Samatta akiwa na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kongo na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika hadi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora Afrika.
Alisema SHIWATA inatoa kiwanja hicho kama zawadi kwa mchezaji huyo kutokana na uwezo wake wa kulitangaza taifa katika medani ya kimataifa katika mchezo wa soka ambako wengine watafuata nyayo zake.
Taalib alisema taratibu za makabidhiano zinafanywa kwa mawasiliano na baba yake mzazi, Ali Samatta na atakabidhiwa eneo hilo mara baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ambako anakwenda kusaini mkataba na timu ya KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji wa miaka minne.
SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 inamiliki ekari 300 za kujenga makazi, kumbi za starehe, viwanja vya michezo na nyumba za kuishi katika kijiji cha Mwanzega wilayani Mkuranga na ekari 500 eneo la Ngarambe kwa ajili ya kilimo.
Wakati huo huo wasanii wanne maarufu nchini wakiongozwa na Ahmed Olotu ‘Chilo’ juzi walinogesha tamasha la sanaa na michezo wilayani Mkuranga walipoalikwa kuona sanaa inavyochezwa na wasanii wa wilaya hiyo.
Mzee Chilo aliyefuatana na Boniface Mwanza Mpango ‘King Kikii’, Wasanii wa Bongo Movie, Suzan Lewis ‘Natasha, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Asha Salvador walijikuta wakishangiliwa mara kwa mara na wasanii wenyeji ambao pia walipiga nao picha.

SOMA KALI HII ETI MASHEKHE 5 WASHUKA KUMUOMBEA NORA!


Muigizaji mkongwe wa filamu nchini, Nuru Nassoro ‘Nora’.
 Baada ya hali ya muigizaji mkongwe wa filamu nchini, Nuru Nassoro ‘Nora’ kubadilika kwa kile kinachodaiwa kuwa ugonjwa unaompanda kichwani, mashehe watano wameletwa kutoka kisiwani Zanzibar ili kuja kufanya maombi maalum ya kumnusuru na hali yake.

Chanzo cha uhakika kilicho karibu na familia ya Nora, kimesema kuwa mashehe hao wanaongozwa na shehe maarufu ndani ya nje ya nchi, Salum Maridhia, ambao tayari wameshawasili jijini Dar es Salaam.

“Unajua Shekhe huyo anafanya sana kazi zake nje ya nchi, lakini kuna ndugu yake alimsaka na kumpata kwa ajili ya kwenda kuondoa maradhi ya Nora, kwa kuwa Shekhe huyo anasifika sana,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Gazeti hili liliwasiliana na shehe huyo ili kujua ukweli wa taarifa hizo, ambapo alikiri na kusema anao uwezo wa kuondoa tatizo la muigizaji huyo na hata wengine wa aina hiyo.

“Mimi nilipoambiwa habari hiyo nilikatiza ziara zangu zingine, nimeamua kuja kumuona na baada ya siku saba atakuwa sawa na nitawasaidia na wengine pia” alisema Shehe Maridhawa.

PLUIJM: NINA DOZI SAHIHI YA MAZOEZI YA NIYONZIMA KUMUWEKA FITI ZAIDI


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Hans van Der Pluijm akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bocco Veteran, (wa pili kulia ni kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzima akisikiliza maelezo ya kocha huku akijikagua tumbo lake).
LICHA ya wanachama wa Yanga kufurahia kurejea kwa fundi wa pasi kikosini hapo, Haruna Niyonzima baada ya kumaliza matatizo yake na klabu hiyo, kocha mkuu wa timu hiyo Hans van Der Pluijm amesema bado siyo yule Niyonzima anayemjua.

Kiungo huyo amerejea kikosini wiki iliyopita baada ya kukaa nje tangu Novemba mwaka jana, alipokwenda kwao Rwanda katika majukumu ya timu ya taifa.

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima wa nne kutoka kushoto akiongoza mazoezi ya kukimbia katika uwanja wa Bocco Veteran .
Hata hivyo, Pluijm alisema kiungo huyo bado hajawa fiti kwa ajili ya kumtumia, badala yake anatakiwa kuongeza bidii mazoezini ili kurejesha kiwango chake kwani alikuwa nje muda mrefu.

