MUVI
mpya ya Pishu kutoka Kajala Intertaiment & Baby Black Productions
itakuwa sokoni kesho usikose kujipatia nakala yako kwani ndani yake
utakutana mastaa wakali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja, Hemedy
Phd, Tausi, Senga na wengine kibao.
Kajala akiongea na mtandao huu amewaomba mashabiki wake na wapenzi wa
filamu za Kibongo kutoikosa muvi hiyo itapatikana sehemu zote Tanzania
kuanzia kesho.
Floyd Mayweather (kushoto) na Manny Pacquiao wakipozi na mkanda wa WBC jana wakati wa mkutano na wanahabari.
SIKU mbili tu zimebaki kuelekea mpambano wa kihistoria wa ngumi za
kulipwa utakaowakutanisha mabondia Floyd Mayweather (Money) na Manny
Pacquiao (Pacman) ndani ya Ukumbi wa MGM Grand jijini Las Vegas,
Marekani.
Muonekano wa sasa wa Hoteli ya MGM Grand iliyopo jijini Las Vegas, Marekani.
Mpambano huo umekuwa gumzo kote duniani kwa sababu wapinzani hao
wamekuwa wakitafutana kwa muda mrefu kabla ya kukubali kupanda ulingoni
na kuzichapa Mei 2 mwaka huu ambapo kwa muda wa huku itakuwa alfajiri ya
Mei 3.
Money na Pacman watakomba kiasi cha dola za Kimarekani milioni 300
sawa na zaidi ya shilingi bilioni 589 za Kitanzania na iwapo Mayweather
atashinda pambano hilo ataweka kibindoni dola za Kimarekani milioni 180
sawa na zaidi ya shilingi bilioni 353 za Kitanzania ambayo ni asilimia
60 ya kiasi cha fedha kinachoshindaniwa.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA DONDOO ZA MPAMBANO HUO: MIKWANJA $300 milioni - Kiasi cha mkwanja
uliotengwa kwa ajili ya pambano hilo ambapo asilimia 60 itakwenda kwa
Mayweather huku asilimia 40 ikikombwa na Pacquiao (Pacman) $321.43 - Kiasi alichotumia Mayweather kwa upande wa vyakula wiki kadhaa akijiandaa kwa pambano hilo. $2 - Kiasi cha fedha alizokuwa akilipwa Pacquiao kwa kila pambano wakati wa ukuaji wake huko Ufilipino
Mwanamuziki Diddy na Mark Wahlberg waliowekeana $250,000 kwa ajili ya mpambano huo.
$250,000 - Kiasi kilichowekwa kubashiri mpambano huo kati ya mwanamuziki Diddy na Mark Wahlberg
$600 milioni - Jumla ya kiasi cha fedha atakachokuwa ametengeneza
Mayweather kutokana na ubondia baada ya pambano lake na Pacquiao $150 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia televisheni zitakazokuwa zimefungwa katika hoteli ya MGM £19.95 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia Kituo cha Sky Sports huko Uingereza $99.95 - Gharama ambazo watalipa mashabiki waliopo Amerika kuangalia pambano hilo kupitia HBO au Showtime $74 milioni - Mapato yanayotarajiwa kupatikana kutokana na tiketi zilizopangiwa kiwango kati ya $1,500 na $10,000 $5.6 milioni - Kiasi kilicholipwa na Tecate kudhamini pambano hilo. $10,000 - Malipo atakayolipwa refa wa mpambano huo, Kenny Bayless
Kenyy Bayless akiongoza mpambano kati ya Mayweather (kulia) na Maidana Septemba 2014.
WAPIGANAJI 47 - Idadi ya mapambano ya kimataifa na ushindi ambao ameupata bondia Mayweather 55.3% - Asilimia za ushindi wa Mayweather kwa knockout (KO) 62 - Idadi ya mapambano ya kimataifa aliyopigana Pacquiao 66.6% - Asilimia za ushindi wa Pacquiao kwa knockout (KO) 39 - Wastani wa makonde aliyotupa Mayweather kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa. 66 - Wastani wa makonde aliyotupa Pacquiao kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa. 74 - Jumla ya umri wa mabondia hao (Mayweather ana umri wa miaka 38 huku Pacquiao akiwa na miaka 36) Milioni 5.8 - Idadi ya wafuasi wa Mayweather katika mtandao wa Kijamii wa Twitter; Pacquiao ana wafuasi milioni 1.8
309 - Idadi ya maili ambazo Pacquiao alisafiri kwa basi lake la
kifahari kutoka Los Angeles kwenda Las Vegas kwa ajili ya mpambano huo.
