Sunday, June 29, 2014

TAIYA ODERO (SUZY) MAPENZI YAZIDI OFISI NA BOSS WAKE

Ile filamu iliyokuwa ikisubiriwa na watu wengi sana duniani ya INSIDE ya Jennifer Kyaka (Odama) cnini ya kampuni ya J-FILM 4 LIFE sasa itakuwa sokoni 10.07.2014. Utaweza kuona vituko vya maofisini kati ya wafanyakazi na mabosi. Taiya Odero (Suzy) ataona anavyofanya vitu vyake dhidi ya boss wa kampuni akitaka mapene kwa kupitia mapenzi na baadae kujutia tabia yake.


WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA MWANANYAMALA WAKABIDHIWA VIFAA


1. Baadhi ya manesi wakiwa na mwakilishi wa Upendo Women's Group Belgium, baada ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya kupunguza matatizo ya kina mama wajawazito katika Hospitali ya Mwananyamala.



2. Wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala wakifurahi baada ya kukabidhiwa vifaa maalumu kwa ajili ya huduma ya uzalishaji.



3. Bi. Begum Chunny, ambaye ni mwakilishi wa Watanzania waishio Ubelgiji akitembezwa katika wodi ya mama wajawazito.
4. Mama huyu mjamzito alikuwa anasubiri ndugu zake waje ili anunuliwe vifaa vya kujifungulia ila Bi. Begum alijitolea fedha kumsaidia.
5. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw. Ngonyani akiwa katika pozi.
6. Mwakilishi wa Upendo Women's Group Belgium, Bi. Begum akimsalimia mama mjamzito katika wodi ya wazazi, kushoto ni Muuguzi SP Mashauri.
7. Stendi maalumu kwa ajili ya drip nazo zilitolewa na Upendo Women's Group Belgium.
8. Wauguzi wakikabidhiwa kitanda maalumu.
9. Mpira huu maalumu kwa ajili ya kutandikwa eneo mama mjamzito analojifungulia.
10. Moja ya wodi ya akina mama wajawazito katika Hospital ya Mwananyamala.
BAADHI ya Watanzania wanawake wanaoishi nchini Ubeligiji kupitia Upendo Women’s Group Belgium, wamekabidhi baadhi ya vifaa katika wodi ya wajawazito Hospitali ya Mwananyamala kwa kumtuma mwakilishi wao ambaye yuko hapa nchini.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi 2,493,000/= ni pamoja na Litman Stethoscope, Ambu bag Paedreatic Bp Machine, drip stand, suction, emergency stretcher na vinginevyo.

WASHIRIKI 20 WA SHINDANO LA TMT WAINGIA RASMI KAMBINI JANA USIKU, TAYARI KWA SAFARI YA KUWANIA MILIONI 50‏



Muonekano wa TMT House ambayo washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents wameweka kambi rasmi kuanzia jana Usiku kwa mchakato wa kuwania Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane.


Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la TMT wakiingia kambini hapo jana usiku.

Mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kusini, Mwanaafa Mwizago akiingia rasmi kambini hapo jana wakati wakitokea kwenye matembezi. Washiriki wote 20 ambao ni washindi kutoka Kanda sita za Tanzania sasa wapo kambini kwaajili ya kujifua ili kuwania kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.

Washiriki wakiwa ndani ya Nyumba ya TMT tayari kwa kambi.

Washiriki wakipewa maelekezo mara baada ya kuwasili kambini hapo jana.


Na Josephat Lukaza - Proin Promotions - Dar Es Salaam.
Washiriki 20 kutoka Kanda sita za Tanzania wameingia rasmi kambini hapo Jana mara baada ya kumaliza zoezi la Kupima Afya, kutembezwa sehemu mbalimbali za Jiji la Dar pamoja na Ofisi za Global Publishers.

Washiriki hao watakaa kambini kwa Siku 64 ambapo wataanza rasmi kufundishwa Hapo kesho siku ya Jumatatu na walimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo ambapo baadae sasa baadae zoezi la kuanza kuwapigia kura washiriki hao litaanza na hatimaye watanzania ndio watakuwa majaji kwa washiriki hao ambapo mshindi mmoja wa Shilingi Milioni 50 atapatikana katika Fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Zoezi la Upigaji kura litaanza mapema wiki ijayo ambapo washiriki wote watakuwa tayari washapewa namba za ushiriki na hatimaye watanzania kuweza kuwachagua washiriki wanaowaona wana vipaji.
Zoezi hili la kupiga kura litapelekea Washiriki wawili kuondolewa kila wiki katika Kambi ya TMT ambapo pona yao ni kutoka kwa Watanzania ambao ndio watakuwa majaji kwa kuwapigia kura.

