Saturday, February 28, 2015

AZAM 'HATUNAYO' KLABU BINGWA TENA, TIMU ZA BONGO ZAJENGA UTEJA KWA WASUDAN...KMKM NAYE MHHH!!...

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC, wametupwa nje ya michuano hiyo kwa wastani wa mabao 3-2.
Azam, wamepigwa mabao 3-0 katika mechi ya marudiano iliyomalizika usiku huu mjini Khartoum, Sudan dhidi ya wenyeji wao, Al Merrikh.
Hata hivyo wenyeji wangefunga mabao mengi zaidi kama wasingekosa penalti katika dakika ya 46'.
Mechi ya kwanza uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam, Azam walishinda mabao 2-0.
Katika mechi hiyo, Azam walipoteza nafasi nyingi za kufunga na kama wangekuwa makini wangepata ushindi mkubwa ambao ungewasaidia ugenini.
Al Merrikh walioanza fitina tangu Azam wanatua Khartoum walikuwa bora kwa kila kitu na walitumia vyema nafasi hizo tatu walizopata kati ya nyingi walizotengeneza.
Azam wameshiriki kwa mara ya kwanza ligi ya mabingwa na wametupwa nje asubuhi kabisa na sasa wanarejea kwenye mechi za ligi ambako nako kuna cheche za Yanga.
Kabla ya ligi ya mabingwa, mabingwa hao wa Tanzania waliwekeza pesa nyingi katika maandalizi, waliweka kambi uganda, wakaenda kushiriki kombe la Mapinduzi mwanzoni mwa mwaka huu na wakamalizia kambi nchini Congo DR, lakini mavuno yamekuwa hafifu.
Wakati huo huo, KMKM, wawakilishi wa Zanzibar kwenye ligi ya mabingwa, wametolewa na wapinzani wakubwa wa Merrikh, Al Hilal kwa wastani wa mabao 2-1.
KMKM walishinda 1-0 jioni ya leo uwanja wa Amaan Zanzibar, lakini mechi ya kwanza walipigwa 2-0 nchini Sudan.
Tanzania imebakiwa na timu mbili tu katika mashindano ya kimataifa kwa maana ya Yanga na Polisi FC ya Zanzibar, lakini kama taswira ilivyo, tutabaki na Yanga tu.
Yanga walifuzu raundi ya pili jana usiku kwa wastani wa mabao 3-2.
Walifungwa 2-1 na BDF XI mjini Gaborone, lakini wao walishinda 2-0 Dar es salaam.
Polisi wana uwezekano mkubwa wa kutupwa nje ya mashindano kwani mechi ya kwanza nchini Gabon, walipigwa 5-0 na CF Mounana, wao wanashuka dimbani kesho kusaka mabao 6-0 ili kusonga mbele.


ANGALIA PICHA MBALIMBALI ZA TAARIFA YA KIFO CHA MH. JOHN KOMBA


Picha ya kwanza ya Marehemu komba mara baada ya kufariki dunia.
Marehemu Kapteni Komba.
Picha ya kwanza ya Marehemu komba mara baada ya kufariki dunia.

...Komba enzi za uhai wake.

MBUNGE wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba amefariki dunia jioni hii jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.

Mmoja wa watoto wa Komba ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, huku akilia, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar.

Habari zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini baadaye akajisikia vibaya, hivyo akaamua kurudi nyumbani ambako alizidiwa ndipo familia yake ilipoamua kumkimbiza Hospitali ya TMJ lakini alipopimwa na madaktari ikathibitika kuwa alikuwa tayari ameaga dunia. habari zaidi zinasema kuwa hivi sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Kapteni Komba ambaye pia ni Mkurugugenzi wa Kikundi cha Maigizo cha Tanzania One Theatre (TOT), ambacho kina kikundi cha taarabu na bendi inayokwenda na mtindo wa Achimenengule, amekuwa akikisaidia sana chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni zake wakati wa uchaguzi kwa kutunga nyimbo za kuhamasisha wapiga kura na kushiriki kupiga live kwenye majukwaa ya kisiasa.

...alipokuwa bungeni

Enzi za uhai wake alitamani sana na kufanya juhudi kubwa ili mtindo wa Achimenengule uwe wa kitaifa lakini ikashindikana, na badala yake Watanzania sasa tuna muziki wa Mduara ambao umekuwa kama mtindo wa muziki wetu kwa sababu zifuatazo.

