Tuesday, July 31, 2012

DEWJI AZIPATIA USHAURI TIMU ZA SIMBA, YANGA




MWANACHAMA maarufu wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Azim Dewji amezishauri klabu kubwa za Simba na Yanga nchini kuanza kuutumia mtaji wa wanachama wake kujijenga kiuchumi, na kuepuka kuwa tegemezi.
Dewji, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashatra maarufu nchini, alisema kwamba kila klabu ina zaidi ya wafuasi milioni 15 nchi nzima, lakini ajabu klabu zinaendelea kuwa ombaomba.
“Huu ni mtaji mkubwa sana, lakini utashangaa klabu haina hata asilimia moja (150,000) ya wanachama wa kweli. Kila siku utasikia wanachama 3,000 hadi 6,000. Kiongozi wa klabu anachaguliwa na wanachama wasiofika 2,000?
“Jamani, kwa klabu inayoshabikiwa na mamilioni ya watu inashindwaje kujijenga kiuchumi kwa kuwatumia mashabiki wake waliozagaa kila kona ya nchi? Jiulize, kama angalau hao watu 150,000 tu wakilipa ada ya mwaka ya 12,000 ambayo hata hivyo bado ni ndogo, si wanaweza kuvuna sh
bilioni 1.8 kwa mwaka, hizi si fedha nyingi?
“Kuna haja ya kufanya mapinduzi ya kweli, badala ya kufikiria kuifunga Simba au Yanga na kutwaa ubingwa wa Bara. Timu yenye uchumi imara, ndiyo inayokuwa na jeuri ya kuwa na kikosi imara na hivyo kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Huko ndiko tunakopaswa kwenda,” alisisitiza.
Aidha, Dewji ameipongeza Yanga kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mwishoni mwa wiki, baada ya kuizamisha Azam kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa fainali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Dewji, aliyewahi kuifadhili Simba na kuifikisha fainali za Kombe la CAF mwaka 1993, alisema pamoja na yeye kuwa `Simba Damu’, ana kila sababu za kuimwagia sifa Yanga kwa kuwa imezika haraka matatizo yake na kugeukia kusaka maendeleo.
“Huwezi kuamini kama Yanga iliyopigwa 5-0 na kuibua tafrani nzito Jangwani, ndiyo hii ya leo. Wameikubali hali na kubadilika ndani ya muda mfupi sana. Wana amani na matunda yake yameonekana ingawa walikuwa na kipindi kifupi cha kusuka timu na kurejesha mshikamano ndani ya klabu.
“Naipongeza Yanga na hasa Mwenyekiti wake, Yussuf Manji kwa sababu naamini imani ya wanachama juu yake ndiyo iliyorekebisha hali haraka, naye kama kiongozi kuhakikisha usajili makini unafanyika, kocha anapatikana na uzalendo ndani ya Yanga unarejea,” alisema Dewji.
Aliongeza kuwa, pamoja na matunda ya haraka ya uongozi wa Manji, wana-Yanga wanapaswa kumpa ushirikiano ili kuiondoa Yanga katika utegemezi wa miaka nenda rudi, huku akisisitiza Manji hatabaki Yanga milele.
“Wana kiongozi shupavu, sasa washirikiane naye kuujenga uchumi wa klabu. Haya mambo ya kutegemea mtu kila kukicha si mazuri. Na hili si kwa Yanga tu, hata Simba na klabu nyingine zinapaswa kujikita katika kujijenga kiuchumi ili ziwe na jeuri ya fedha bila ya kutegemea mifuko ya mwanachama mmoja mmoja,” alisema.

MENEJA WA KINYWAJI CHA GRAND MALT WAKIKABIDHI RAMBIRAMBI KWA MAKAMU WA RAIS WA ZANZIBAR



Meneja masoko wa Kinywaji cha Grandmalt Fimbo Buttalah Kulia akimkabidhi makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy Hundi ya Shilingi milioni tano kama sehemu ya Rambirambi zilizotolewa kwa pamoja kati ya Grandmalt ambao ni wadhamini wa Ligi kuu ya Zanzibar na Chama cha Soko Zanzibar ZFA. Kushoto ni Makau wa rais wa Zfa Kassum Suleman

Meneja masoko wa Kinywaji cha Grandmalt Fimbo Buttalah Kulia akimkabidhi makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy Fedha Shilingi milioni tano kama sehemu ya Rambirambi zilizotolewa kwa pamoja kati ya Grandmalt ambao ni wadhamini wa Ligi kuu ya Zanzibar na Chama cha Soko Zanzibar ZFA. Kushoto ni Makau wa rais wa Zfa Kassum Suleman



makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akizungumza katika hafla fupi ofisini kwake wakatiti akipokea fedha taslimu shilingi milioni tano toka Grandmalt na ZFA Kwaajili ya kuwafariji wale wote waliopatwa na maafa ya ajali ya meli hivi karibuni