Manny akiwa kwenye basi lake la kifahari wakati akielekea Las Vegas akitokea Los Angeles alipokuwa ameweka kambi.
MPAMBANO 36 - Idadi ya dakika ambazo kila bondia atatumia kwenye ulingo iwapo pambano litachukua muda wote uliopangwa. 5 - Idadi ya miaka tangu pambano hili la kihistoria lianze kujadiliwa kwa undani.
Wafanyakazi wa MGM Grand wakiandaa mabango kwa ajili ya mpambano huo.
UKUMBI 16,500 - Idadi ya viti vya wageni wanaoruhisiwa kuingia katika Ukumbi wa MGM Grand wakati wa pambano hilo 9,000 - Idadi ya watu walioajiriwa katika Ukumbi wa MGM Grand 100,000 - Idadi ya watu wanaotarajiwa kuwepo katika hoteli ya MGM Grand kati ya Ijumaa na Jumamosi 7,000 - Idadi ya vyumba vilivyopo katika hoteli ya MGM Grand
STAA
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' jana ametupia picha hii
mitandaoni akihakiki tiketi kwa ajili ya shoo ya mpenzi wake Zarinah
Hassan 'Zari' ya ZARI ALL WHITE PARTY itakayofanyika Ijumaa ya Mei 1,
mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
Staa huyo aliisindikiza picha hiyo kwa maneno haya: "Sio kwa kiingilio hiki cha kuanzia Elf
50 hadi Milioni 3 eti nikajifanya naleta Uboss ... Mzigo Nausimamia
mwenyeweee!!! Kushoto Manager @salaam_sk katikati nna @juju_utamu huku
@queendarleen4real halaf kwambaaaaaali Mtoto katulia zake Anachat
chat!... HAYA WALE WA ELFU HAMSINI NA WA LAKI KESHO NTAWATAJIA VITUO
ZITAPOPATIKANA TICKET!!! #ZARIALLWHITEPARTY Friday May 1st 2015 Mlimani
City Dar!!" Kwenye shoo hiyo ya Zari, watu mbalimbali
mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo dairekta mkubwa Afrika,
Godfather wa Afrika Kusini na Top Ten ya Washiriki wa Shindano la Big
Brother ‘Hot Shot’ 2014.
Musa Mateja SHAKA! Familia ya ‘President’ wa Kruu ya Wasafi, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ imeamua kuweka kikao kummbana staa huyo aweke wazi
kama ni kweli ana uhakika mimba aliyonayo mjasiriamali Zarinah Hassan
‘Zari’ ni ya kwake au magumashi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Diamond Plutnum akibusu tumbo la mpenzi wake Zari.
TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo, ndugu wa
karibu akiwemo mama, binamu yake Romy Jons, wajomba zake, mameneja na
marafiki wa karibu wa familia, waliamua kuweka kikao hicho usiku hivi
karibuni ili Diamond athibitishe kama kweli kiumbe kinachoripotiwa kuwa
ni cha kwake magazetini ni chake kweli.
Diamond akiwa katika pozi na mpenzi wake Zari.
“Ndugu walichachamaa, walitaka kujua kama kweli mimba inamhusu Diamond au ni magumashi ya kiki za vyombo vya habari. “Kwenye hicho kikao walimualika na Diamond mwenyewe ili aweze
kufunguka kama ana uhakika kweli mimba ni yake,” kilisema chanzo hicho WALITAKA ATOE MSIMAMO “Mbali na kutaka kujua kama mimba ni yake, walitaka pia kujua ana
msimamo gani na Zari maana kila kukicha wanasikia mambo tofauti katika
mitandao na vyombo vya habari,’’ kilisema chanzo hicho. SABABU ZAZIDI KUANIKWA Chanzo hicho kilipobanwa na mwanahabari wetu kuhusiana na sababu
zilizowafanya ndugu wa Diamond watilie shaka mimba hiyo, kilisema ni
kauli ambazo ziliwahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa
‘Penny’ na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga. “Walishitushwa na kauli ambayo aliwahi kuitoa Penny kwamba Diamond
hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini kama hiyo haitoshi,
waliitafakari kauli ya mume wa Zari ambaye alidai Zari hawezi kumzalia
Diamond ndiyo maana wakataka wapate uhakika,” kilisema chanzo hicho.