Kwanza, ni mtindo halisi wa Kitanzania uliochipuka kutoka mahadhi ya kimwambao ya Tanzania. Pili, ndiyo mtindo pekee uliowahi kutumiwa na bendi nyingi baada ya kuasisiwa na ‘mabingwa’ wa muziki wetu, wana Njenje, The Kilimanjaro Band.

Baada ya bendi hiyo kuuasisi, mtindo huo, tayari umepigwa na bendi kama TOT Plus, Chuchu Sound, Pamo Sound, Inafrika Band, wana mipasho kadhaa na mwanamuziki mahiri lakini asiyethamini kiwango chake kikubwa cha muziki, Bob Haisa.

Sababu ya tatu ni kwamba mtindo huo umekuwa wa kupigwa na bendi nyingi, vikundi vingi na wanamuziki wengi si kwa kulazimisha bali kwa mapenzi tu ya mashabiki wa muziki wa Tanzania.

Kapteni Komba awali alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuingia jeshini na kuwa kiongozi wa kikundi cha maonesho cha jeshi na baadaye Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akamshawishi aachane na jeshi na kujiunga na CCM wakati wa mfumo wa vyama mingi ulipoingizwa mwaka 1992.

“Mzee Mwinyi ndiye aliyenifanya niache jeshi wakati huo nikiwa na cheo cha ukapteni. Aliniomba nikisaidie chama kwa kuanzisha kikundi ambacho lengo lake lilikuwa kukipigia debe CCM,” aliwahi kusema hivyo Kapteni Komba.

Ameshiriki kampenzi za marais Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na aliye madarakani hivi sasa, Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi hadi kifo kinamchukua.

Licha ya siasa Kapteni Komba alikuwa anamiliki shule na pia alikuwa na biashara kadhaa.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.

Baada ya kurejea nchini alisema upasuaji huo ulichukua saa tano na ulifanyika katika Hospitali ya Apollo, India na alikanusha kuwa alikuwa na ugonjwa wa figo.Ugonjwa uliomuua ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
..marehemu Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake Mbezi tangi Bovu akielezea kuimarika kwa afya yake aliporejea kutoka India kwenye matibabu, Julai 27, 2012.

MALI ZAKE ZATISHIWA KUUZWA

Mapema mwezi uliyopita mwaka huu, mali za Kapteni John Komba zilitangazwa kupigwa mnada kutokana na kushindwa kulipa deni analodaiwa na Benki ya CRDB.


Mali hizo zilihusisha eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,214 lililopo Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam, kiwanja namba 1030 kilichosajiliwa kwa jina la John Damiano Komba na Salome Komba.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari, Kampuni ya Uwakili ya Mpoki & Associates Advocates inayoiwakilisha CRDB ilitangaza kuuza eneo hilo la kibiashara lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, maduka makubwa, benki, sehemu ya kufanyia mazoezi, hospitali na huduma nyingine za kijamii.

SIMBA vs PRISONS, UPDATES FROM TAIFA, LEO JUMAMOSI NOV. 28 MPIRAAAA UMEKWISHAAAAAAA!

Simba inaondoka na ushindi wa mabao 5-0

KIPINDI CHA PILI, 5-0, RED CARD!!

GOOOOAAAAL 5-0
Dakika ya 81, Ramadhan 'Messi' anaifungia bao la tano Simba, shukurani kwa kazi nzuri ya Okwi aliyepiga krosi murua na kumkuta Messi katika nafasi nzuri.
OKWIII
Dk 75, Okwi anaiandikia bao la nne Simba kwa shuti nje ya box linamuacha kipa wa Prisons asijue la kufanya
Simba 4-0 Prisons
MABADILIKO
Simba wanafanya mabadiliko:
Ajibu anatoka nafasi yake inachukuliwa na Awadh Juma, Sserunkuma anatoka, yake inachukuliwa na Twaha Ibrahim  
  
PRISONS WABADILIKA
Prisons wanaonekana kubadilika kimchezo, walau sasa wanafika langoni mwa Simba, lakini hakuna la maana wamefanmya zaidi ya kuonesha ukakamavu wa kupeleka mashambulizi, lakini yote yanaishia kwa mabeki.
Ajibu wa Simba anaoneshwa kadi ya njano pamoja na beki wa Prisons, Chona. 
Chona anaonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
FOWADI YA SIMBA 
Licha ya kuongoza kwa mabao 3-0, lakini bado safu ya ushambuliaji ya Simba haina makali yoyote, Sserunkuma licha ya kuasist bao la kwanza, lakini anaonekana bado ana safari ndefu tena sana kuhimili mikikimikiki ya Kibongo.
 
