Thursday, February 28, 2013

TICKETS KWA AJILI YA SHOW YA BEYONCE UK ZIMEISHA NDANI YA DAKIKA 10



Sekunde kadhaa baada ya tiketi kuingia sokoni kwa ajili ya UK world tour ya Beyonce inayoitwa
"Mrs. Carter" siku ya juma mosi asubuhi,kuuzika zote ndani ya dakika 10
(sold out) mashabiki waanza kufurika kwenye internet na malalamiko kwamba
kila show ticket zimeisha na watu wamejitosheleza (sold out)

lakini masaa machache baadae, scores za ticket zimeanza kujionyesha kupitia katika
sites za brokers wakiziuza kwa paund 660 kila moja, ambayo ni zaidi ya shilingi
1,500,000 za kitanzania, na muuzaji mmoja akiuza ticket 6
kwa paund 2,000 kupitia eBay.


kuuzika kwa ticket hizo na kumalizika ndani ya dakika 10, kunasababisha kuwepo kwa
tuhuma kuwa inawezekana Beyonce na uongozi wake wamezinunua wenyewe, kama
justine Beiber na Taylor Swift ambao walikamatwa wakifanya hivyo mwaka jana

LINEX AMVISHA MCHUMBA WAKE PETE KIMYA-KIMYA



Weekend hii, mtu mzima Sunday Mjeda aka Linex aka Mr VOA (Voice Of Africa),
alifanya yake kwa kumvisha pete mpenzi wake, ambae ni ambae ni mwenyeji wa Finland anaeitwa Suvi.
Linex aliamua kufanya kimya kimya tena wakiwa wawili tu,
kwasababu hakutaka kujionyesha, na anaamini ile ni kitu
very personal haikuhitaji manjonjo mengi...all in all blog hii
inakutakia kila la kheri...!!



Linex na mchumba wake






RAIS KAGAME AMPA UWAZIRI MTANZANIA, NI PROFESASILAS RWAKABAMBA WA MKOA WA KAGERA.


RAIS Paul Kagame.
Kwa ufupi: Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi). 
Baada ya kumaliza elimu ya msingi wilayani Muleba alijiunga na shule ya sekondari Ihungo, Kagera.
-WASIFU:
-Aliwahi kuwa mkuu wa kitivo cha Uhandisi Dar es Salaam.

-Alikwenda Rwanda mwaka 1997 baada ya Rais Kagame kuwaomba wahadhiri UDSM kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa hilo.

RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda.

Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).

Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija...

“Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”

Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.

“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.

Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.

Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.

Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.

Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.

Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.

Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.

Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu.

JOHN MNYIKA.....NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAWO WA UMEME, SERIKALI IELEZE WANANCHI UKWELI NA HATUA KUHUSU UDHAIFU KWENYE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA DHARURA



Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012.


Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.


Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo.


Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.




Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme.


Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012.


Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika.


Wenu katika uwakilishi wa wananchi,


John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

MSANII OMOTOLA ANG'AA HOLLYWOOD


 
Muigizaji wa Nollywood, Omotola, Jalade- Ekeinde, ameanza kuonekan kwenye televisheni za Marekani, kwenye kipindi kiitwacho Bounce

Nyota huyo ambaye amekuwa Marekani kwa muda sasa ameanza kuonyesha uwezo wake mbele ya wakali wa Hollwood nchini Marekani

Baadhi ya wasanii mbalimbali kutoka Nigeria walishindwa kung'aa lakini msanii huyo amefanikiwa kushiriki kwenye tamthilia nchini Marekani

Katika tamthilia hiyo Omotola amecheza na Kimberly Elise

NIKKI MBISHI ASALUTI KWA LADY JAYDEE




Nikki Mbishi ni rapper usiyeweza kumfananisha na yeyote Tanzania kwa uwezo wake usioelezeka katika uandishi wa haraka wa mashairi yenye mistari konde na uwezo wa kufanya mitindo huru (freestyle). Pia ana kumbumbuku ya ajabu na akiwa na uwezo wa kuimba nyimbo za wakongwe kama Profesa Jay na hata wa Marekani utadhani kaziandika yeye.
Lakini pamoja na maisha yake ya muziki kuzungukwa zaidi na utamaduni wa Hip Hop, Nikki aka Terabyte huchukua muda pia kusikiliza muziki laini wa wasanii wenzake wa Bongo na kwa mtazamo wake Lady Jaydee ndiye msanii wa kike anayemkubali kuliko yeyote.

