Wednesday, February 29, 2012

WAKALI HAWA KUKAMUA DAR LIVE J2 HII

VODACOM YATOA MIKOPO YA KIFEDHA KWA VIKUNDI VYA KINAMAMA MKOANI MANYARA

 Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akiongea na wakina mama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mara alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama, ambapo urudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba, Mikopo hiyo huendeshwa na Mfuko wa kampuni hiyo MWEI kupitia Vodacom Foundation, zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba (9,700,000).


Bi.Johari Mwaselela wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,akisaini nyaraka za kupewa mkopo wakati Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wapili toka kulia alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama, Huduma hiyo ya Mikopo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa kusaidia wakinama MWEI na kurudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba, zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba (9,700,000) kulia ni Afisa wa Mradi huyo Ally Mbuyu na kushoto ni Meneja wa Mradi huo Mwamvua Mlangwa.


Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akimkabidhi mmoja wa kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, fedha za mkopo unaolenga kuwakomboa wakinamama hapa nchini, Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa (MWEI) na kurudisha fedha hizo bila riba kwa njia ya m-pesa, zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba (9,700,000).


Baadhi ya kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Ofisa Mkuu na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, wanne toka kushoto na Meneja wa Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa mara baada ya kufika hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama kijijini hapo, Mikopo hiyo urudishwa bila riba kwa njia ya m-pesa, Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kwa kupitia Mradi wao wa MWEI, zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba (9,700,000).




· Akabidhi mikopo nafuu kwa vikundi tisa vya Mirerani
· Ni kupitia mradi wa MWEI


Na Mwandishi wetu
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Bi. Mwamvita Makamba amewataka wanawake wajasiriamali hususan wadogo kutambua kuwa maendeleo ya biashara zao na hatimae hali zao za kiuchumi kutategemea pamoja na mambo mengine namna wanavyotumia vizuri fursa za uwezeshaji wanazotengenezewa.

Bi. Mwamvita ametoa changamoto hiyo Wilayani Simanajiro, Mkoani Manyara katika kijiji Cha Mirerani wakati akikabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Tisa kwa vikundi tisa vya akina mama iliyotolewas na mradi wa Vodacom wa kusaidia wajasiriamali wadogo wanawake wa MWEI.

Bi. Mwamvita amesema kadiri ambavyo wanawake watakuwa tayari kutumia vema fursa wanazotengenezewa ikiwemo ya MWEI wanajiweka katika nafasi nzuri ya kujiwezesha kiuchumi na kuondokana na dhana kwamba mwanamke ni kiumbe tegemezi.
“Wanawake wenzangu leo Vodacom inapowakabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana ni fursa adhimu sana kwenu, ni wajibu wenu kutumia vema fursa hii kujiinua kama ilivyokuwa wajibu wa Vodacom kuwatafuta, kuwafikia na kuwawezesha, kazi sasa ni kwenu”Alisema Bi. Mwamvita.

Bi. Mwamvita amesema kumekuwepo na kilio kikubwa cha wanawake wajasiriamali wadogo kutofikiwa kwa urahisi ama kukosa uwezo wa kukopesheka kutoka taasisi za fedha, hivyo katika kutimiza azma ya kubadili maisha ya watanzania Vodacom ilibuni mradi wa MWEI kutatua changamoto hiyo.

“Ni vigumu kupata taasisi itakayokukopesha mfnyabishara wa vitumbua, genge mchuuzi wa samaki, msusi n.k tena bila riba wala dhamana na zaidi kukupatia mafunzo ya ujasiriamali kwa gharama zake, Vodacom licha ya kwamba biashara yetu ni huduma za simu imethubutu kubuni mradi wa mikopo kwa kuwa inapenda kuona maisha ya watanzania wakiwemo akina mama yanabadilika”Aliongeza Mwamvita

Aidha Bi. Mwamvita amewataka wanawake hao kuhakikisha mikopo waliyoichukua inleta tija katika biashara zao hasa kuinua mitaji ili nao waweze kusimama na kusaidia wanawake wengine.