 HALF TIME...SIMBA IMEISHAMLA MTU KILO TATU!!
Simba imeonekana kurudi kwenye ubora wake, baada ya kuziona nyavu za Wanajelajela wa Prisons kutoka Mbeya mara tatu mpaka sasa kipindi cha kwanza kwa mabao ya yosso hatari kwa sasa, Ibrahim Ajibu Migumba, akitumia vema kazi nzuri zilizofanywa vema na Emmanuel Okwi pamoja na Dan Sserunkuma.

Hadi dakika 45, Simba imeonekana kuutawala mchezo ambapo wapinzani wao wamefika langoni mara moja tu huku wakiwa hawajapia shuti la maana hata moja golini mwa Simba achilia mbali shuti moja lililopaa sentimita kadhaa juu.

Ajibu alianza kuzifumania nyavu mapema dakika ya 18 akimalizia vema kazi iliyofanywa na Waganda, Okwi na Sserunkuma ambapo Okwi alitoka na mpira langoni mwa Simba na kukimbia nao, kisha kumpa Sserunkuma ambaye ‘alim-setia’ Ajibu na kumchambua kipa na kuukwamisha kambani.

Ajibu alirejea tena nyavuni dakika ya 23 akimalizia mpira uliopanguliwa na kipa wa Prisons, Mohamed Yusuf aliyepangua shuti kali la Okwi, kisha Ajibu akafanya maajabu yake.

Simba walipata penalti dakika ya 41, baada ya beki wa Prisons kunawa mpira, penalti iliyopigwa kifundi na fundi Ajibu.
Hadi dakika 45, Simba 3-0 Prisons

Hali ya mashabiki

Katika kile kinachoonekana uongozi wa Simba una kazi kubwa, ni kurudisha morali ya mashabiki, kwani idadi ni ndogo sana, sana, sana ten asana kupita maelezo kwa wale wanaojua udhurio la mashabiki katika mechi za Simba.

VIKOSI

Simba: Ivo Mapunda, Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein Tshabalala, Hasan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhan Singano, Said Ndemla, Dan Sserunkuma, Ibrahim Ajibu na Emmanuel Okwi.

Sub: Peter Manyika, Nassor Masoud, Issa Rashid Abdulaziz Makame, Twaha Ibrahim, Elias Maguri na Awadh Juma

Prisons: Mohamed Yussuf, Lugano Mwangama, Laurian Mpalile, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil/ Mtei, Adam Chimbongwe, Freddy Chudu, Ibrahim Isaka, Boniface Hau na Godfrey Magetha

Sub: Enock Balagashi, John Matei, Jimmy Shoji, Julius Kwanga, Meshack Seleman, Hassan Omar na Amir Omar

NDOA YA TEMBA YAPUMULIA MASHINE

Mh. Temba.


NDOA ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ inadaiwa kupumulia mashine kutokana na madai ya kuwepo kwa usaliti baina yao.

Habari kutoka kwa chanzo kilicho karibu na wanandoa hao wanaoishi wilayani Temeke, kinasema kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya watu hao, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kusaliti, jambo linaloonyesha wakati wowote ndoa yao inaweza kusambaratika.
“Jamaa hayuko ‘peace’ kabisa na ndoa yake, yaani kila siku ni mgogoro, wife wake anamshutumu mshkaji kuwa msaliti kwa wanawake wengine na mke naye anatuhumiwa hivyohivyo ili mradi hakuna amani kabisa. Inaonekana kuna tatizo kubwa,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Gazeti la Risasi Jumamosi halikuweza kuwapata wanandoa hao kutokana na simu zao kutopatikana, lakini wakati linakwenda mitamboni, lilipata taarifa za kufikishwa mahakamani kwa Mheshimiwa Temba, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua, kitendo alichokifanya kwa Godfrey Deogratius anayemtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ akiwa na mke wake siku ya ndoa yao.

HAAA! ETI ZARI WA DIAMOND AKIMBIA BONGO KUKWEPA UCHAWI!!!! ......


