Saturday, March 31, 2012

ANGALIA JINSI DIAMOND ALIVYOKUWA AMEJIANDAA KWA SHOO YA "DIAMOND ARE FOREVER" NA MASHABIKI ZAKE


UKIZUNGUMZIA shoo kali kumi zilizoteka mioyo ya mashabiki hapa nchini na ukaacha kuizubgumzia shoo iliyopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, basi utakuwa hufuatilii kwa makini burudani zinazofanyika Bongo.

Shoo ya “Diamond Are Forever”, iliyochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku wa Machi 30, mwaka huu ni funga kazi ambayo kwa hakika ni namba moja kati nyingi zilizowahi kufanyika hapa jijini Dar.

Shoo hiyo ilipigwa na Nasseb Abdul ‘ Diamond’ au ukipenda unaweza kumwita ‘Platinum’ ilianza majira ya saa nne usiku na kuhudhuriwa na baadhi ya mastaa wa Bongo, akiwemo mpenzi wa zamani wa Diamiond, Miss Tz mwaka 2006 na mcheza filimu,Wema Isaac Sepetu.

Diamond alidhihirisha kuwa ana jina na uwezo wa kujaza mashabiki zaidi ya elfu moja peke yake bila msaada wa msanii mwingine.

Pamoja na shoo hiyo kutawaliwa na vituko vya hapa na pale kutoka kwa Diamond na Wema bado mashabiki walipata fursa ya kufurahia na wengine kukubaliana na uwezo wa Diamond katika kulitawala jukwaa.




Mwanamitindo anayeitendea haki fani hiyo nchini, Martin Kadinda katika pozi, na huyu ndiye aliyemvalisha Diamond na wote unaowaona wamevaa vikoti kama hivi vyake.































































Mavazi yaliyotawala katika shoo hiyo ukiachilia mbali la Mchomvu na Baby wake, yamebuniwa na Mwanamitindo anayeshika kasi Bongo, Martin Kadinda aliye katika picha ya pili juu.

DIAMOND ARE FOREVER BURUDANI MWANZO MWISHO!!!

Wanenguaji wa THT, wakiwa wamembeba juu Diamond wakati wa shoo hiyo.

Diamond akionesha uwezo wake katika kucheza.

UKIZUNGUMZIA shoo kali kumi zilizoteka mioyo ya mashabiki hapa nchini na ukaacha kuizubgumzia shoo iliyopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, basi utakuwa hufuatilii kwa makini burudani zinazofanyika Bongo.

Shoo ya “Diamond Are Forever”, iliyochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku wa Machi 30, mwaka huu ni funga kazi ambayo kwa hakika ni namba moja kati nyingi zilizowahi kufanyika hapa jijini Dar.

Shoo hiyo ilipigwa na Nasseb Abdul ‘ Diamond’ au ukipenda unaweza kumwita ‘Platinum’ ilianza majira ya saa nne usiku na kuhudhuriwa na baadhi ya mastaa wa Bongo, akiwemo mpenzi wa zamani wa Diamiond, Miss Tz mwaka 2006 na mcheza filimu,Wema Isaac Sepetu.

Diamond alidhihirisha kuwa ana jina na uwezo wa kujaza mashabiki zaidi ya elfu moja peke yake bila msaada wa msanii mwingine.

Pamoja na shoo hiyo kutawaliwa na vituko vya hapa na pale kutoka kwa Diamond na Wema bado mashabiki walipata fursa ya kufurahia na wengine kukubaliana na uwezo wa Diamond katika kulitawala jukwaa.

Wasanii kutoka THT Elias Barnabas (kulia) na Amini wakimpa sapoti Diamond.

Diamond akicheza juu ya meza aliyokuwa ameketii Wema na marafiki zake.

Q Chief, akiimba huku amekaa chini katika shoo hiyo muda mfupi baada ya kukaribishwa na Diamond.

… akikumbatiana na mama yake mzazi.

Wema Sepetu akishangalia wakati Diamondi akicheza.

