Friday, November 30, 2012

AIRTEL TANZANIA YAANDA PART YA KUMPONGEZA BALOZI WAKE AMBWENE YESSAYA "AY" NYUMBANI LOUNGE LEO



Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya Channel O aliyoipata Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa ushindi alioupa pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam


Afisa Uhusiano wa Airtel akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya video bora, Katikati ni AY akifatiwa na DJ wake Athur Baraka
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya “ AY “ na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “ I don’t wanna be alone”
Akiongea na wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fursa hiyo kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
Naye Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii mbalimbali toka Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa kusherehekea ushindi huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu. Tunapenda pia kuchukua fursa hii kuwaalika watanzania na wateja wetu leo pale nyumbani lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa Mziki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY'



Thursday, November 29, 2012

HAWA NDIO WAREMBO WATAKAOWANIA TAJI LA MISS EAST AFRICA 2012 NDANI YA MLIMANI CITY TAREHE 7 DECEMBER




Burundi

Warembo watakaowania taji la Miss East Africa 2012 wakiwa katika vazi la ufukweni, jijini Dar es salaam. Shindano hilo litafanyika tarehe 7 December 2012 (Ijumaa wiki ijayo), kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam.

Mashindano haya Yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd na kudhaminiwa na TANAPA, Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Ethiopian Airlines, Seascape Hotel, Darlings Hair, Ako Catering, DTP, Satguru, na Clouds FM.
 
Eritrea
 
Ethiopia
 
Kenya
 
Rwanda
 
Tanzania
 
Uganda
 
Somalia

"NIKIACHIKA TENA NITAOLEWA UARABUNI...." JACK WOLPER




PAMOJA na kukataa kumwanika hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa akipigwa chini na jamaa yake huyo, atatimka nchi na kwenda kuolewa uarabuni.

Wolper amesema anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze kuvunjika na ikitokea hivyo, hatataka tena kuwa na mpenzi wa Kibongo.

“Kwa kweli siwezi kuachika tena sasa hivi! Ikitokea sitakuwa na amani moyoni mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda kuolewa nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas’.

MAMA RAY C AKANUSHA UVUMI ULISAMBAA KUWA RAY C AMEFARIKI......



Usiku wa novemba 27 2012 zilisambaa habari za msanii Ray c zikidai kuwa amefariki dunia.....

Habari hizi ziliwagusa wengi ambao walitaka kujua undani na ukweli wa habari hizo.Ukweli ni kwamba, Ray c ni mzima na anaendelea vizuri na matibabu

Mama Ray c ameamua kuvunja ukimya na kuueleza umma kuwa mwanae ni mzima.Wanaosambaza habari hizo ni adui zake tu.....

“inasikitisha sana kusikia taarifa hizo, Ray C ni mzima kabisa namshukuru Mungu anaendelea vizuri na matibabu tuko nae, anakula vizuri anapata usingizi vizuri, hizo habari zimetoka wapi? nazikanusha kabisa kwa jina la Yesu nalikataa hilo neno” MAMA RAY C


Hivi karibuni, hali ya Msanii Ray c ilibadilika na kuwa tete kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya hali iliyomfanya mama yake aombe msaada kwa wasamalia wema ili kugharamia matibabu yake

Wednesday, November 28, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA SAFARI YA MWISHO YA SHARO MILIONEA, VILIO NA MAJONZI VYATAWALA WAOMBOLEZAJI WASHINDWA KUJIZUIA .


Mwili wa marehemu Sharo Millionea ndio umelala humu, nivigumu kuamini
 
Mama mzani wa Marehemu Sharo Millionea Akilia Kwa Uchungu
Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana wa leo,Muheza mkoani Tanga.



Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana wa leo kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele

Nape akizungumza na wananchi waliohudhuria msibani
 

sehemu ya umati wa waombolezaji katika msiba wa Sharo milionea
 
Mwili wa marehemu Sharo Millionea ukiwa umebebwa

Meneja wa Sharo anayejulikana kwa jina la HK akizungumza
Waombolezaji waliopoteza fahamu wakipatiwa huduma ya kwanza msibani hapo.

Miss Kinondoni namba 2, 2011, Husna Maulid akilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya Sharo Milionea leo.

 



 


Tuesday, November 27, 2012

NAPE AWAKILISHA CCM KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MSANII WA BONGO MOVIES, JOHN MAGANGA


 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akitoa salamu za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.
Wasanii wa Bongo Movies wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.

 
Msanii wa Bongo Movies, Husna Maulidi 'Lishez', akitulizwa na wenzake, Babby Candy na Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movies, marehemu John Maganga leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa msanii, John Maganga, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam leo.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Stephen Maganga, baba wa msanii John Maganga wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyama, Dar es salaam leo.
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba (kulia).



HIVI NDIVYO ALIVYOTUTOKA SHARO MILLIONEA .