ISHU ya uchawi kwa wanawake wajawazito ndilo suala kubwa linaloingia kwenye hisia za baadhi ya watu hasa mimba inapokuwa changa, hofu hiyo sasa imemwingia mwandani wa Mbongo-Fleva anayeuza zaidi kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ ambaye anadaiwa kuikimbia Bongo kwa muda ili mimba yake isije kuchoropoka kama ilivyokuwa kwa akina Wema Sepetu na Penniel Mungilwa ‘Penny’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya Diamond, hivi karibuni Zari aliondoka Bongo mara tu baada ya kurejea kutoka Zanzibar walikokuwa wameenda kula bata katika Msimu wa Valentine.
Chanzo hicho kilidai kwamba, wakati

Friday, February 27, 2015

MPIRAAAAAAA UMEISHAAAAA

Mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho, DBF XI 2-1 Yanga, lakini Yanga wanafuzu kutokana na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa awali uliopigwa Dar es Salaam.

Hata hivyo Yanga wanatakiwa kujilaumu wenyewe kutokana na washambuliaji wake, Tambwe, Msuva na Ngassa kukosa mabao mengi huku wakigongesha mwamba mara tatu




GOOOOOAAAALLLL

DBF wanapata bao la pili dakika ya 85 kwa Madziba kwa kumalizia mpira uliogonga mwamba na kurudi wuanjani, akatumia udhaifu wa mabeki wa Yanga watatu waliokuwa eneo hilo na kukwamisha mpira wavuni.
BDF 2-1 Yanga

Dk 87, Ngassa anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Kpah Sherman.
Dakika 90 zinakamilika. wanaongeza nne

RED CARD NYINGINE!!!!

Dakika ya 73, Yanga nao wanapata pigo kwa Mrwanda kutolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi za njano mbili....

*** KUMRADHI Matukio ya dakika kuanzia 45-68 hatukuyapata kutokana na mawasiliano kutokuwa sawa kutoka Botswana...

Lakini BDF wamesawazisha, 1-1

Dakika ya 70, Yanga wanakosa bao la wazi kwa mara nyingine, Tambwe na Ngassa wote wanashindwa kuweka mpira kimiania








GOOAAAAAAAALLLLLLL

Dakika 29 Mrisho Ngassa anaipatia Yanga bao la kuongoza, akipiga kichwa ya kuchumpa akimalizia pasi ya Amisi Tambwe, ambaye wametokea kushabihiana sana..

Yanga 1-0 BDF....

Jahazi la BDF linazidi kuzama, maana bao hilo linawafanya kusaka mabao manne kama wana nia ya kupenya katika hatua ya kwanza.

RED CARD!!!!!

Dakika ya 19, BDF wanapata pigo la aina yake, kwa mchezaji wao Othusitse Mpharithe, kupigwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya Simon Msuva kwa kuacha mpira na kumkanyaga, lakini anaendelea kucheza

..........................

Danny Mrwanda anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 26

DAKIKA YA TATU, NGASSA ANAKOSA BAO LA WAZI AKIWA PEKE YAKE

Mrisho Ngassa anainyima bao la wazi kabisa Yanga, baada ya kunasa mpira uliomshinda beki wa BDF, akiwa yeye na mlinda mlango, mpira unatoka nje, sentimita chache kutoka golini.

KIKOSI KAZI CHA LEO KILICHOANZA



Ally Mustafa 'Bartez'
Juma Abdul
Oscar Joshua
Nadir Haroub ‘Cannavaro’
Kelvin Yondani
Mbuyu Twite 

Simon Msuva
Mrisho Ngassa
Amissi Tambwe 

Dan Mrwanda
Haruna Niyonzima

TUKO LIVE BILA CHENGA YANGA vs BDF XI KUTOKA LOBATSE, BOTSWANA

NI UKICHAA AU!!?? ANGALIA PICHA WAKIVUNJA AMRI YA SITA KATIKATI YA UWANJA WA TIMU YA CHARLTON

Ni laana sio jingine! Ndivyo unaweza kusema kutokana na tukio la aina yake, wapenzi wawili video yao kunaswa wakivunja amri ya sita katikati ya uwanja wa Klabu ya Charlton Athletic.
Timu hiyo imethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitupiwa mtandaoni juzi Jumatano.
Picha hizo zinawaonyesha wawili hao wakiwa wamegandana katikati ya uwanja huo unafahamika kama Valley.
Mtu mmoja ambaye hakujatwa jina lake, alisema tukio hilo hilo ni la kweli na kitendo hicho kilitokea siku ya Jumanne.
Hata hivyo Charlton, imeijia juu mitandao kuwa ndio imeeneza tukio hilo, ambapo mpaka sasa ziadi ya watu milioni wametazama video hiyo.