 “Haruna bado hajawa fiti, anatakiwa kujituma zaidi ili kuwa fiti, hata mchezo uliopita (dhidi ya Friends), alikuwa asicheze, lakini  nililazimika kumtumia tu kwa kuwa Makapu (Said) alifiwa na kaka yake na mazishi yalikuwa siku hiyo.


 “Vinginevyo Haruna alitakiwa angalau acheze dakika 20 kwa kuwa hakufanya mazoezi na sisi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana.

Tuesday, January 26, 2016

BUNGE LAANZA KURINDIMA DODOMA LEO!

Spika mpya wa Bunge la 11, Job Ndugai.
MKUTANO wa Pili wa Bunge la 11 unaanza leo mjini Dodoma ambapo Bunge litajadili hotuba ya Rais kwa muda wa siku tatu.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya alisema hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari mjini hapa.

Alibainisha kuwa Bunge litamaliza vikao vyake Februari 5, mwaka huu.

Alisema kutakuwa na kujadili hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge jipya la 11 Novemba 20, 2015.

“Mjadala kuhusu hotuba ya Rais unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Januari 26 hadi Januari 28, 2016” alisema.

Alisema kwa kuwa Bunge la 11 mpaka sasa lina idadi ya Wabunge 380, ni wazi kuwa kwa siku tatu zilizotengwa, wabunge wote hawatapata nafasi ya kuchangia.

Pia, alisema katika kikao cha kwanza leo, itawasilishwa hoja ya kutengua Kanuni za Bunge ili badala kila Mbunge kuchangia kwa dakika 15 sasa iwe dakika 10 tu.

Aidha, Kipindi cha Jioni badala ya kuanza saa 11 jioni, kianze saa 10 jioni na hilo litaongeza idadi ya wachangiaji kutoka 63 ambao wangepatikana kwa utaratibu wa kawaida hadi 114 baada ya Kanuni husika kutenguliwa.

Vilevile, utaratibu utaandaliwa ili Spika aweze kuchagua wabunge watakaochangia kwa kuzingatia uwiano wa vyama na vigezo vingine. Pamoja na hayo, Bunge litajadili na kuridhia Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Alisema Bunge litajadili na kuidhinisha Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 5, unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mpango huo ni wa Mwaka 2016/17 – 2020/21 na itakumbukwa kuwa kila mara tunapoanza Bunge jipya Serikali huwasilisha Mpango huo bungeni ili uweze kujadiliwa na Bunge”.

Mkutano uliopita wa Novemba 2015 ulikuwa ndio wa kwanza wa Bunge jipya na mahsusi kwa ajili ya ufunguzi wa Bunge tu, hivyo kulazimika kuhamishia katika mkutano huu wa Pili, ambao kimsingi hushughulikia Taarifa za Mwaka za Kamati za Bunge.

Shughuli nyingine itakuwa ni kiapo cha uaminifu kwa wabunge 11, ambao wamechaguliwa na wengine kuteuliwa na Rais baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge.

Wabunge hao ni pamoja na Goodluck Mlinga wa Jimbo la Ulanga, Shaaban Shekilindi wa Lushoto, Godbless Lema wa Arusha Mjini, Omar Kigoda Jimbo la Handeni, Deogratias Ngalawa wa Ludewa na Rashid Chauchau wa Masasi.

Katika Mkutano huu, jumla ya maswali ya msingi ya kawaida 125 yanategemewa kuulizwa na kujibiwa. Alisema utaratibu wa kumuuliza Waziri Mkuu maswali ya hapo kwa papo kila Alhamisi utaendelea.