“Kabla ya kuwakibidhi mikopo hii tumewapatia mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo somo la utunzaji wa mahesabu ya biashara, tutumie elimu hiyo na mikopo hii kujiimarisha ili kuinua sauti zetu kwenye jamii”Aliongeza Mwamvita huku akisindikizwa na vigelegele vya furaha kutoka kwa akina mama.

Mradi wa MWEI ni mahsusi kwa ajili ya kusaidia akina mama nchini kama mchango wa Vodacom kuunga mkono juhudi za kitaifa za kumwezesha kiuchumi mwanamke wa kitanzania na unalenga hasa wanawake wenye biashara zenye mitaji ya kati ya Sh. 5000 na 200,000
Bi. Mwamvita amesema kuwa mradi wa MWEI umejiwekea lengo la kuwafikia wanawake wengi zaidi hususan maeneo ya vijijini ambao pamoja na kujituma katika bishara ndogondogo wanakabiliw ana uchache wa fursa za uwezeshaji.

“Ni hatua muhimu katika maisha yetu kama Vodacom kusaidia ujenzi wa ustawi wa jamii hapa nchini, tuna namna nyingi ya kubadili maisha ya watanzania kama dira yetu invyosema, MWEI ni namna mojawapo”. Alisema Mwamvita.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa mikopo hiyo mbali na kuishukuru Vodacom, wanufaika hao wameahidi kuitumia vizuri mikopo hiyo ili kutimiza malengo ya kibiashara waliyonayo.

“Wengi wetu hapa ni wajasiriamali wadogo tunaojishughulisha na biashara za ususi, mama lishe n.k changamoto kubwa tuliyokuwa tukikabiliana nayo ni kuweza kufikiwa na mikopo nafuu, leo tunafuraha kuona tumepata mikopo isiyo na riba hata shilingi moja” Alisema Johari Mwaselela Mmoja wa viongozi wa Vikundi.

Amesema kupitia vikundi vyao, watahakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na kuhimizana ili mikopo waliyopatiwa itoe tija ya kuinua mitaji yao, wakuze faida sambamba na kusaidia kubadili hali zao za maisha.

Tunawaomba Vodacom kama mlivyotufikia sisi hapa kijijini muwafikie na wenzetu wengine waliopo vijijini kama sisi na muwaokoe, kwa kweli wanawke bado tupo nyuma, tunawashukuru sana MWEI.”Aliongeza Mamam Mwaselela.

Awali Meneja wa Mradi wa MWEI Bi Mwamvua Mlangwa alisema hadi kufikia Januari mwaka huu kiasi cha Shilingi 150 Milioni kimeshatolewa na kunufaisha akina mama zaidi ya 6,000
Bi. Mwamvua amesema idadi ya wanaohitaji mikopo hiyo ni kubwa hivyo amewasihi kina mama hao wa Mirerani kutumia vizuri fursa hiyo na kuhakikisha wanarudisha mikopo kwa wakati ili kuwafikia wanawake wa sehemu nyengine nchini.
Kupitia mradi wa MWEI Vodacom huvipatia vikundi vya akina mama mikopo pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kazi ambayo hufanywa na Shirika la kuhudumia viwanda Vidogo – SIDO kwa gharama za Vodacom.

Mikoa ya Arusha, Manyara, Morogoro, Tanga, Rukwa na Katavi, Dodoma, Mara, Mwanza,Shinyanga na Pwani imeshanufaika na mikopo ya MWEI tangu mradi huo ulipoanzishwa mwaka 2011.

Mwisho.
HAPPY BIRTHDAY SSEBO & LADYNAA!!!



Ssebo akiwa kwenye pozi na marafiki zake
MTANGAZAJI wa Magic FM, Denis Busulwa ‘Ssebo’, usiku wa kuamkia leo alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake na mrembo mmoja aliyefahamika kwa jina la Nasra a.k.a Lady Naa ndani ya ukumbi wa New Maisha Club Masaki jijini Dar es Salaam.





