Wednesday, April 29, 2015

SHOO YA ZARI ALL WHITE PARTY YANUKIA, DIAMOND AJIPINDA KUHAKIKI TIKETI


STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' jana ametupia picha hii mitandaoni akihakiki tiketi kwa ajili ya shoo ya mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari' ya ZARI ALL WHITE PARTY itakayofanyika Ijumaa ya Mei 1, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
Staa huyo aliisindikiza picha hiyo kwa maneno haya:
"Sio kwa kiingilio hiki cha kuanzia Elf 50 hadi Milioni 3 eti nikajifanya naleta Uboss ... Mzigo Nausimamia mwenyeweee!!! Kushoto Manager @salaam_sk katikati nna @juju_utamu huku @queendarleen4real halaf kwambaaaaaali Mtoto katulia zake Anachat chat!... HAYA WALE WA ELFU HAMSINI NA WA LAKI KESHO NTAWATAJIA VITUO ZITAPOPATIKANA TICKET!!! #ZARIALLWHITEPARTY Friday May 1st 2015 Mlimani City Dar!!"
Kwenye shoo hiyo ya Zari, watu mbalimbali mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo dairekta mkubwa Afrika, Godfather wa Afrika Kusini na Top Ten ya Washiriki wa Shindano la Big Brother ‘Hot Shot’ 2014.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...