Charlton kwa sasa ipo nafasi ya 16 kwenye Championship, pointi nane kutoka katika timu za kushuka daraja.

CANNAVARO, SHERMAN: ZENU DUA WATANZANIA


Hakuna jingine zaidi ya dua za Watanzania kwa ujumla, awe mtu wa Simba au wa Majimaji, kila mmoja anahitajika kuomba kwa moyo mkunjufu, kuiombea Yanga ambayo leo ndio siku pekee ya kujua hatma yake kwenye michuano ya kimataifa, watakaposhuka dimbani kumenyana na wanajeshi wa Botswana, BDF XI.
Mechi hiyo itapigwa leo majira ya saa mbili usiku huko Labtse, mji ulio takribani KM 70 kutoka mji mkuu wa Botswana, Gabrone.
Nahodha na beki tegemeo wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ pamoja na straika Kpah Sherman wamefunguka na kuwaomba Watanzania bila kujali uhamisimu, kuiombea kwani inawalikilisha taifa na haiku kule kama Yanga klabu.
Wakizungumza na blogu hii kwa njia ya mtandao kutoka Botswana, Cannavaro alisema, “Muhimu sala, Watanzania watuombee na sisi hatutawangusha. Cha msingi ni kucheza kwa nidhamu, naamini tutaweza kufanikiwa.
“Uzuri hali ya hewa ya hapa (Botswana), haitofautiani na nyumbani, ila hapa ni baridi kidogo lakini sio kesi kusema kuwa inaweza kutuathiri na tusishwe kucheza. Mungu kwanza jamani,” alisema Cannavaro huku Sherman naye akiongez; “Inshallah tutafuzu, japo mchezo hautakuwa mwepesi.”
Katika mchezo wa leo, Yanga inahitaji sare yoyote ilea ma hat aikifungwa isiruhusu mabao 2-0, kutokana na kujiwekea kibindoni hazina ya mabao 2-0 katika mchezo wa awali uliopigwa wiki mbili zilizopita hapa Bongo. Mabao yote yakifungwa na Amissi Tambwe.

MWANAMITINDO WA KIMATAIFA TAUSI LIKOKOLA ATEMBELEA GLOBAL TV


Mwanamitindo wa kimataifa Mtanzania anayeishi nchini Marekani, Tausi Likokola akijiweka sawa kufanya mahojiano kupitia Global TV Online leo.
...Akifafanua jambo wakati wa mahojiano.
Tausi Likokola akijibu maswali ya wanahabari wa Global Publishers (hawapo pichani).
Akiwa katika pozi baada mahojiano.
Musa Mateja (kulia) akiwa katika pozi na Tausi.

Thursday, February 26, 2015

QUEEN SUZY HATIMAYE AJIFUNGUA


MWANAMUZIKI wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ hivi karibuni amejifungua mtoto wa kike na ameeleza kuwa, amefarajika kwani alikaa muda mrefu tangu alipopata wa kwanza wa kiume.
Mtoto wa , Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ akiwa na babaake.
Mwanadada huyo alijaaliwa kupata mtoto huyo baada ya kuuficha ujauzito wake kwani alikuwa akikaa ndani tu mpaka alipojifungua.

NISAMEHE: HAKYANANI, NENO HILI LITAMWINGIZA LOWASSA IKULU

KIPYENGA! Mpambano wa kuteuliwa na hatimaye kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu kuwania urais unazidi kushamiri huku jina la waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ‘EL’ likiongoza kutajwa midomoni mwa Watanzania.
Imebainika kuwa pamoja na  kelele nyingi zinazosikika mitaani za “Lowassa! Lowassa!” bado hazitoshi kumwingiza madarakani, kama Rais Kikwete hatamwona anafaa kuwa mrithi wake.
Lowassa alikuwa mmoja wa wanamtandao waliofanikisha kuingia ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ katika uchaguzi wa mwaka 2005. Baada ya JK kuingia ikulu,  Lowassa aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya nne hadi alipojiuzulu, Februari 2008 kufuatia tuhuma za kashfa ya mkataba tata wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond.