MABALOZI WA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSTELI ZA SEKONDARI ZA WASICHANA, WAZINDUA KAMPENI IITWAYO ELIMU YAO WAJIBU WETU




Miss Tanzania 2005 Nancy Sumari akielezea jinsi alivyoguswa na kuamua kujitoa kusaidia kampeni hii ya TEA inayokusudiwa kuchangisha jumla ya shilingi bilioni 2.3

Mtangazaji wa kipindi cha FEMA, Rebeca Gyumi ambaye pia ndiye mratibu mkuu wa mabalozi hao akielezea jinsi walivyojipanga kuhakikisha wanachangisha fedha za kutosha.



Jokate Mwegelo (kulia) akielezea imani yake kwa watanzania na kuwaomba raia wanaoiombea mema nchi yetu kuguswa kama walivyoguswa wao kujituma katika kuchangia kampeni hii ambapo ujumbe mmoja wa CHANGIA TOFALI ni shilingi 250/=, Kushoto kwake ni Mwanablog maarufu na mwanamitindo Mariam Ndaba



Waandishi wa habari waliofika kuhudhuria uzinduzi wa ‘Elimu yao, Wajibu wetu” kampeni iliyoandaliwa na mabalozi waliojitolea kwa hiari kuhakikisha fedha hizo zinapatikana. Kiasi chote kitakachopatikana katika kampeni hiyo kitaingizwa katika mradi huu.
PICHA: 8020FASHIONS BLOG

TFF WAANIKA MAPATO YA MECHI YA NGORONGORO HEROES NA NIGERIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MECHI YA NGORONGORO HEROES YAINGIZA MIL 12/-
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria (Flying Eagles) iliyochezwa juzi (Julai 29 mwaka huu) imeingiza sh. 12,901,000.
Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 3,377 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sehemu iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani ambapo 2,697 walikata tiketi kwa kiingilio cha sh. 3,000 kila mmoja. Viingilio vingine katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 15,000 kwa VIP A iliyoingiza watazamaji 21.
Mgawanyo wa mapato hayo ni kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ilikuwa sh. 1,967,949.15, gharama ya kuchapa tiketi sh. 2,250,000, gharama za waamuzi na kamishna wa mechi hiyo sh. 760,000 na ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000.
Malipo kwa Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000, asilimia 20 ya gharama za mchezo ni sh. 714,610.17, asilimia 10 ya uwanja sh. 357,305.08, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 178,652.54 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,322,483.05.
Mechi ya marudiano ya michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Agosti 12 mwaka mjini Ilorin, Jimbo la Kwara, Nigeria.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA SIREFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (DOREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Julai 28 mwaka huu.
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Singida.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SIREFA chini ya uenyekiti wa Baltazar Kimario ambaye amechaguliwa kwa mara ya kwanza.
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Singida kwa kuzingatia katiba ya SIREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SIREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Singida ni Baltazar Kimario (Mwenyekiti), Hussein Mwamba (Katibu Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Gabriel Mwanga (Mhazini), Hamisi Kitila (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Salum (Mwakilishi wa Klabu TFF), Yagi Kiaratu na Dafi Dafi (wajumbe wa Kamati ya Utendaji).
Nafasi za Makamu Mwenyekiti, Mhazini Msaidizi na wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji zitajazwa katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye.
MICHELSEN AITA 22 KAMBI YA COCA-COLA
Kocha wa timu za Taifa za vijana za Tanzania, Jakob Michelsen ameita wachezaji 22 kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Coca-Cola itakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Baadaye watachujwa na kubaki 16 ambao ndiyo watakaokwenda kwenye michuano ya Afrika Kusini. Wachezaji waliochaguliwa wametokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani kuanzia Juni 24- Julai 2 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni Abdulrahman Mandawanga (Dodoma), Abraham Mohamed (Mjini Magharibi), Ayoub Alfan (Dodoma), Bakari Masoud (Tanga), Daniel Justin (Dodoma), Denis Dionis (Ilala), Edward Songo (Ruvuma), Fikiri Bakari (Tanga), Hassan Kabunda (Temeke), Joseph Chidyalo (Dodoma), Mutalemwa Katunzi (Morogoro) na Mwarami Maundu (Lindi).
Wengine ni Nankoveka Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Omari Saleh (Singida), Rajab Rajab (Mwanza), Said Said (Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman (Kigoma), Tumaini Baraka (Kilimanjaro) na William John (Ruvuma).
Pia Michelsen ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi cha Serengeti Boys ambacho Septemba mwaka huu kitacheza na Kenya kuwania tiketi ya fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi hicho ambao pia wametoka kwenye Copa Coca-Cola ni Abdallah Baker (Mjini Magharibi), Abdallah Kheri (Mjini Magharibi), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Hassan Mganga (Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni) na Mzamiru Said (Morogoro).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

NAPE AJIBU MAPIGO KWA LISU


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.
"Mfano mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni mbunge wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;
"Cha kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema, yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".
Nape alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.
"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.
Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.
"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.
Nape alisema CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.
"Tunaamini uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada zao", alisema Nape.
Alisema, pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.
"Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.