Jokate naye akicheza kwa furaha.

Diamond akiserebuka na mmoja wa mashabiki zake.

Wema akimtunza Diamond, ambaye alikataa kupokea mkwanja wake

Wema akionesha hudhuni baada ya Diamond kukataa kupokea fedha zake na kurejea kwenye meza yao.

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiingia ukumbini hapo.

Wema Sepetu wakati akiingia Ukumbini.

Diamond, Mama yake Mzazi na Queen Doreen wakiwa katika pozi mara baada ya kuwasili ukumbini.

Diamond na Mama yake wakiwasili.

Ndugu na marafiki wa Diamond, wakihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili ukumbini.

Mwanamitindo Martin Kadinda akihojiwa mara baada ya kuwasili ukumbini hapo.

Diamodi akiimba huku amempigia magoti Aunt Ezekiel.

Baadhi ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo wakiserebuka.

Friday, March 30, 2012

ROMA, IZZO B IMEBAKI SIKU MOJA

BEST AFRICAN MUSIC OF 21ST CENTURY "NGOMA AFRICA BAND"



THE NGOMA AFRICA BAND
It's the first African band to use is music as cross culture bridge from Tanzania in East Africa to the World! Ngoma Africa Band wich has been named The Golden Voice of East Africa is a fast-growing band with a huge fans base worldwide.Its's the first African band to use is music as cross culture bridge from Tanzania in East Africa to the World. Ngoma Africa Band, a Tanzanian band base in Germany,founded in the year 1993 by Ebrahim Makunja aka ras makunja,named several time is the best band in many festivals. This is beacuse of the way the band presents itself Live on stage.It penetrates the souls of the fans and automatically the audience became crazy!,especially when the band applies the EXTRA ORDINARY "Bongo Dansi" or "MZIKI WA DANSI" wich simple means danceable music from Tanzania.
The Fans found rhythm unique,you only can hear this beat when the Ngoma Africa band plays.Because of this reputitation of sends fans crazy with the beats and rhythm.



Ngoma Africa band have numbers of talented musician's including mult-talented soloist Christian Bakotessa aka Chris-B,other is
Said "Jazbo" Vuai,Maxime Buanda,Richard Makutima, Severn Okomo,Diva Bedi Beraca aka Bedi Bella and others
The spirit of the Ngoma Africa Band unites with the sprits and souls of the fans and other audience.
The Ngoma Africa Band have released the album "Mama Kimwaga"(sugar Mum),also numbers of Hit sigles CD,like Apache wacha Pombe(Stop over Drinking alcohol),Anti-Corruption Squard,Single CD "Jakaya Kikwete 2010".
Most of the songs are written in various east African languages.But majority in SWAHILI or KISWAHILI the spoken language in Tanzania and its neighbouring east African countries.



The Ngoma Africa Band bellong to the fans!Musician are just the servant'sIt's the first African band to use is music as cross culture bridge from Tanzania in East Africa to the World!




Listen songs at www.ngoma-africa.com and be connected at contact@ngoma-africa.com
AIRTEL YAWATANGAZA WASHINDI WA PROMOSHENI YA "NANI MKALI"


Afisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi.
Jane  Matinde  akitanzanga washindi wa  promosheni ya Mkali nani kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) ambapo washindi wa siku
hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki
hujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kulia ni Afisa
mawasiliano wa kampuni ya Airtel Bi. Dangio Kaniki akishuhudia  tukio
hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini
Dar-es-Salaam.