Baadhi ya wafanyakazi wenzake na Ladynaa wa pili kutoka kulia.




Sintah akisimamia zoezi la shughuli hiyo kama MC.




Ssebo, Ladynaa na rafiki yao katika pozi.




Sintah, Ladynaa & rafiki yao





Ssebo & Ladnaa katika pozi









Ssebo (kulia), akikata keki na Lady Naa.

Ssebo akimlisha keki mmoja wa marafiki zake.

Keki ya birthday.

Lady Naa, akishangiliazoezi la kufungua shampeni.

Warembo waliokuwa katika hafla hiyo.

Mcheza sinema, Jacqueline Wolper, akiwa na Lady Naa.

Lady Naa akimlisha keki rafiki yake.



Tuesday, February 28, 2012

ACHEZEA KICHAPO KWA WIZI WA NYAMA


 
Kijana huyu aliyefahamika kwa jina la George Julius amechezea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kupola nyama na kwenda kujificha katika choo cha stendi kuu ya magari yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro.



ASKARI wa Doria akimuokoa kijana huyo tayari kwa kumfikisha kituo cha polisi cha mtaa wa Kitope Morogoro.

Friday, February 24, 2012

SUPER NYAMWELA, DANGER BOY WAITEKA MZALENDO PUB

 
Kiongozi wa wacheza shoo, Super Nyamwela akichuana na Danger Boy katika kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Mzalendo Kijitonyama Dar es Salaam

 
Super Nyamwela, Danger Boy, wakichuwana.

 
Wacheza shoo wa bendi hiyo wakifanya makamzi ya nguvu.

 
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky akicheza wakati mcheza shoo wake Danger Boy akimshudia
 
MKURUGENZI wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky ameibomoa safu yambele ya Bendi ya Stone Mayasika.
Akizungumza na mtandao huu Chocky alijijitea kuwa si yeye aliyefanya hivyo

bali ni wacheza shoo wenyewe wameamua kuihama kwa mapenzi yao na maslahi

yao binafsi.

Wakizungumza na mtandao huu walisema ukweli kuwa Extra Bongo iko

juu,kuanzia kwenye jina huwezi kuilinganisha na Stone Mayasika,pili Extra

Bongo ina wapenzi wengi ukilinganisha na Stone Mayasika,tatu ni bendi

inayoongoza kwa sasa katika Bendi za muziki wa Dansi na mwisho ni maslahi

ndio yaliyowatoa Stone Mayasika kwenda Extra Bongo.

Kiongozi wa wacheza shoo, Super Nyamwela alisema ni kweli wacheza shoo hao

wapo na tayari wameshaanza kucheza wakati wakiwa kambini kufundishwa

yaliyopo na yanayojili Extra Bongo.

Extra Bongo leo watakuwa viwanja vya Kijichi,kesho jumamosi ni katika

Uwanja wa Nyumbani Meeda Sinza Dar es Salaam na jumapili ni Dar Live

Mbagala.

Thursday, February 23, 2012

TAMKO LA G-SOLO KUHUSU SUGU NA RUGE


G- Solo akiwa na mwanye...


NI LAZIMA SUGU NA MKOLONI MNAJUA CHANZO CHA HAYA YOTE MLIYO AFIKIANA NA RUGE NA MWISHO WA MAAFIKIANO LAZIMA YAMEKUWA NA MANUFAA KWENU NYINYI NA SIO WASANII WA TANZANIA AMBAO TUKO KWENYE HALI NGUMU NA NYINYI MNAJUA. NAFIKIRI NAFSI ZENU ZINAJUWA KWANINI MMEFANYA HIVI. LAKINI SISI WENZENU TULIOBAKIA TUNAPENDA KUUAMBIA UMMA HATUJUI,