SKENDO! LULU, WOLPER WAONESHANA JEURI YA MABWANA!

Stori: Musa Mateja/Ijumaa
Sakata la kupangishiwa nyumba za kifahari na wanaume linazidi kuchukua sura mpya kwa mastaa wa kike ndani ya tasnia ya sinema za Kibongo ambapo safari hii mastaa wawili, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper ‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja ambao awali walikuwa juu wakipotezwa.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
TAMBO ZA NANI ZAIDI?
Uchunguzi wa Ijumaa umebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko wengine.

ANGALIA PICHA ZA BERTHDAY YA RECHO WA THT

Keki ya sherehe ilivyokuwa.
 MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Winifrida Josephat ‘Recho’, usiku wa kuamkia leo alifanya  sherehe ya kuzaliwa kwake na baadhi ya jamaa na marafiki aliowaalika katika Hoteli ya Regence Mikocheni jijini Dar ees Salaam.
Linah akiwasha mshumaa kama ishara ya upendo kwa shoga’ake. Mzazi mwenzake na mwanamuziki Barnaba aitwaye Mama Steve (kulia) akilishwa keki na Recho. Mtangazaji wa kituo cha EFM, Ssebo (kulia), akilishwa keki.Staa wa Bongo Fleva, Winifrida Josephat ‘Recho’, akilishana keki na Estelinah Sanga ‘Linah’, usiku wa kuamkia leo ndani ya Regence Hoteli Mikocheni jijini Dar, katika sherehe za bethidei yake. Mmoja wa marafiki zake Recho akimtunza fedha. Recho akiwa na wenzake baada ya ufunguzi wa shampeni kufanyika kwa usahihi.  
Recho katika pozi.


CHID BENZ JELA MIAKA SITA, AKUBALI KULIPA FAINI YA LAKI TISA


Chid Benz (mwenye shati jeupe) baada ya kuachiwa na mahakama.
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Rashidi Makwilo maarufu kama ‘Chid Benz’, aliyekuwa anatuhumiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin na bangi, leo ameachiliwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 900,000.

Katika maelezo ya awali yaliyosomwa na mwendesha mashtaki wa Jamhuri Diana Lukendo, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, msanii huyo alimwambia hakimu kuwa mshtakiwa alikamatwa na dawa hizo za kulevya akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, akitaka kusafiri kuelekea mkoani Mbeya.

Hata hivyo mshtakiwa huyo ambaye alikiri kosa mnano tarehe 18 Aprili mwaka huu, leo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba asingetumia tena ulevi huo na atawaelimisha vijana wenzake juu ya madhara yake.
…Akiondoka mahakamani.
…Akielekea kwenye gari lililomleta.

Wednesday, February 25, 2015

NDOA YA SLIM YAVUNJWA MAHAKAMANI

NDOA ya staa wa filamu nchini, Salim Mbegu ‘Slim’ na mkewe Asia Morgan imevunjwa rasmi na Mahakama ya Mwanzo ya Magomeni jijini Dar kufuatia mgogoro wa muda mrefu.
Aliyekuwa mke wa staa wa filamu nchini, Salim Mbegu ‘Slim’, Asia Morgan akiwa katika pozi.
“Mahakama hii imevunja baada ya mdai (mke) kusema hata iweje hawezi kurudi tena kwa mumewe huyo kutokana na kuwa na wivu wa kupindukia na kingine kibaya walivyokuwa kwenye mgogoro kuna mwanamke alikuwa akijinadi  kwa kupiga picha nyumbani kwa mumewe na kuzituma kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram,” alisema Hakimu Mwanaidi Madeni wa mahakama hiyo.
Hakimu aliamuru watalaka hao kugawana mali zote walizochuma pamoja likiwemo gari walilozawadiwa wakati wa harusi yao, ambalo ndilo lilikuwa chanzo cha mgogoro huo.Wakati mume akisema anaiheshimu hukumu hiyo ingawa anaona kama ni filamu, mke alionyesha furaha yake na kudai sasa ataishi kwa amani.