 
Airtel yawatangaza washindi wa "Nani Mkali" promosheni

*         Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki atangazwa
29, March 2012 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma
nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewatangaza
washindi wa wiki hii ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo
washindi wa kila siku watakabidhiwa shilingi milioni moja kila  mmoja
na mshindi wa wiki ataondoka na shilingi milioni tatu. Washindi hao
wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Arusha,
Zanzibar, Dar es Salaam, Nzega - Tabora na Manyara
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel
Dangio Kaniki alisema" Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania
kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa
washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika
promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali.  Na leo napenda kuchukua fulsa
hii kuwatangaza washindi wa wiki hii ambao ni
KAANAEL LEMLE KANUYA

ARUSHA

50

          1,000,000.00

RAKESH MANSUR DEYAL

ZANZIBAR

34

          1,000,000.00

NAPEGWA DAVID MONGO

DSM

58

          1,000,000.00

MARIAM WAZIRI HAMISI

DSM

32

          1,000,000.00

GUVANTRAI SACHDEV SHANTILAL

ARUSHA

54

          1,000,000.00

YUSUPH NOHAI ANNAI

MANYARA

35

          1,000,000.00

YUSUPH  MATHIAS MANONI

NZEGA-TABORA

25

          3,000,000.00


Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha
washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya
kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu
yetu ya jisikie huru, aliongeza Dangio
 kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na
kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali
na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo
sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja
na kodi.                                                        

Thursday, March 29, 2012

SUPER SHINE MODERN TAARAB WAJIMWAYA MWAYA USIKU WA VIDOLE JUU DAR LIVE

Mmoja wa viongozi wa Super Shine Modern Taarab, Hassan Zumo, akiimba.



Mcheza shoo wa bendi hiyo akitoa ‘machejo’ ya kiduku.

Bendi ya muziki wa mwambao ya Super Shine Modern Taarab, usiku wa kuamkia leo ilionyesha uwezo mkubwa wa baadhi ya waimbaji wake baada ya kila mmoja kupanda jukwaani na kuimba wimbo wake, ndani ya Kiwanja cha Taifa cha Burudani cha Dar Live, ilipokuwa ikitoa shoo ya ‘Usiku wa Vidole Juu’ ambao hupatikana kila siku ya Jumatano.

Baadhi ya wapiga vyombo na waimbaji wa bendi hiyo wakiwajibika.



Mmoja wa waimbaji wa kike wa bendi hiyo akionyesha uwezo wake.




IDD AZZAN, AWA MGENI RASMI MIAKA 4 YA MAZOMBI CAMP

Aunt Ezekiel akimrisha keki Mh. Idd Azzan iliyokuwa imeandaliwa katika sherehe hizo.

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azzan, usiku wa kuamkia leo alijichanganya kwenye sherehe ya kutimiza miaka minne ya Mazombi Camp zilizofanyikia kitongoji cha Ally Maua Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na watu wengi wakiburudishwa na wasanii wengine mbalimbali wa filamu na muziki, wakiwemo Aunt Ezekiel, Tip Top Connection, TMK Family, AT, Shilole, Godzillah, 20%, AY na Mwana FA, ambao walitoa burudani za kutosha

Shilole naye akirishwa keki hiyo.

Mh. Idd Azzan (wa kwanza kulia), akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa mahali hapo.

 
AT akitoa burudani mahali hapo.

Wasanii kutoka kundi la TMK Family Chege na Temba wakikamua mahari hapo.

Dogo Janja akipagawisha mahari hapo.

Godzilah akionyesha uwezo wake.

Wasanii wanaounda kundi la Tip Top Connection Tunda Man na Madee wakipagawisha.

Aunt Ezekiel (katikati), akikata keki hiyo mapema kabla ya kumrisha Mheshimiwa na wageni wengine.

Mwenyekiti wa Mazombi Camp akirishwa keki hiyo.

Mmoja wa waigizaji wa filamu Daudi Kipunguni akirishwa keki kwenye hafla hiyo.

20% akitoa burudani mahari hapo.

Shilole akiwa amezingilwa na baadhi ya wadau wa Mazombi Camp, wakati akitoa burudani.

AT, Shilole na wanenguaji wao wakipagawisha.

Mh. Idd Azzan akiongea jambo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo.

 
… akishuka jukwaani hapo.

Mashabiki waliofurika kwenye hafla hiyo wakiserebuka.

Muonekano wa umati huo.







POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...