Msanii wa rnb Ben Pol maetia wino kwenye mkataba wa usimamizi na kampuni ya Panamusiq Ltd. Mkataba huu utasimamia kazi zote za Ben Pol na kufanikisha ndoto zake
za kuwa msanii wa kimataifa. Panamusiq ni kampuni iliyosimamia kazi za
Vanessa Mdee kama ‘Nobody But Me’. ” The new partnership aims at
developing Ben Pol into a sustainable global brand and consolidating his
fame in Tanzania and across Africa. We expect to realize this plan
through the production of great music, highly professional services and
the co-operations with global brands and international music industry
players.”
Diamond
Platinums akiwa na Mpenzi wake Zari mara tu baada ya kuwasili uwanja wa
Ndege wakitokea Zanzibar ambao Diamond Alifanya Show Bab kubwa na
Kuacha Historia katika Maeneo yote ya Zanzibar.Wawili hao wamewasili Dar
tayari kwa Maandalizi ya Mwisho ya Show Kubwa ya Zari Ijulikanayo Kama
White Party Itakayofanyika Mwishoni Mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani
City.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani
Lindi Mh. Abdallah Ulega akipokea mashuka 150 kutoka kwa Rehani
Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii
CHF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa
Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Taifa ya
Afya NHIF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati
ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata
Raymond.
Rehani
Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi
wilaya ni Kilwa. Baadhi ya akina mama wakishindana kukuna nazi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo waliunganiswa katika huduma za CHF.
Imekuwa ikielezwa kuwa wasanii ni kioo cha jamii. Kwa maana hiyo
wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na wale wanaowatazama.
Hata hivyo, maisha wanayoishi baadhi ya wasanii hayaakisi msemo huo. Wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo mbalimbali zinazowafanya wasiwe na vigezo vya kuitwa kioo cha jamii. Miongoni mwa mambo yanayowafanya wakati mwingine wadharaulike ni
kutoa maneno machafu, ‘live’ au kupitia kwenye mitandao ya kijamii. Katika makala haya nitawazungumzia mastaa wanaoongoza kwa kutukana
mitandaoni lakini pia wale ambao wanaongoza kwa kutukanwa katika siku za
hivi karibuni. Wastara Juma Huyu
Wastara amekuwa akiheshimika kwenye jamii kwa muda mrefu na alikuwa ni
miongoni mwa mastaa wa kike ambao wangesimama na kuamua jambo
wangesikilizwa kutokana na jinsi alivyokuwa amejiweka na kuwaaminisha
watu.
Ali Chocky (katikati) akiwa na waimbaji wenzake, Luiza Mbutu (kulia), na Kalala Junior baada ya kutambulishwa.
Wanamuziki
wa ‘Twanga’ wakiongozwa na Kalala Junior (kushoto) wakiwa na begi
ambalo ndani yake alikuwemo mnenguaji Super Nyamwela kama moja ya staili
ya kutambulishwa.
Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakifungua begi hilo tayari kwa utambulisho wa mnenguaji mwenzao, Super Nyamwela.
Dar/Mikoani.
Katika kile kinachoonekana kuendelea kujiimarisha kuelekea Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
vimegawana maeneo mbalimbali nchini vikifanya mikutano ya hadhara na
mafunzo kwa viongozi wake ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa ushindi.
Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF. Chadema
kilianza ziara zake mikoani wiki zilizopita baada ya kuzindua mkakati
wake uitwao ‘Hakuna kulala, Hakuna kula, Mpaka Kieleweke’ nchi nzima
wakati timu ya NCCR-Mageuzi ikiweka kambi mkoani Kigoma kwa kile
ilichokiita kuimarisha majimbo ya kimkakati.
Sanjari na
vyama hivyo, CUF tangu juzi kiliingia katika moja ya ngome zake, mkoani
Mtwara pamoja na mipango mengine ya kiushindi, kinahamasisha wananchi
kujitokeza kujiandikisha kupiga kura.
Jitihada za Ukawa
kuzunguka mikoani zinakuja ikiwa ni majuma kadhaa tangu Chama cha
Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na Katibu Mkuu wake Abdulrahman Kinana
kilipomaliza ziara ya kujiimarisha na kukagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya mwaka 2010.
Pia, ziara hizo ziligongana na zile
za Chama cha ACT - Wazalendo zilizosababisha Chadema na chama hicho
kipya kugongana Butiama.
ACT - Wazalendo kinachoongozwa na
Zitto Kabwe kilihitimisha ziara yake ya kimkakati katika mikoa tisa
inayoonekana kuwa ngome ya CCM, wiki iliyopita wilayani Bariadi,
Shinyanga na kuvuna wanachama zaidi 6,000 katika mikoa hiyo.