WASTARA AZIMIA KISA MAPENZI

DIVA wa filamu nchini, Wastara Juma ambaye kwa sasa anaripotiwa kuwa katika mapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Bin Suleiman anadaiwa kupoteza fahamu mara tu baada ya kupewa taarifa kuwa mpenziwe huyo amepata mtoto wa nne kwa mwanamke mwingine, Risasi Mchanganyiko linakupa stori kamili.
DIVA wa filamu nchini, Wastara Juma akiwa hospitali baada ya kuzimia.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara alipenyezewa ubuyu na mpenzi wa zamani wa Bond, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na kuambiwa kwamba asijishebedue kwani Bond ana mwanamke mwingine ambaye amejifungua mtoto wa nne hivi karibuni.

EXCLUSIVE: MALICK BANDAWE AFUNGUKA KUHUSU MAPENZI YAKE NA ROZI NDAUKA

Tuesday, February 24, 2015

BARCA YAINYOA MAN CITY UEFA, JUVE YAWAFUNGA MIDOMO WAJERUMANI

Kiulainiiiiii...Suarez akumbushia mavituzi yake enzi akiwa na Liver, awalaza na mawazo Man City. Kulia picha ya chini Messi akificha uso baada ya penalti yake kupanguliwa.
 Wazee kwa 'tik-taka game', Barcelona wamezidi kudhihirisha ubora wao, baada ya kuifumua Manchester City tena nyumbani kwake, Etihad kwa jumla ya mabao 2-1, idadi sawa na kicheko cha KIbibi Kizee cha Turin, Juventus waliowafundisha soka Wajerumani wa Borussia Dortmund katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’.
Luis Suarez ndiye aliibeba Barca katika mchezo wa leo, kwa kufunga mabao yote, kwa kujitengenezea mwenyewe moja na nyingi akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na staa, Lionel Messi, yote akiyafunga kipindi cha kwanza.
Vijana wa Man City walionekana kuzidiwa soka kipindi cha kwanza, huku pengo la Yaya Toure likionekana wazi ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, hata hivyo walibadilika kipindi cha pili hasa baada ya kuigia kwa Fenandinho aliyechukua nafasi ya Samri Nasri.
Mabadiliko hayo yliipa nguvu City na kuanza kulisakama lango la Barca, tofauti na kipindi cha kwanza na kufuanikiwa kupata bao kupitia kwa Sergio Aguero.
Messi aliinyima bao la usiku timu yake, baada ya mkwaju wake wa penalti dakika ya mwisho kabisa, kupanguliwa na kipa wa Man City, Joel Hart kabla ya Messi kuunganisha tena mpira kwa kichwa, lakini ukatoka nje.
Kichapo hicho kinaiweka pabaya Ciy kwani inahitaji ushindi wa lazima ugenini katika mchezo wa marejeano kule Nou Camp, lakini habari mbaya ni kumkosa beki wa kushoto, Gael Clichy aliyepigwa kadi nyekundu katika mchezo wa leo, lakini Toure atakuwa anamaliza adhabu yake.

Juve vs Dortmund

Mabao ya Carlos Tevez na Alvaro Morata yaliipa ushindi wa mabao 2-1 Juve mbele ya Dortmund , mchezo uliopigwa Turin, Italia. Mchezo huu ni wa kwanza kwa timu hizo kukutana tangu mwaka 1997, ambapo zilikutana fainali na Dortmund kushinda kwa 3-1 na kuivua ubingwa Juve, lakini leo wamelipiza kisasi hicho.
El Apache..!!! Straika tegemeo wa Juve, Carlos Tevez a.k.a El Apache, kushoto mbele, akikwamisha mpira langoni mwa Dortmund katika michuano ya Uefa.

KOMBE LA DUNIA 2022 SASA KUPIGWA KRISMASI

 Bado fukuto kubwa linazidi kujitokeza kuhusu fainali za Kombe la Dunia ya mwaka 2022, zitakazoandaliwa nchini Qatar na sasa imehamishiwa mwezi Novemba na Desemba, kwa mujibu wa kikosi kazi cha Fifa.
Wakurugenzi wa soka wamekutana huko Doha, Qatar kujadiliana mengi kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa fainali hizo kutokana na hofu ya joto kali nchini humo, ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa wachezaji na mashabiki watakaozifuata timu zao.
Inatajwa kuwa joto nchini Qatar, hukufikia sentgridi (40°C) wakati wa kiangazi, huku miezi ya Novemba na Desemba likishuka hadi 25°C.
Pendekezo lilotolewa leo Jumanne, linatarajiwa kuafikiwa na kamati kuu ya Fifa huko Zurich, kati ya Machi 19 na 20.
Bosi wa kikosi kazi cha Fifa, Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa aliongeza kuwa michuano ya 2022 kuna uwezekano wa kufupishwa kwa siku. Tayari tetesi zinadai kuwa fainali hizo zitafungua dimba Nov. 26 na kutamatishwa Des. 23, siku mbili kabla ya Sikukuu ya Krismasi.
Lakini Fifa tayari imesema kuwa haina mpango wa kufupishwa kwa michuano kutoka timu 32 au mechi 64 kama ilivyo ada ya michuano yenyewe.