NA WALA HATUKUA TUNAJUA, NA HATUTOTAKA KUJUA, ILA MZIGO HUU WA MAAFIKIANO NYINYI NDIO WAKU UBEBA. SERIKALINI KUNA WATU WENGI WANA UHASAMA TENA MKUBWA, KWANINI SERIKALI ISHUPALIE KUWAPATANISHA SUGU NA RUGE? NA NINA IMANI SUGU ANGEKUWA SIO MMBUNGE RUGE ASINGEOMBA SULUU KWANI HATA NYINYI MNAJUA NI JINSI GANI TULI HASTLE PAMOJA SERIKALINI NA KWENYE IDARA NYETI KUMSAIDIA SUGU APATIWE HAKI ZAKE TENA BEFORE KUWA MMBUNGE NA ILISHINDIKANA NA SERIKALI ILISIKIA NA HAIKUSEMA CHOCHOTE NA ILIKUWA WAZI KWELI NIGGA KADHURUMIWA KWA VIGEZO VYA USHAHIDI ALIVYOKUWA NAVYO.



SO IMEKUWA EASY KIASI GANI SUGU KUKUBALI YAISHE? NA KWENYE HII MOVEMENT KUNA WATU WENGI AMBAO NI FRONT LINERS KWANINI HATUKUSHIRIKISHWA? KWANINI IWE SIRI? MNAFAHAMU KAMA HII KITU INAGUSA MAISHA YA WATU WENGI? MNAFAHAMU KWA KILE MLICHO AFIKIANA NYINYI KIMECHANGIA BIASHARA ZA WATU KUHARIBIKA? NA SISI HATUPAMBANI NA VIRUS WAFU TU, BALI HATA SISI KWA SISI YEYOTE KATI YETU ATAKAYEZINGUA. SO RUGE AMETUMIA MBINU ILE ILE YA DIVIDE AND RULE TULIYOKUWA TUNA IKATAA NA KAFANYA HIVYO KWA KUSHIRIKIANA NA NYINYI SO MNATUAMBIA NINI?



NA MJUE UGOMVI ULIOPO KATI YA MITAA NA HAWA WAFU SIO SUGU TU, WALA SIO MARALIA TU, NI MAISHA YA KUNDI KUBWA LA WATU WALIOWEKA MATUMAINI YA MAISHA YAO KWENYE SANAA NA WAKALOSTISHWA KISENGE SENGE. NINACHOWEZA KUSEMA,,,, KWAKUWA NYINYI NDIO MLITOA TAMKO LA MAAFIKIANO YENU NA HUYO BB.. TENA NYINYI WENYEWE TOENI TAMKO LA KUKANUSHA YALE MLIYO AFIKIANA KABLA HII KITU HAIJA WACOST NYINYI.



TUNAISHUKURU KAMATI YA BUNGE, MH TINDU NA MH NCHIMBI KWA KAZI KUBWA MLIYOIFANYA KUWAPATANISHA HAWA JAMAA ILI HATA KWENYE TARATIBU ZA KUTAFUTA VAZI LA TAIFA WAFANYE KAZI PAMOJA KAMA ILIVYOKUWA INATAKIWA ILA, ILA INGEKUWA VIZURI ZAIDI KAMA MNGETUSHIRIKISHA WOTE WENYE VILIO JUU YA WAFU NA VIRUS WALIYOKO MEDIA HOUSES NYINGINE. AU LA, INGEKUWA POA ZAIDI MKATUMIA MUDA KAMA HUO MLIO UTUMIA, MMBADILISHE SYSTEM NZIMA YA SHERIA YA HAKI MILIKI. NA SISI MADAI YETU JUU YA SANAA SIO STUDIO TU, WALA SIO VYAMA TU, NI MAMBO MENGI TENA YA MSINGI IKIWEMO SHERIA YA HAKI MILIKI AMBAYO BADO MBOVU NA NDIO INAYOTUANGAMIZA…. TUNASHUKURU ILA SISI HARAKATI ZETU HAZIJAFIKIWA MAAFIKIANO NA HII ISSUE ISIGEUZWE KISIASA HUYO VIRUS AJIUZULU KAMA ALIVYO JIUZULU MH LOWASSA…G-SOLO
TOT TAARAB & MASHAUZI CLASIC BAND WAZINDUA USIKU WA TAARAB DAR LIVE



Malkia wa mipasho Bongo, Khadija Omar Kopa, akitumbuiza kwenye uzinduzi huo.