SAKATA LA WABUNGE KUHUSISHWA NA RUSHWA, ZITTO KABWE NAYE ABANWA


KUFUATIA lile sakata  la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.
Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.


Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.
Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.


“Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Tweeter.


Lissu ataja wengine
Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.



Monday, July 30, 2012

VODACOM YATOA TUZO KWA WAMILIKI WA BLOG


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa, akizungumza jambo muda mfupi kabla ya zoezi la utoaji tuzo kuanza.
 
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, mapema leo imetoa tuzo kwa baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa, alisema tuzo hizo ni mpango wa kampuni hiyo kutambua, kuendeleza na kuongeza jitihada na maudhui katika mitandao ya kijamii na tovuti, na kuthamini mchango wa waandishi katika utoaji wa taarifa kwa jamii.
Washindi 10 katika kipengele cha mitandao ya jamii na tovuti ni wafuatao:
1: Elsie Eyakuze wa Mikocheni Report
2: Muhidini Michuzi wa Issa Michuzi Blog.
3: John Kitime wa Wanamuziki Tanzania Blog
4: Masoud Kipanya wa Kipanya .co.tz
5: Umoja wa Vijana FM
6: Millard Ayo wa Millardayo.co
7: Miriam Rose Kinunda wa Taste of Tanzania
8: Mike Mushi wa Jamii Forums
9: Rachel Hamada wa Mambo Magazine
10: Fatma Hassan wa DJ Fetty Blog.
Washindi hao wanawawakilisha wengine wengi wanaoonyesha vipaji vyao ambapo pia mchango wao unahitajika kuthaminiwa.

Mmoja wa washindi wa tuzo hizo, Masoud Kipanya (kulia), akipokea zawadi zake kutoka kwa Kelvin Twisa, huku akishuhudiwa na mmoja wa wasimamizi wa zoezi hilo kutoka Vodacom.

DJ Fetty (kulia) akipokea zawadi zake.

John Kitime (kulia) akituzwa.

Baadhi ya wadau na viongozi wa utoaji tuzo hizo wakiwa pamoja baada ya zoezi hilo.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati), akishuhudia zoezi hilo na baadhi ya wageni wengine waliofika mahali hapo.


Baadhi ya waalikwa na wanahabari wakifutilia kwa makini zoezi la utoaji tuzo hizo.






ZANTEL EPIQ BONGO STAR SEACH YANASA 6 TANGA


Washiriki waliokosa nafasi ya kufanya usaili jana wakisuburi kuingia kuwaona majaji ndani ya ukumbi wa La Casa Chica mjini Tanga.
Mshiriki Sarah Mbwambo akitabasamu mara baada ya kutoka kuwaona majaji.
Washiriki kutoka Tanga wakitoa…
Washiriki waliokosa nafasi ya kufanya usaili jana wakisuburi kuingia kuwaona majaji ndani ya ukumbi wa La Casa Chica mjini Tanga. Mshiriki Sarah Mbwambo akitabasamu mara baada ya kutoka kuwaona majaji.Washiriki kutoka Tanga wakitoa alama ya poa muda mfupi kabla ya kuingia kuwaona majaji.Majaji wakimsikiliza mshiriki kwa umakini ndani ya ukumbi wa La Casa Chica Tanga. Washiriki wa mwisho wakifanya usajili tayari kuingia kuwaona majaji.Washiriki wakizidi kufanya usajili.Washiriki wakiwa ndani ya chumba cha usaili wakisubiri zamu yao kuingia.
Haya ndiyo yaliyojiri katika siku ya pili ya usaili wa Zantel Epiq Bong Star Search uliofanyika katika ukumbi wa La Casa Chika jijini Tanga. Majaji wameonekana kufurahishwa na vipaji na kuamua kuchukua watu sita badala ya watano ambao wataenda Dar es Salaam kuiwakilisha Tanga. Zaidi ya washiriki 800 walijitokeza katika usaili wa mjini Tanga. Usaili utaendelea tena tarehe 1 mwezi Agosti katika eneo la Coco Beach Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEMEJI YAKE LINDI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Julai 30, 2012 amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi (45), aliyefariki siku ya jumamosi iliyopita jijini Dar es salaam, na kuzikwa katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.
Rais Kikwete akishiriki katika swala ya kumuombea marehemu mjini Lindi leo.