Vilevile Mara baada ya washindi hawa wa kanda kuingia kambini Vipindi vyetu vitaendelea Kurushwa kila siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku na Kurudiwa kila Siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa tano usiku kupitia Runinga ya ITV.
Tunawaomba watanzania kuendelea kutizama vipindi vyetu kwani vimekuwa na mvuto wa hali ya juu sana lakini pia kuendelea kuwawezesha

Washiriki wanaowaona wana vipaji ili kuwa ushindi.


Namba za washiriki zitaanza kuonekana katika Kipindi chetu kijacho ambapo Sasa watanzania wataanza kuwapigia kura kwenda namba 15678

Na ili kuweza Kufahamu taarifa zaidi za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678.

Saturday, June 28, 2014

AJALI YA BASI LA NBS YATOKEA KIMARA DAR


Muonekano wa mbele wa basi la NBS T719 AZC baada ya kugonga basi la Princes Muro T892 BUR lililokuwa likitokea Dar kwenda Mwanza eneo la Kimara.


Basi la Princes Muro T892 BUR likitokea Dar kwenda Mwanza limegongwa nyuma na basi la NBS T719 AZC likiwa safarini kuelekea Tabora eneo la Kimara leo.


Askari wa Usalama barabarani akiongea na abiria wa basi la NBS baada ya kutokea ajali.


Abiria wa basi la Princes Muro T892 BUR wakikagua basi lao.

CHANZO cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi la Princes Muro aliyekuwa akiendesha basi lenye namba za usajili T892 BUR ambapo akiwa upande wa kulia wa barabara, ghafla alichepuka upande wa kushoto kwa lengo la kumshusha mfanyakazi mwenzake mahala ambapo si kituo cha kushusha abiria.

WAAJIRI NCHINI KUCHUKULIWA HATUA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU



Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw. Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakifatilia mada mjini Dodoma leo.

BodiyaMikopoyaElimuyaJuunchiniimepangakuwachukuliahatuawaajiriwotenchinikwakushindwakuwasilishataarifazawahitimuwaelimuyajuuwanaodaiwanaBodihiyo.
HayoyalisemwanaMkurugenziMsaidiziUrejeshajiMikopokutokaBodiyaMikopoyaElimuyaJuuBw. Robert KibonaalipokuwaakitoamadakuhusuurejeshwajiwamikopoyaelimuyajuukwenyemkutanomkuuwamwakawaWakurugenziwaUtawalanaRasilimaliwatuSerikalinimjini Dodoma leo.

“MpakasasatumewachukuliahatuajumlayawaajiriwatanoambaowameshindwakuwasilishataarifazawatumishiwaowanaodaiwanaBodiyaMikopoyaElimuyaJuu” alisemaBw.Robert.

Alisema,mwajiriatakayeshindwakutoataarifazawahitimuwaelimuyajuukatikaBodikwawakatiatatakiwakulipafainiyashilingimilionisaba au kutumikiakifungokisichopunguamiezi 12 au vyotekwapamoja.

Aidha,Bw. Robert alisemakuwampakasasatakribaniwaajiriwa18 wamefikishwamahakamanikwakosa la kushindwakurejeshamikopohiyo.

Bw.Robertalifafanuakuwailikufanikishazoezi la urejeshajimikopokutokakwawadaiwa, BodiyaMikopoyaElimuyaJuuinatungasherianamifumombalimbaliyakuwadhibitiwadaiwahao.
“Tunatengenezasheriaambazozitawazuiawadaiwawamikopoyaelimuyajuukupatahatiyakusafirianjeyanchiau kibali cha kusafirihadiatakapowasiliananaBodi.”

Pia,alisemamhitimuatakayeshindwakulipamkopotaarifazakezitatangazwakwenyevyombovyahabarinakwenyetaasisizamikopoiliasipatehudumayoyoteyakifedha.
Naye, MsaidiziwaMkurugenziMtendajiBodiyaMikopoyaElimuyaJuu Dk. Veronica

Nyahendeamewatakawahitimuwaelimuyajuunchinikutumiaelimuwaliyonayokujiajiriwenyewebadalayakusubirikuajiriwa.
Alisemachangamotoyakurejeshamikoponikubwakwaupandewawahitimuwaelimuyajuuambaohawanakaziamahawajajiajiri.
“Changamotoiliyoponiwahitimukushindwakulipamikopohiyokutokananakuwanakipato cha chiniamakukosaajira.” AlisemaBodiimeingiamkatabanakampunizitakazokusanyamikopokwawalionufaikanamikopohiyonakushindwakuilipa
BodiyaMikopoyaElimuyaJuuikokatikamchakatowakuelimishaummanawatendajiwakuuSerikaliniilikuhakikishawanawasilishataarifazawatumishiwaowanaodaiwamikopohiyo.