BENDI za muziki wa mwambao Bongo, Tanzania One Theater Taarab ‘TOT TAARAB’ na Mashauzi Clasic Band, usiku wa kuamkia leo kwapamoja zimezindua tamasha la usiku wa Taarabu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakheem jijini Dar es Salaam, ambalo litakuwa likifanyika ukumbini hapo kila siku ya jumatano.



Baadhi ya waimbaji wa TOT Taarab wakiwa katika viti tayari kwa kutimiza jukum lao.



Kiongozi wa Mashauzi Clasic Band Isha Ramadhani, akitumbuiza kwenye uzinduzi huo.

Waimbaji wa mashauzi Clasic Band wakiwajibika jukwaani hapo.

Wacheza Kiduku wa Mashauzi Clasic Band wakikamua jukwaani hapo.





Baadhi ya mashabiki waliohudhulia katika uzinduzi huo wakiselebuka kwa raha zao.

Wednesday, February 22, 2012

KAULI YA SUGU MUDA MFUPI  BAADA YA SULUHISHO KATI  YAKE NA RUGE


Mh. Josephu Mbilinyi 'Sugu' katika pozi...



Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Josephu Mbilinyi 'Sugu' (kushoto), akiwa kwenye kikao cha usuluhisho na Mkurugenzi mwandamizi wa Clouds Media, Rugemalila Mtahaba, kilichofanyika jana.


KWANZA  poleni na samahanini kwa hali ya sintofahamu iliyotokea leo kutokana na taarifa za ghafla za usuluhishi kati yetu na Ruge/Clouds FM, ni kutokana na unyeti wa issue yenyewe ilibidi tufanye hivyo kwa nia njema kabisa...

Kwanza naomba tujipongeze kwa kuwa tukio la leo ni ushindi kwa Vinega kwa maana kwamba madai yetu yote ya msingi ndiyo yalikuwa msingi wa majadiliano na Ruge amekubali kuyatekeleza yote...

Kuanzia suala la studio ya rais kurudishwa kwa Basata ili iwe ya wasanii wote, pia T.F.U ijikabidhi kwa chama halali cha wasanii yaani T.U.M.A kama ambavyo tulikuwa tunadai na mpaka issue za wasanii kunyanyaswa na kubaniwa na pia suala la malipo hafifu vyote vimejadiliwa na kukubaliwa kwa utekelezaji...

Haikuwa kazi rahisi, kwanza ilianza kwa wao kumpigia Mwenyekiti wangu (wa Chadema) Mbowe kutaka tukae chini, ambapo Kamanda Mbowe alinishauri tukae nao chini kama kweli wana nia ya kuyamaliza...



Baadaye wakampigia Mr .Shigongo ambaye ni wazi kuwa ni kati ya watu wangu wa karibu naye baada ya kuongea na Mr. Kusaga tu alinipigia na kunishauri hivyo hivyo...na kama haikutosha wakalifikisha hili suala kwenye kamati ya bunge ambayo ilinitaka niipe maelezo ya kiini cha mgogoro na nikafanya hivyo ambapo pia baada ya kunielewa wakashauri nikae nao chini...na hatimaye suala hili likaishia mikononi mwa Waziri Nchimbi pamoja na Mhe. Tundu Lissu(Mb) kuwa wapatanishi wetu...

Waziri Nchimbi akaanza kwa kumuita Ruge Dodoma na alikuja tukakaa kwa hatua ya kwanza na hatimaye leo tukakaa tena makao makuu ya wizara ya utamaduni chini ya Dr. Nchimbi na Mhe Tundu Lissu na hatimaye tukafikia hatua hii ya leo...