ECO BANK YATIKISA NA PROMOSHENI YA SHINDA BABU KUBWA



Balozi wa Eco Bank, Joyce Mrema akizungumza na wateja wakati wa promosheni ya Shinda Babu kubwa na EcoBank katika viwanja vya Mlimani City  jijini Dar es Salam.

 

SHINDA  Babkubwa Promo na Ecobank Promo, enhancing personal,
family and business lives..
Shinda Babkubwa na Ecobank promotion is creating lots of excitement in Dar es Salaam. The first set of winners emerged in the June draw and they are right now redeeming their prizes amidst celebration and jubilations. Being one of the most exciting promotions in Dar es Salaam right now, the promotion mechanics is simple and easy to understand. The prizes are functional and intended to add value to a winner’s life, personally, as a family or even as a business owner.

Taji Kaaya a student of Kampala University who won an Ipad said ‘I came back from Kampala to hear I had won a laptop. It put some sunshine into my holiday’. The story of Kelvin Kipenge . who won a laptop was equally touching when he said ‘I have longed to own a brand new laptop to help me get information around the world that I need to do my business’. Another winner, CEO of Federal Trading Company Limited, was excited about giving his wife the opportunity to shop in Mariedo. ‘I will give the voucher to my wife to shop and I will watch her pick those lovely clothes she has been dreaming of’.

While some winners opted to redeem their prizes same day, others said they will take their time, shop around and eventually settle for what they want. Some winners went to Clocktower Shopping Centre while others went to Home Shopping Centre. This is the beauty of the Shinda Babkwuba na Ecobank promo. You have options with your prize and you can redeem it at your convenience.

Mr. Sam Ayim, Executive Director of the Ecobank Tanzania, said …‘Our branches have seen tremendous growth in traffic from June 4th when the promotion started. This is a clear indication that the objectives of the promotion which included fostering a saving culture in Tanzania, is being achieved. Saving is an essential tool in planning for the future. Thanks to Shinda Babkubwa na Ecobank na Ecobank Promo. He further explained.. ‘We have exciting products and services that have been carefully developed to deliver endearing value to our customers’ and encouraged potential customers to visit any of Ecobank branches to avail themselves of more information.

For those who did not win in the first draw, the promotion continues until November, so there is still time to win. Simply open an account with Ecobank and grow your deposit to Tsh 100,000 each month to qualify for a chance to win. Prizes include a brand new Hyundai Tucson grand prize and monthly prizes including Ipads, Laptops, Air Tickets and more. Visit an Ecobank branch today to open your account. Ecobank, The Pan African bank.

MAMBO YA CHAGA DAY LEADERS CLUB

Wadau wakipata pombe aina ya mbege yenye asili ya Kichaga. Wadau wakipata mbege na Chakula wakati wa tamasha la CHAGGA DAY lilofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam Wadau wakipata Mbege Bendi ya msondo ngoma ikitoa burudani wakati wa tamasha la Chagga Day Wacheza shoo wa Bendi ya Twanga Pepeta wakicheza wakati wa Chaga Day. Wadau Wadau wakipata mbege wakati wa tamasha la CHAGGA DAY lilofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam

Thursday, July 26, 2012

WAZIRI WA UCHUKUZI DR HARRISON MWAKYEMBE AZINDUA HUDUMA MPYA ZA SHIRIKA LA NDEGE LA QATAR KUTOKA KIA


Picha ya pamoja mara baada ya Shirika la ndege la serikali ya Qatar (Qatar airways) leo kuzindua huduma ya safari zake za anga kutoka Kilimanjaro kuelekea sehemu mbalimbali za dunia kila siku na kufanya huduma za safari za anga kufikia zaidi miji 118.
 

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar zawadi ya picha yenye kivuli cha Mlima Kilimanjaro .


Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akimpa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison zawadi ya yenye nembo ya ndege ya shirika hilo la Qatar.


Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.

Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.

Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat,Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakijadiliana jambo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh lakizungumza machache na pia kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo mapema leo iliofanyika kwenye uwanja wa KIA.

Wakuu wa uzinduzi wakipga makofi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akipiga makofi wakati kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza,shoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika hilo aina ya Ndege namba QR546,shoto kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimpokea Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe mara baada ya kuwasili KIA tayari kwa uzinduzi

Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe akishuka kwenye ndege ya Qatar kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa ameambatana na Mkewe pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.

Ndege ya Qatar ikiwasili kabla ya kuzinduliwa rasmi KIA.

Ikifanyiwa shower kwa mbwembwe zote.

Wageni waalikwa mbali mbali wakisubiri kushuhudia uzinduzi huo.








Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Mhe.Novatus Makunga akizungumza jambo na Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima,Bw.Absalom Kibanda.



Baadhi ya Wanahabari Waandamizi wakiwa kwenye uzinduzi huo mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...