“Leo nimeamka na dada mkuu tu @JideJaydee hakuna kama huyu kwenye historia ya wanamuziki wa kike Bongo @GraceMatata fuata huyo dada.,” ametweet Nikki Mbishi.

Rapper huyo controversial ameendelea kutweet majina ya nyimbo kibao za nguli huyo wa muziki wa Tanzania ambaye jina lake halisi ni Judith Mbibo.

"MIMI SI MGONJWA.."...RAY AFUNGUKA


Picha hiyo ya kushoto inamuonesha alivyokuwa mwanzo..na kulia na jinsi alivyo sasa
------------




Muigizaji aliyepo kwenye list A ya waigizaji wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi aka Ray ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia anaumwa kutokana na kupungua mwili wake kwa kiasi kikubwa.

Ray amezikanusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo gazeti la udaku la Kiu wiki hii lilikuwa na habari isemayo, ‘Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa.

Hata hivyo Ray amesema hali hiyo imetokana na kufanya mazoezi zaidi siku za hivi karibuni. “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.

ALAMA JABIR AKERWA NA MGAO WA UMEME


S










Siku za hivi karibuni kumekuwepo na katizo la umeme la mara kwa mara katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kiasi cha kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi.
Kufuatia tabia hiyo ya Tanesco kufanya yao kila siku na kuwaweka wajasiriamali wanaotegemea umeme kwenye mawe, mtangazaji wa kipindi ca Mkasi, Salama Jabir, ameamua kuzipunguza hasira zake kwenye Twitter kwa kuandika:

Kazi inabidi ziende jamani…The f**k is wrong na hii nchi?!Umeme tu?????!Shida isotatulika miaka nenda rudi?!Tunachoshaaaana. F**k that shit!! Taarifa hakuna…kuunguziana mali tu,kulipa hamlipi,kauli nzuri hamna!! Who does that?! Well..Mnatufunza sana,Asanteni!!

Watu wakiamua kuishi nje serikali inalalamika Ooh vijana hawana upendo na nchi yao!!Utapendaje nchi inayokurudisha nyuma? What the f**k?! Well KZMZ!!!


Alosema bora mthamini mbwa naona hakuwa mbali na Ukweli..Ki ukweli misemo ya wahenga yote ni ukweli mtupu, again…KZMZ.

Nimejipigapiga mwenyewe nikanunua kaTV ka kitundika ukutani kama tunazoziona kwenye TV mkaunguza,nikarudisha dukani watengeneze.

MAPACHA WATATU KUZINDUA YARABI NAFSI MARCH 2

Waimbaji wa bendi ya Mapacha watatu Khalidi Chokolaa (kushoto) na Jose Mara wakiwa wameshika CD ya albam yao mpya Dar es salaam jana watakayoizindua March 2 katika ukumbi wa bussines park.

Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wao

Msanii wa bendi ya mapacha watatu Catherine Fidelic ' Cindy' akiimba mbele ya wana habari

BABA MTAKATIFU BENEDIKTI XVI AKUTANA KWA MARA YA MWISHO NA WAUMINI ST. PETER'S SQUARE



Umati Mkubwa wa Waumini

Moja la jukwaa kubwa la wapiga picha wa kimataifa

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome alikuwepo kuiwakilisha Tanzania.

Wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma walikuwepo pia.

Baba Mtakatifu akiingia kwenye St. Peter's Square

Picha ya Baba Mtakatifu alipotupitia Karibu huku akitubariki

Bendera ya Tanzania


Baba Mtakatifu Benedikti XVI tarehe 27 Februari amekutana na waumini kwa mara ya mwisho kabla ya kung'atuka kwenye nafasi yake ya kuliongoza kanisa katoliki hapo kesho kwenye mida ya saa mbili za usiku.