Monday, January 25, 2016

SOMA HAPA HABARI YA KUSIKITISHA MAMA KUWAUA WANAE WAWILI


 Eliza Bugusi Steven (28),Mwanamke anayedaiwa kuwaua wanaye

MARA: Mwanamke mmoja Eliza Bugusi Steven (28), mkazi wa Kijiji cha Kamugegi, Kata ya Kamugegi, Wilaya ya Butiama mkoani Mara, ameelezewa jinsi alivyowaua kwa kuwanywesha sumu watoto wake wawili wa kuwazaa.
Nicholaus Steven (miaka 4)
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa Eliza alifanya tukio hilo Januari 7, mwaka huu, saa nne usiku akiwa nyumbani kwao, kwa kile kilichodaiwa kunyanyapaliwa na ndugu zake baada ya mwanamke huyo kurejea kuishi kijijini akitokea jijini Mwanza alikokuwa akiishi na mumewe.
Francis Steven (miaka 2)
Marehemu hao, Nicholaus Steven (4) na Francis Steven (2) walinyweshwa sumu hiyo iliyokuwa kwenye kikombe na baada ya kuhakikisha wamepoteza uhai, mwanamke huyo naye alikunywa iliyobaki, lakini akaokolewa muda mfupi baadaye baada ya kupiga mayowe ya kuomba msaada.
Waombolezaji siku ya msiba
Inadaiwa kuwa, Eliza ambaye mumewe alifariki dunia mwaka jana, tangu alipofika kijijini hapo amekuwa akinyanyapaliwa na mama yake mzazi pamoja na mdogo wake, ambao wamekuwa wakimtuhumu kuugua ugonjwa unaotokana na ngono.

Diwani wa Kata ya Kamugegi, Ikungura Charles, amesema: “Mdogo wa Eliza ambaye aligombana naye muda mfupi kabla ya tukio hilo, ametoweka nyumbani hapo.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.



“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji na jaribio la kujiua baada ya hali yake kutengemaa,” alisema kamanda huyo.

IDRIS AJITOA FAHAMU KWA WEMA, ATANGAZA KIMAFUMBO KUWA MKEWE!

Wema na Idris katika pozi.
Idris & Wema

Kumekuwa na uvumi mkubwa kuwa Idris Sultan na Wema Sepetu wana uhusiano wa kimapenzi na pengine very soon wawili hao watamkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza! Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaompenda Idris ama Wema Sepetu na utapenda kufahamu aliyoyasema mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan kuhusu Wema Sepetu na vichwa vya habari za ujauzito, yapo mapya.
Wema Sepetu na Idris Sultan.
Kupitia page yake ya Instagram @Idris Sutlan kafunguka na kusema haya kuhusuWema…

 “ Mimi na wewe sio kama watu wengine. Nalala, nakula na naamka nikiwa nakufikiria wewe. Unafikiri una bahati ya kuwa na mimi ila hapana hapana mimi ndio mwenye bahati ya kuwa na wewe. Mara ya kwanza ilikuwa ajabu kwangu kuangalia ndani ya kabati langu la nguo na kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia “Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike“ au ukiingia jikoni kwangu na kuitawala nyumba yangu na vyakula vizuri. Jinsi unavyowatazama wanawake wengine wakinisogelea, jinsi vile unavyojua ni wakati gani nahitaji kupewa a kiss au kumbatio zito. Jinsi unavyonilazimisha kuangalia channel ya Disney, jinsi unavyoniamsha mapema siku hizi kunitengenezea chai. Naweza nikakuletea ua zuri la waridi lakini halitaweza kufikia uzuri wako. Ukiwa na wivu unasonya sonya, nikiwa na wivu natabasamu. Naweza kufanya lolote hata kuhamisha milimia kwa ajli yako. Nitakulinda, nitakupenda, nitakudekeza, nitakupikia, nitagombana na wewe, tutaangalia movies pamoja, nitakaa na wewe kuangalia nyota. Wewe ni zaidi ya kile nilichokiomba, wewe ni kila kitu changu “My Wife

Sunday, January 24, 2016

MANJI:TIBOROHA ALIFICHA BARUA ZA NIYONZIMA!

Mwenyekitiki wa Klabu ya Yanga Yussuf Manji akionge mbele ya wanachama wa klabu hiyo na Waandishi wa habari hawapo pichani.
JANA mwenyekiti wa Klabu ya Yanga SC, Yussuf  Manji alikutana na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu ya Yanga kwa ajili ya kutoa ufafanuzi juu ya sakata la kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo pamoja na kutoa taarifa ya maandishi ya sababu za kung’oka kwa Dr. Jonas Tiboroha.