            Kwanini Nov-Des?
Tarehe nyingine iliyotajwa kuwezekana kuhamishia ni Mei na Januari-Februari. Fifa imesema idadi kubwa ya mapendekezo yameangukia Nov-Des kwa sababu:
*Jan-Feb, michuano ingeweza kuingilia na michuano ya Olympiki.
* Mwezi Ramadan utaanza Aprili 2, 2022, pia Mwezi Mei kwenda Septemba ni majira ya joto jingi sana
Katibu Mkuu wa Fifa, Mbrazili, Jerome Valcke alisema: "Kulikuwa na mabaya na mazuri kwa kila pendekezo, lakini mwisho wa yote tumeona ni bora iwe Novemba na Desemba." 

KINDA LA MAN U MIAKA 18 LAPIGA BAO LA MITA 40!

 Kinda wa Manchester United, aliye kwenye kiwango kwa sasa, Oliver Rathbone amefunga bao la mwaka, baada ya usiku wa kuamkia leo kupiga bonge la bao, mita 40 na kuipa ushindi Man United ya vijana (U-18) wa mabao 2-1 dhidi ya Derby. Cha kuvutia zaidi ni kwamba bao hilo lilikuwa ni la dakika ya 90.

Kinda huyo anayemudu nafasi ya kiungo, alijiunga na United mwaka 2013, bao lake linafananishwa na lile la kptaini Wayne Rooney ‘Wazza’ alililofinga dhidi ya West Ham mwaka jana. Lakini la Wazza linatajwa kuwa la umbali wa mita 20 zaidi, lakini yanafafana katika 'action'.
Ushindi huo umeipaisha United hadi nafasi ya tatu kwenye ligi ya vijana, inayoongozwa na Middlesbrough.
 
bofya link hapa chini kuangalia 'muwa' huo uliopigwa na dogo.


https://vine.co/v/OQO7innHiT7

LUIS NANI AMWAGA MACHOZI UWANJANI BAADA YA KUFUNGA BAO LA MITA 30..ANGALIA VIDEO

Nani, aliyeinamia chini, akificha uso wenye machozi baada ya kufunga bao kali


Winga wa zamani wa Manchester United, Luis Nani amemwaga machozi uwanjani kwa kuzidiwa na furaha baada ya kufunga bonge la bao, mita 30, wakati timu yake ya Sporting Lisbon ikiichakaza Gil Vicente mabao 2-0 juzi usiku.
Nyota huyo ambaye yupo Lisbon kwa mkopo akitoka Man United, ali-control mpira karibu na eneo la kona kabla ya kuachia fataki kali lililotinga wavuni moja kwa moja. 

Lakini hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyu, na inaonekana ni tabia yake kumwaga chozi, ikikumbukwa aliwahi kumwaga chozi uwanjani  kwenye mchezo baina ya Man United na Livewrpool baada ya Jamie Carragher kumchezea rafu, ilikuwa 2011 na United kulala mabao 3-1 pale Anfield.
Carragher kwa ungwana alimfuata kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kuomba radhi  punde baada ya mchezo kumalizika kabla ya Nani kufunguka kisa cha kulia siku hiyo kwa kusema:
“Nilivyouona mguu wangu kwa mara ya kwanza, nilikuwa msimu wangu ndo basi tena, ndiyo maana nililia sana, siku hiyo.”
Nani kushoto, enzi akiwa Man United akionesha jeraha baada ya kupigwa daruga na Carrager wa Liverpool.

 Angalia video kwa kubofya link hapa chini

http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2964603/Nani-breaks-tears-scoring-Sporting-Lisbon-30-yard-stunner.html#v-4074974010001

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...