Umati mkubwa wa watu ulijumuika nje ya kanisa la Mtakatifu Petro kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kuliongoza kanisa katoliki kwa kipindi cha miaka 8 tokea kuchaguliwa kwake.Itakumbukwa kuwa Baba Mtakatifu Benedikti XVI alichaguliwa kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha Baba Mtakatifu John Paul II. Mwenyezi mungu amuongoze Baba mtakatifu kwenye maisha yake yote nje ya uongozi wa Kanisa katoliki.


Jumuiya ya Watanzania Roma ikiongozwa na Katibu wake ilikuwepo kuiwakilisha Tanzania kwenye siku hii ya Kihistoria duniani. kwa picha zaidi mnaweza kutembelea hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.


Picha zote zimeletwa kwenu na Andrew Chole Mhella (Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma)

Wednesday, February 27, 2013

RIHANNA NA CHRIS BROWN WARIDHIA KUFUNGA NDOA JULY MWAKA HUU



Jarida maarufu (Star Magazine) limeripoti kwamba mastaa wa muziki Chris Brown na Rihanna wanampango wa kufunga ndoa mwishoni mwa July 2013 nyumbani kwa kina Rihanna huko Barbados.

Jarida hili limeendelea kutiririka kwamba kwenye ndoa hiyo wamepanga kusherehekea na watu mbalimbali wakiwemo wanaoamini kwamba Chris Brown amebadilika kitabia.

Ni harusi ambayo watu wote walioalikwa watakua wamesimama na wahudumu watakuepo kumfata kila mtu alipo, pia wale wachoraji wa tattoo watakuepo pia.

OMOTOLA NA GENEVIEVE NNAJ HAKUNA BEFU TENA




Stori za kuaminika kutoka kwenye ardhi ya Nigeria ni kwamba beef iliyokuepo kati ya waigizaji mastaa wa Nigeria Omotola Jalade na Genevieve Nnaji imekwisha ambapo kuonyesha kwamba uhasama umefutika Genevieve alihudhuria suprise ya pili ya birthday ya Omotola Jalade kama inavyoonekana kwenye hizi picha.

Wengine waliohudhuria ni Bimbo Akintola, Monlisa Chinda, Guild of Nigeria president Ibinabo Fiberisima, Chidi Mokeme, pamoja na mwimbaji staa wa Nigeria Banky W, Sound Sultan na wengine.



Omotola na Genevieve Nnaji.


.





.

RIPOTI KAMILI KUHUSU KUFUNGWA KWA VITUO VIWILI VYA REDIO PAMOJA NA FAINI WALIYOTOZWA CLOUDS FM



Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari  jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo

KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake  kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.

Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.


Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa

uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.


Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa kufanya.

Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa wakiviamini vituo hivyo.

Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.

Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo



*MSD YAWEKA WAZI WANAOWALINDA WANAOTOROSHA DAWA NJE YA NCHI


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti z\ilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini.

Meneja wa Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi ikiwemo Cameroon.
Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati ya usajili wa maduka ya dawa baridi vijijini wakati wa kongamano hilo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO

Monday, February 25, 2013

PICHA: PENZI LA DIAMOND NA PENNY SIO SIRI TENA!








tagazo

MCHUNGAJI ALIYEKUBALI KUWATAHIRI WATOTO WAKE ARUSHA AVULIWA NGUO ZOTE NA KUCHAPWA VIBOKO



Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo katika kata ya Ngusero mkoani Arusha aliyedhalilishwa na vijana wa jamii ya kifugaji kwa kuvuliwa nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na kisha kutandikwa viboko amesema atanunua bunduki na kuitumia kuua endapo Serikali haitachukua hatua.

Mchungaji huyo alifanyiwa udhalilishaji huo hivi karibuni baada ya kuwatahiri wanawe katika hospitali ya Kiteto, jambo ambalo vijana wa jamii hiyo walisema ni kosa kwa kwenda kinyume na mila na desturi ya kuwatahiri kimila, na hivyo kumvua nguo, kumchapa, kumpiga na kumjeruhi.