Yapo mengi lakini hizi ndiyo baadhi ya sababu ambazo zimetolewa na uongozi wa Yanga kwa maandishi zikianinisha sababu za Dr. Tiboroha kuondoka kwenye klabu ya Yanga.

Ktibu ametajwa kama ndiye ambaye alisababisha au alitoa sababu za uongo kuhusu suala la Haruna Niyonzima. Taarifa alizokuwa akizipata zilikuwa hazifiki kwenye kamati ya utendaji, kamati ya nidhamu ambayo ilikaa haikupata ushirikiano mwisho wa siku kamati ikaamua kuchukua uamuzi ambao baadaye wakaja kuuona kwamba haukuwa sahihi kwasababu katibu alikuwa amekalia baadhi ya taarifa muhimu.

Sababu nyingine iliyotolewa ni kwamba, katibu hakuweza kufikia malengo ambayo aliwekewa. Wakati anaikuta Yanga ilikuwa inatumia bajeti ya Tsh. 500 kwa mwaka lakini sasahivi Yanga inatumia karibu bilioni 2 kwa mwaka. Katibu kashindwa kuongeza mapato ya klabu ya Yanga kwahiyo ameshindwa kuitumia nafasi yake vizuri.

BDF ya Botswana ilianzima US$ 5,000/- ambazo hadi sasa hazijarejeshwa: EXCOM iligundua taarifa kuhusiana na deni hili, imekuwa ikifichwa na hakuna maelezo mrejesho kuhusiana na hilo kutoka kwa Tiboroha ambaye amekuwa na ukaribu na wahusika kutoka Botswana.

Manji akasisitiza kuwa Tiboroha alikuwa ni mwajiriwa, kwahiyo mwajiri wake anao uwezo wa kusitisha kibarua chake wakati mwingine hata watu wasijue kwanini.

Sababu nyingine iliyotajwa ni kwamba Katibu alikuwa najiendeleza binafsi kuliko taasisi. Alionekana kutaka kujiendeleza binafsi kusikika peke yake na kujulikana mwenyewe kama Mungu mtu jambo ambalo lilichochea kelele ndani ya klabu kama vile yeye ni malaika.

Hakufuata ushauri aliopewa na wataalamu wa TRA, hali iliyosababisha akaunti za Yanga kufungwa, hivyo mimi kulazimika kuanza kutoa fedha zangu za mfukoni katika uendeshaji wa Klabu kwa kipindi chote na wakati huo wachezaji walikuwa wakidai mishahara na tuko katikati ya msimu.

Katibu kushirikiana na TFF katika masuala mengi ambayo Yanga kama klabu ilikuwa inapinga, Katibu alikuwa anaonekana kui-support TFF. Alisahau kama yeye ni mwajiliwa wa klabu ya Yanga. Lile la kushindwa kumpigania msemaji Msemaji wa Klabu, Jerry Murro asifungiwe na TFF, huku akimchimba huku akijua alikuwa akipitia taarifa zote kabla ya Jerry kuzitoa. Alikuwa na roho mbaya kwa kuwa Jerry alipata umaarufu zaidi kwa wanachama kutokana na kuipigania klabu.

Kuna madai kwamba klabu ya Yanga ilipata mwaliko kutoka FIFA kwenda semina Ghana lakini Katibu akajipitisha mwenyewe kwamba ataenda kuhudhuria yeye bila kamati ya kukaa na kuamua nani ataiwakilisha.

Ngoma alipewa taarifa na Tiboroha kwamba anatakiwa kwenda kufanya majaribio na klabu moja nchini Uturuki. Tiboroha alifanya hivyo akijua Ngoma alikuwa anakwenda kushiriki michuano ya MAPINDUZI Cup, mbaya zaidi hakuwa amewasiliana na EXCOM kuhusiana na hilo kabla kumfahamisha mchezaji na kumpa taarifa hiyo.