NCCR-Mageuzi ipo Kigoma Katibu
Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema jana kuwa Ukawa ina
mikakati inayofanana ndani ya vyama vyao ya kuhakikisha inajiimarisha
kisiasa nchi nzima ili ishinde Uchaguzi Mkuu.
Alisema siku
10 zilizopita, timu ya NCCR ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti - Zanzibar,
Haji Hamis Hamad ilianza ziara Kigoma kuhakikisha majimbo ya mkoa huo
yanaendelea kuwa ngome yake.
“Kigoma nzima ina majimbo yetu
ya kimkakati na Ukawa wameshatukabidhi sasa kilichobaki ni kufanya
‘political management’ (usimamizi wa kisiasa) katika kiwango
kinachotakiwa.
Musa Mateja
Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku
wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa
mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa
wanaishi kama mke na mume.
Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.
Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili liliwadamkia nyumbani
kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na
kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya
asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua
kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda
mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja
kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu
amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku
akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana
mahaba motomoto.
...Wakipozi kimahaba.
“Kwani tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye
uhusiano wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa
anajua kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi
wetu. Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:
“Yeah! Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda
mbele, sipendi kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu
upo vipi kwa sasa, ninampenda Shamsa.”
...Wakipata msosi.
Nay na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo
kudai kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya
sita kwa sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta
akiangukia kwa mwigizaji huyo.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba mmoja ya nyimbo yenye hisia kali sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sony Masamba akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Aneth Kushaba(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi(Kulia)
Ashura Kitenge akiimba kwa pamoja na Sam Mapenzi mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Joniko Flower(wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Aneth Kushaba AK 47 (kushoto) akiimba sambamba na Sony Masamba mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiwaimbia mashabiki wa bendi hiyo waliofika kwenye Kiota Cha Thai Village kuburusika na Bendi hiyo.
Mwandishi wetu
Taarifa zilizotua kwenye dawati la gazeti hili zinadai kuwa, wale
wamama wa mjini ambao walikuwa mashosti hadi kufikia hatua ya kusema ni
kama ndugu, mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven
Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’,
Lucresia Karugila, sasa kimenuka!
Mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.
DALILI KUWA PAKA NA CHUI Chanzo chetu cha kuaminika kilidai kuwa,
dalili za wawili hao kuelekea kugeuka kuwa paka na chui zilianza muda
mrefu lakini hali ikazidi kuwa mbaya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha
Kanumba, Aprili 7, mwaka huu alipokuwa akitimiza miaka mitatu kaburini. CHANZO NI LULU Ubuyu ulidai kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo
cha Kunumba, Mama Kanumba alimtuhumu Lulu kutotoa ushirikiano na kufikia
hatua ya kutoa maneno makali zaidi yaliyomkera mama Lulu.
Mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
MAMA KANUMBA NA SMS MBAYA KWA MAMA LULU Ilidaiwa kwamba, siku ya
kumbukumbu ya kifo cha Kanumba, mama Kanumba alimtumia mama lulu sms
mbaya ya kejeli (kuiandika hapa siyo busara) ndipo mama Lulu
‘alipofyumu’ na kuona kwa hali hiyo bora kama mbwai na iwe mbwai.“Ile
sms mama Kanumba alimtumia mama Lulu siku ile (Aprili 7) majira ya saa
11:00 alfajiri.
The Rock, Vin Diesel na Paul Walker ni baadhi ya majina ambayo yametajwa mwishoni mwa filamu ya kusisimua ya "Furious 7" iliyoingia sokoni hivi karibuni ... tatizo ni kwamba kuna baadhi ya watu ambao walishiriki kikamilifu kwenye matukio muhimu ya filamu hiyo ambao hawakupewa 'credit' mwishoni.
Sehemu ya matukio waliyoshiriki watu hao.
Vyanzo vya karibu na wazalishaji wa filamu hiyo vimeeleza kuwa watu hao walishiriki katika matukio muhimu ya filamu hiyo ikiwemo sehemu ya magari yenye parachuti na kukimbizana kwa magari maeneo ya milimani.
Mojawapo ya picha katika filamu ya Furious 7.
Kundi hilo la watu waliosahaulika limeeleza kuwa lilitoa jumla ya watu 25 ambao walihatarisha maisha yao katika filamu hiyo japo hawajatajwa mwishoni mwa filamu hiyo iliyojizolea umaarufu na kufanya vizuri sokoni ndani ya muda mfupi tangu itolewe.