Mchungaji huyo anasema aliripoti shambulio hilo katika kituo cha polisi na amekuwa akifuatilia lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya vijana hao wala kuulinda usalama wake ikiwa ni pamoja na kuenedelea kupewa vitisho. 
habari/picha:mpekuzi blog

ODAMA ASEMA ,,,,SITEGEMEI MWANAUME KAZI NDIO KILA KITU KWANGU



Jenifa kyaka (Odama)



Mwanadada nyota kutoka bongo movie Jenifa Kyaka Odama amefunguka na kusema katika maisha yake hategemei wanaume na ndio siri ya mafanikio aliyo nayo kwa sasa

Mwanadada huyo amesema anashukuru Mungu kwa kila hatua anayopiga na kwa sasa amejipanga kuhakikisha anafanya vizuri sana katika tasnia hii ya filamu hapa nchini.


Odama amekanusha vikali uvumi uliozagaa kuwa mambo yote anayofananya ni msaada kutoka kwa pedeshee flan hapa mjini na badala amesema kila kinachoonekana ni juhudi zake binafsi na hakuna mkono wa mwanaume unajua watu wakimuona mwanamke kafanikiwa wanadhani ni nguvu ya mwanaume kiukweli hili huwa linaniumiza sana na ndio sababu tosha inayonifanya nisonge kila kukicha.


Hapa akikagua camera

Mwana dada Odama ameendelea kusema kuwa anajua anachokifanya hivyo haoni sababu ya kuongozwa na mtu mwingine,
Amesema anafanya kazi kwa bidii sana na ndio maana alisafiri kwenda china kwa ajili ya mahitaji ya kampuni yake ya J-FILIM 4 LIFE Ambayo imeshatengeza filamu kibao zinazofanya vyema sana dukani kwa sasa


Odama ametoa wito kwa wasanii wachanga na hata mastaa kuwa hakuna kitu kizuri kama kujituma kwani unapofanya kazi kwa bidii basi jua pesa zitamiminika tu ila ukikaa na kupiga domo basi utaishia domo kwani pesa zinatafutwa na hazitutafuti sisi..Nachoshauri kina dada wenzangu tufanye kazi tukikaa na kusema bila vitendo tutabaki kilalamika kila siku maana hakuna kitu kibaya na adui wa pesa kama uvivu.Odama alizidi kutiririka na kusema kama kuna wanawake haswa mastaa wenye tabia za kuwa tegemezi waache kwani siku wakigombana wajue ndio mwisho wa kupata pesa ila ukiwa na chako huwezi kuteseka.


Akiendelea kununua

Kwa sasa mwanadada huyu amesema anajipanga na atafanya fila kubwa na ya historia ambayo itakayotumia gharama kubwa sana kwa wengi wawatakaoshiriki watatoka nje ya nchi bila kufafanua nchi gani na wanaotoka nje wanakuja kama wasanii au crew.

Kwasasa Odama anamiliki biashara zake na ana mipango kibao ambayo itakamilika muda si mrefu kama mungu akitujalia na kila mtu atajua Odama anataka kufanya
Wakizungumza na sisi kwa nyakati tofauti mashabiki wa filamu wamesema wanamkubali sana mwandada huyu kwani anakwepa sana kuandikwa kwa habari za uwongo pili wanamkubali kwani ni mwanadada mpiganaji mwenye ndoto kubwa sana za maisha bora.


Hapa akikagua stick ya boom

Odama amefunguka kuwa ana amini filamu aliyoifanya na kuwashirikisha Riyama Ally, Cath na wasanii wengine wengi itafanya vizuri sana sokoni kwani ni filamu nzuri na ina mafunzo na ana amini itapendwa sana kwani watu waliocheza wamefanya vizuri sana

SIMBA YAKATWA MKIA NA MTIBWA SUGAR, YAFUNGWA 1-0



Kikosi cha Simba kilichoanza katika mchezo wa leo.

Kikosi cha Mtibwa Sugar.

Mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba akichuana na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaban Nditi.


Wachezaji wa akiba wa Simba wakiwa hawaamini macho yao wakati jahazi la timu hiyo likiwa linazama

Golikipa wa Mtibwa Sugar, Hussein Shariff akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mtibwa imeshinda bao 1-0.

Waamuzi wa mchezo wa jana wakitoka uwanjani
Kocha wa Simba, Patrick Liewig akitoka uwanjani baada ya mchezo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...