Baadaye kocha Kocha Mkuu, alilalamika kwamba kufanya vile ilikuwa ni kuondoa morali ya mchezaji katika michuano hiyo ya MAPINDUZI CUP na baada ya hapo, angekuwa akiwaza kuhusiana na Uturuki tu. Mwisho, kocha alisema, Ngoma alicheza chini ya kiwango katika michuano hiyo, akiamini Yanga inamzuia kusonga mbele kimaisha.

Taarifa hiyo pia inaonesha kwamba, Katibu alimwajiri daktari ambaye alihudumu mechi dhidi ya Mgambo lakini baadaye ikagundulika kwamba daktari huyo alikuwa ni mwanachama anayemiliki kadi ya Simba.

Ukiangalia hayo juu, ni kati ya machache ambayo nimeona ninaweza kuyaanika kwenye vyombo vya habari, lakini yako mengi ambayo ni nyeti na haitakuwa sahihi kuyaanika kwenye vyombo vya habari kwa maslahi ya klabu. Yanga ilianza kung’amua mambo yanayomhusu Tiboroha muda sasa, alipoona mengi yamegundulika. Januari 14, 2016 aliandika barua kuomba radhi kwangu, akikiri kufanya makosa na kusema alikuwa akiyajutia.

Sisi, hatukukubaliana na kutoa msamaha kutokana na hofu ya unafiki wake, na nilitoa ushauri; kwamba vizuri akachukua hatua ya kujiuzulu mara moja na huenda ingekuwa vizuri aeleze ana matatizo ya kifamilia pia kiafya, lengo lilikuwa ni kumpa nafasi ya kuachana na Yanga kwa amani pia kuilinda familia maisha yake huko mbeleni. Lakini nilimtaka ahakikishe zile fedha tunazowadai BDF kutoka Botswana, mara moja zinawasilishwa Klabuni na baada ya hapo, rasmi atakuwa amejiondoa.

Tiboroha alikubaliana na hilo na kuandika barua ya kujiuzulu alioiwasilisha Januari 22, 2016.

Pamoja na kumshauri ili ajiuzulu kwa heshima, lakini alionekana kuanza kutengeneza “Presha ya wanachama” kama vile mtu aliyeonewa. Kuna mkutano wa ujanjaujanja uliitishwa makao makuu ya Klabu, Tiboroha akiwa mshiriki mkuu nyuma ya pazia, hii ilikuwa ni Januari 23, 2016. Lengo ni kutengeneza hali ya hofu kwa Wanachama, jambo ambalo si sahihi.

Kwa yote hayo hapo juu: Kamati ya Utendaji (EXCOM) inapenda kutoa taarifa kuwa imevunja mkataba wa Tiboroha kama Katibu Mkuu wa Yanga.

Inaonekana kulikuwa na fukuto la muda mrefu kati ya Katibu na uongozi wa juu wa klabu hiyo na kulikuwa na sababu nyingi za kumng’oa katika kiti hicho lakini sakata la Haruna Niyonzima limekuwa kama chambo au chanzo cha Katibu huyo kutimka kunako mtaa wa Jangwani.

CHELSEA YAIBAMIZA ARSENAL

Mshambuliaji wa timu ya Chalsea Diego Costa (katikati), akijaribu kuipenya ngome ya Arsenal mapema kwenye mchezo uliyomalidhika kwa timu hiyo kuwalaza Arsenal kwa bao 1-0.
Ozil akijaribu kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo ambalo limedumu hadi mwisho wa mchezo huo.

YANGA YAICHAPA 3-0 FRIENDS RANGERS TAIFA

Washambuliaji wa timu ya Yanga SC, Paul Nonga na Simon Msuva wakiwa wamekumbatiana wakati wakishangilia bao lililofungwa na Msuva.
 TIMU ya Yanga SC, mapema leo imefanikiwa kutinga raundi ya 16 bora kwenye michuano ya ya Azam Sports Federation Cup maarufu kama FA baada ya kuichapa magoli 3-0 timu ya Friends Rangers ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga Paul Nonga akiwatoka mabeki wa timu ya Friends Rangers.
Msuva kushoto akionyesha uwezo wake uwanjani hapo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...