Marehemu Sharomilionea enzi za uhai wake

Taarifa kuhusu kifo cha Msanii wa maigizo na Mziki wa Bongo fleva kufariki zimasamba nchi nzima masaa machache yaliopita.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari ni kwamba amepata uthibitisho kutoka kwa diwani Makame Seif ambaye ni rafiki yake wa karibu sana wa Marehemu Hussen Ramadhani Mkiete maarufu kama Sharo Millionea amepata ajali mida ya saa mbili eneo la maguzoni Tanga na amefariki dunia papo hapo.

Polisi walitambua ni Sharo Millionea kwa vitambulisho vyake na picha moja ya passport aliokuwa nayo mfukoni ambavyo kwa sasa viko na polisi.
Diwani huyu alimfahamisha mwandishi kuwa Sharo Millionea aliumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono.
Pia Mjomba wa marehemu amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na asubuhi ya leo ratiba ya msiba ingetolewa.
Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo iliwasiliHospitali ya Teule ya Tanga mara baada ya kupata taarifa hizo.

 
Hii ndiyo gari aina Toyota Harrier yenye namba T278 BVR iliyopinduka na kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha msanii Sharo milionea jana usiku mishale ya saa mbili.











Monday, November 26, 2012

STUDENT’S SPECIAL BASH YATIKISHA DAR LIVE KWA WASANII WA NGUVU


Fid Q na Stamina wakifanya makamuzi ya hatari jukwaani.

Dullayo akiwapelekesha puta mashabiki.

Rich Mavoko akionyesha cheche zake jukwaani.

Kala Jeremiah akiwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.

Stamina akiwatuliza mzuka mashabiki.

P Square wa Bongo (waliovaa ‘jeans’ na miwani) na madansa wao, wakilishambulia jukwaa.

Tano Bora wa shindano la The Mic King wakiwa katika picha ya pamoja.

Wanenguaji wa ‘Twanga’ wakionyesha ‘matindo’ wakiwa chini.

Fid Q ‘Ngosha’ akikamua mbele ya mashabiki wake.

Dullayo akifanya vitu vyake.

Kala Jeremiah akitoa burudani ya aina yake stejini.

Mashabiki wakimshangilia Kala (hayupo pichani).

Sehemu ya mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini hapo.

Stamina akiwachombeza kwa staili mashabiki.
 
WASANII wa nguvu nchini wakiwemo Fid Q, Rich Mavoko, Dullayo, Kala Jeremiah, Stamina, bendi ya ‘Twanga Pepeta’, na mchuano wa wasanii wa muziki wa kufoka wa The Mic King waliwapagawisha maelfu ya wapenzi wa burudani waliofika katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

UGANDA YALEGEZA KAMBA , YAONDOA ADHABU YA KIFO KWA MASHOGA


Spika wa bunge la Uganda, Rebecca Kadaga.

Bunge la Uganda limeshindwa kupitisha sheria ya kuua watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja(ushoga) kama ilivyoahidiwa na spika wa bunge la nchi hiyo Rebecca Kadaga na badala yake bunge hilo limejikita katika kufanyia marekebisho muswada huo kwakutafuta tiba mbadala kabla ya kuisha kwa mwaka, ikiwa ni tofauti na spika huyo alipoongea na vyombo vya habari wiki mbili zilizopita alipoahidi kwamba sheria hiyo itapitishwa kabla ya kuisha kwa mwaka huu.

Lakini amerejea tena katika vyombo vya habari ijumaa iliyopita akisema kwamba hawatapitisha sheria hiyo kwasasa mpaka hapo baadaye akidai kwamba wametoa zawadi ya Christmas kwa mawaikili wa watu wanaojihusisha na vitendo vya kishoga akidai kwamba wamekuwa katika kampeni kwa muda mrefu ya kupinga sheria kali za serikali ya Uganda dhidi ya matendo ya ushoga.

Uganda ni kati ya nchi za kiafrika ambazo zina msimamo mkali juu ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, awali kwa upande wa bwana James Nsaba Buturo ambaye ni waziri mstaafu wa maadili wa serikali na kiongozi wa umoja wa maendeleo ya maadili nchini humo amesema hakuna maswali juu ya hilo anauhakika wa asilimia 99 kwamba muswada huo utapitishwa na kuwa sheria kamili.

Amesema kama kuna kiongozi yeyote nchini humo ambaye anayeonea huruma mambo ya ushoga hawezi kuthubutu kusema hadharani kwakuwa anajua waganda hawataki utamaduni huo katika nchi yao.Uganda imebakia na msimamo dhabiti juu ya vitendo vya kishoga nchini humo licha ya kelele nyingi kutoka mataifa ya magharibi ambao wameonekana kuzitishia nchi zitakazokataa maswala ya ushoga zitanyimwa misaada hali iliyofanya nchi kama Malawi kulegeza kamba juu ya vitendo vya kishoga.


POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...