Vita yetu ilikuwa na hoja hatukuwa tunapigana tu kwa chuki binafsi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanajaribu kuiweka, kwahiyo kama hoja zetu zimeeleweka kwa sasa tunatakiwa kushukuru na kufurahia...lakini naomba niwahakikishie misimamo iko pale pale na nimewaweka wazi kuwa Anti-Virus itaendelea kuwepo ili kuendelea ku-scan virus wengine kama mameneja masoko na wengine watakaojitokeza kwani nchi inaposhinda vita au hata kufikia tu makubaliano ya amani na nchi adui yake haina maana nchi hiyo inavunja jeshi lake... Asanteni sana...
PEDESHEE WEMA ATUA  BONGO BAADA YA KUFANYA  SHOPPING YA MILIONI 45 DUBAI

 Wema Sepetu akiwa kwenye pozi siku chache alipokuwa ameenda kufanya shopping  Dubai

Msanii machachali ndani ya chimbo la filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu 'Pedeshee Wema,' ambaye pia ni miss Tanzania 2006/007, mapema jana alitua nchini akitokea katika falme za kiarabu mjini Dubai alikoenda kwaajili ya mapumziko ya siku ya wapendanao 'Valentine Day' na kufanikisha mahemezi ya mavazi yake ya kila siku na vitu vingine vidogo vidogo vya familia yake.
Wema anadai kuteketeza zaidi ya milioni 41, katika shopping hiyo na sasa amelejea kujenga heshi yake kama ilivyo ada.
Gazeti la risasi lilibahatika kupata baadhi ya vifaa na ngu alizonunua akiwa huko Dubai, so kwa picha na habari zaidi tembelea mtandao wa www.globalpublishers.info

 
Wema Sepetu wa enzi hizo...


SHOPPING YA GHARIMU ZAIDI YA SHILINGI MIL. 45
Habari zilizosambaa kwenye mitandao mingi ya burudani na kijamii ndani na nje ya Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, zilisema kuwa Wema siyo wa bei ndogo tena baada ya kumwaga mamilioni ya fedha kwa ajili ya shopping iliyodaiwa kugharimu dola za Kimarekani 40,000 (zaidi ya Sh. milioni 45 za madafu).
AFIKIA HOTELI YA NYOTA TANO
Katika habari hiyo, Wema aliyefikia katika hoteli ya nyota tano ya DXB mjini humo, alipiga picha akiwa kwenye moja ya maduka ya kistaa akinunua bidhaa za bei mbaya zikiwemo pafyumu, dhahabu, viatu na mazagazaga mengine.
MSHANGAO
“Inavyoonekana mwanadafada Wema siku hizi baada ya kuachana na Almasi (msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’), amekuwa akijiachia na kufanya matanuzi ambayo duh! Amekuwa mtu wa shopping hapa home na sasa yuko zake Dubai kwa ajili ya shopping na matembezi kidogo,” ilisomeka sehemu ya habari hiyo ikiambatanishwa na picha.

MASWALI TATA
“Najaribu kutafakari ni kazi gani anayofanya Wema siku hizi ambayo imekuwa ikimlipa hadi anafuja fedha kiasi hiki? Maana zile pesa ni zaidi ya milioni 45, tena ni kama milioni sitini na pesa hivi...ni hela nyingi sana! Je, ni filamu tu au kuna kingine?” alihoji mmoja wa watu aliyesoma habari hiyo ambapo maswali ya sampuli hiyo yalikuwa mengi.

WEMA PEDESHEE?
Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ulibaini kuwa, mbali na gari la Sh. milioni 35, aina ya Toyota Lexus Hybrid Harrier analosukuma mnyange huyo baada ya kusota na teksi kwa muda mrefu, pia amekuwa akituza wanamuziki wanapokuwa stejini katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar es Salaam.
Katika utetezi wake, Wema aliliambia gazeti pacha na hili, Risasi Jumamosi kuwa, gari analoendesha alinunuliwa na familia yake kama zawadi baada ya kuachana na Diamond.
Achilia mbali gari na shopping za kufuru, pia Wema anaishi kwenye nyumba ya kifahari aliyopangisha maeneo ya Makumbusho Mwanayamala jijini Dar es Salaam.