Filamu hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza huko Australia Aprili 2, 2015, na baadaye kuzinduliwa nchini Marekani Aprili 3, 2015, na baada ya hapo iliachiwa kimataifa katika mfumo wa 3D.
Afisa Masoko na Mahusiano wa Proin Promotions Ltd, Josephat Lukaza akizungumzia Uzinduzi wa msimu wa pili wa Shindano la TMT 2015 lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao pia ni wasambazaji, wauzaji na watengenezaji wa filamu za Kitanzania. Anayeshuhudia pembeni ni Mratibu wa Masoko wa ITV/Radio One ambao ni mmoja wa wadhamini wa Shindano la TMT 2015.
Mratibu wa masoko kutoka ITV/Radio One (wa pili kulia) akizungumzia juu ya umuhimu wa wao ITV/Radio one kuwa washirika wa TMT 2015 na kuhaidi makubwa zaidi kwa mwaka 2015.P
Mmoja wa majaji wa shindano la TMT 2015 Yvonne Cherry au Monalisa akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na shindano la TMT 2015 lililozinduliwa rasmi leo jijini Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 limezinduliwa rasmi leo huku baadhi ya vigezo vikiwa vimeboreshwa, akizungumzia hayo Meneja wa Mradi wa TMT 2015, Saul Mpock amesema kuwa "Mwaka Huu Kigezo kimojawapo ni mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 16 na kuendelea huku fomu za kushiriki shindano hilo zikipatika siku ya usaili katika mkoa husika na bila gharama yoyote"
Shindano la Tanzania Movie Talents 2015 linaanza rasmi Kesho huku Kanda ya Ziwa ndio itakayofungua pazia la shindano hili kwa Mwaka 2015, Shindano hili linafanyika kikanda ambapo kanda sita za Tanzania zitafikiwa na shindano hili.
Kwa kanda ya Ziwa usaili utaanza tarehe 24 Aprili 2015 huku zoezi zima likifanyika mkoani Mwanza na hatimaye zoezi kuendelea kanda ya Kaskazini, Arusha, Kanda ya Kati, Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, Kanda ya Kusini, Mtwara na Kumalizika Kanda ya Pwani, Dar Es Salaam.
Katika kanda zote tano ikiwa Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kati, nyanda za juu kusini na Kusini Washindi watakuwa ni watatu kutoka kila kanda ambapo kila mshindi ataibuka na kitita cha shilingi laki tano kila mmoja huku kanda ya Pwani itatoa washindi watano na kila mmoja kuondoka na shilingi laki tano pia na kupelekea Washindi kuwa 20 na kuingia kwenye nyumba ya TMT kwaajili ya Hatua ya Mchujo.
TMT 2015 itarushwa na kituo cha ITV siku ya Jumapili saa tatu usiku huku kipindi cha kwanza kabisa cha TMT kikitarajiwa kuonekana tarehe 10 May 2015.
Shindano hili la TMT 2015 limedhaminiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Precision Air, I-View Studio, Global Publishers na Kituo cha ITV/Radio One ambao ndio watakaokuwa wakirusha matangazo ya TMT 2015. TMT ikiendelea kupata sapoti kutoka katika vituo mbalimbali za redio mikoani. Vilevile tunatoa nafasi kwa makampuni mengine ambao wangependa kushirikiana na TMT kwa mwaka 2015
Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers
Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho
kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji
wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania
wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.
Sifa kuu kwa mwanachama ni
kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa
mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka
kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania
Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala
na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Mwanachama muitaji wa kujiunga
kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha
mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa
mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama
(utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/-
na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi
kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu
litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu
pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na
Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.
Kwa wanachama wa
mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na
wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN.
Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu
usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa
muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu
zoezi la kujiunga uwanachama wa TBN.
Mikoani TBN itagawanyika
kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani
yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar
es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa,
Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara
na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na
Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa),
Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda
ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).
Kwa
wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama
wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili
kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama
waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.
NB;- Kwa
watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy
hiyo wataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft
coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.
Imetolewa na: Joachim Mushi, 0756469470 Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
Riri aka Rihanna ameng’arisha jarida la V na picha mpya zilizorudisha
muonekano wake wa Bad Girl Riri. Riri kaonekana kwenye picha hizi kifu
wazi akiwa na wig la ki blonde. Kwenye interview na jarida hili
amefunguka kuhusu album yake ya nane iliyotayarishwa na producer Kanye
West.