Tuesday, February 21, 2012

 MAKAMU WA RAIS WA AIRTEL AFRIKA ATUA BONGO

Toka kushoto ni Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika kitengo maalum cha mawasiliano Michael Okwiri akipokelewa na Bi. Joyce Luhanga Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP (kati) mara baada ya kuingia katika ofisi kuu za IPP Mikocheni jijini Dar leo. Mwishoni ni kiongozi wa vipindi Radio One na Mtangazaji wa ITV, Bw. Isack Gamba akiwaongoza pia.
Bw, Isack Gamba ambae ni kiongozi wa vipindi Radio One na Mtangazaji wa ITV akiwaelezea jinsi wanavyofanya vipindi na kushirikisha wasilizaji live katika studio za Radio One Sterio Mikocheni jijini Dar.
Bw Wens Mushi ambae ni Kaimu Naibu Mhariri wa The Guardian akitoa maelekezo kwa Makamu wa raisi wa Airtel Afrika kitengo cha mawasiliano (alieshikilia gazeti) huku Bw Alexander Doll Mkurugenzi mkuu wa Hill+Knowlton Strategies (w apili toka kushoto) toka kampuni maalum ya Mahusiano ya Airtel Afrika akifuatilia kwa undani zaidi. Anaefuata ni Mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe Bw Jesse Kwayu pamoja na wadau wa Airtel nchini Tanzania.
Kulia ni Nasa Kingu Mkuu wa Vipindi wa East Afrika TV/ Radio akiwapokea na kutoa maelezo jinsi wanavyofanya shughuli za habari katika ofisi za East afrika TV/Radio.
------
• Apongeza juhudi za wanahabari nchini Tanzania
• Ahaidi Airtel itakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wanahabari katika mawasiliano

Makamu wa raisi wa Airtel Afrika katika kitengo maalum cha mawasiliano kwa umma leo amepongeza juhudi za wanahabari nchini mara baada ya kutembelea baadhi ya vyombo vya habari Tanzania ikiwemo IPP media na Mwananchi Communication ikiwa ni ziara ya siku mbili aliyojiwekea ili kujionea mambo mbalimbali katika ulimwengu wa Habari na Mawasiliano nchini.
Akiongea wakati wa ziara hiyo akiwa na wadau mbalimbali na wanahabari, Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika bw, Michael Okwiri alisema “Nimegundua Tanzania kunamaendeleo mazuri sana hasa ukiangali mitambo na vyombo vya habari kwa kweli vinaonyesha kupiga hatua kwa kiwango” Vile vile nawapongeza sana wanahabari (Journalists) kwa juhudi zenu za kutafuta habari na kuziwahisha kuzichapa kwa muda wa siku pamoja na mambo mengi, kwa kweli ni juhudi inayohitajika kukamilisha mambo haya mapema ili wasomaji wapate taarifa inayoendana na muda. Kwa upande wetu Airtel naomba niwashukuru wanahabari wote kwa ujumla nchini Tanzania hasa mnaoshirikiana nasi Airtel kuhakikisha huduma ya mawasiliano ya uhakika inawafikia wananchi kwa kupitia baadhi ya habari zinazochapwa na kusambazwa nchini na vyombo vyenu. Airtel tunaahidi ushirikiano wa kutosha katika mawasiliano ili tuweze kutimiza dhamira yetu ya Uhuru wa kuongea nchini kote” alimaliza kwa kusezema bw Okwiri.

 DKT BILAL AKABIDHIWA UCHIFU WA KABILA LA KIKONONGO

Makamu Wa Rais wa Jamhuti ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Mtemi na Chief Mkuu wa Kijiji cha Inyonga, George Mbaula (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Machief wa Inyonga, baada ya kumvisha nguo za asili ya Kabila la Kikonongo na kumkabidhi mikoba ya kuwa Chief wa Kabila hilo, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana.



Makamu a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Inyonga Mkoa wa Katavi wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa katavi jana.



Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Inyonga, baada ya kumaliza kuwahutubia katika mkutano wa hadhara akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi jana.



Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...