Friday, June 27, 2014

VUNJA MBAVU ZAKO NA KITU CHA "INSIDE" AMBAYO INATOKA JULAI10.2014

Filamu hii Jennifer Kyaka (Odama) ambayo inayonyesha maisha ya wafanyakazi maofisi wanaovyofanya vituko na mabosi wao na wengine hata kumkufuru na kumuudhi Mungu kwa vitendo vya rushwa na uvivu kazini, kwa mana Mungu amesema asiyefanya kazi na asile. Watu badala ya kufanya kazi wanabaki kupiga stori na majungu maofisi. Wadada wanavyotumia uzuri wao kuwalaghai waume za watu kwa kutoa rushwa ya ngono. Hakika kama mcha Mungu ndani ya hii filamu utajifunza mengi na utaburudika na vituko vya wasanii maarufu wa kuchekesha kama KING MAJUTO na  BENY, pia utamuona marehemu RACHEL HAULE, DAVINA, ODAMA, DULLAH WA PLANET BONGO, na wengine wemgi sana. Filamu hii ambayo imetengezwa na kampuni bora Tanzania ya J-FILM 4 LIFE itakuweka mahali fulani KIMAWAZO.


EMMANUEL MBASHA NA MKE WAKE WA NDOA FLORA MBASHA WAPATANA


HAKUNA neno zuri la kusema zaidi ya Mungu mkubwa! Ule mtafaruku ndani ya ndoa ya mwimba Injili mahiri Bongo, Flora na mumewe, Emmanuel Mbasha umedaiwa kumalizika kwa wawili hao kupatana, Risasi Jumamosi linakuwa nambari wani kukuhabarisha.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, wawili hao walikalishwa kikao cha upatanishi mapema wiki hii kilichokuwa chini ya familia.
Mume wa Flora Mbasha, Bw. Emmanuel Mbasha.
MANENO YA CHANZO
“Kikao cha familia kilikaa, Mbasha aliitwa akafika, Flora naye aliitwa akatokea, mazungumzo yalikuwa marefu lakini kimsingi waliamua kuweka kando mtafaruku wao na kuijenga upya ndoa yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliongeza kuwa katika kikao hicho cha mwanzoni mwa wiki hii, miongoni mwa adidu za rejea ilikuwa kutokumbushia vikao vilivyopita ambapo hakukupatikana muafaka.
VIKAO VILIVYOPITA
Katika vikao vilivyopita, wahusika wakuu walikuwa wazazi wa Mbasha (mzee Maneno Mbasha, Zulfa Maneno), ndugu wa Flora na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Mwimbaji Injili mahiri Bongo, Flora Mbasha.
VIKAO VYA BAADAYE
Kwa mujibu wa chanzo, vikao vilivyofuata, wawili hao wakawa tayari kila mmoja ametema nyongo yake pembeni na kufikia makubaliano kwamba, ndoa yao isimame tena wakitumia maandiko kwenye Biblia kutoka kitabu cha Waebrania yanayosema:    Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
WAKORINTHO YAFUNGA KAZI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, maneno mengine ya Biblia yaliyotumika kwenye kikao hicho mpaka wawili hao wakaamua kurudiana ni 1 Wakorintho 7:1-10 ambapo maandiko yanasema:
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
Flora Mbasha akiwa kwenye picha ya pamoja na mumewe, Emmanuel Mbasha.
Mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe. Msinyimane, isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali, mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala hapo si mimi, ila Bwana (Mungu), mke asiachane na mumewe, lakini ikiwa ameachana naye na akae asiolewe au apatane na mumewe, tena mume asimwache mkewe.
KIKAO CHA JUMAMOSI KUMALIZIA
Chanzo kilisema kuwa, kikao cha mwisho ambacho kitamalizia kuweka mambo sawa ili wawili hao waanze ngwe ya pili ya ndoa yao ambayo inaaminika itakuwa ya mwisho mpaka kifo kiwatenganishe, kinatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam mahali ambapo hapakutajwa.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
MWANASHERIA ATAJWA
Mwanasheria wa Flora aliyejulikana kwa jina moja la Ado ametajwa kusimamia kikao hicho ili wawili hao waanze maisha mapya baada ya safari fupi ya mvurugano uliowafanya kuwa mbalimbali.
AONGEA NA RISASI JUMAMOSI
Juzi, Risasi Jumamosi lilimsaka mwanasheria huyo kwa njia ya simu yake ya mkononi ili kumsikia anasemaje kuhusu kutajwa kwenye usuluhishi wa ndoa hiyo ambapo alipopatikana alisema:
“Niko Arusha, Ijumaa nitarudi Dar. Kuhusu kikao cha usuluhishi siwezi kukwambia lakini suala la kuwapatanisha nalifahamu, nawaomba na ninyi msaidie kufanikisha jambo hilo zuri.”
VIPI KUHUSU KESI YA MADAI YA KUBAKA?
Hata hivyo, Wakili Ado hakutaka kugusia kuhusu kesi ya Mbasha iliyopo Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo anadaiwa kumbaka shemejiye mara mbili (jina tunalo) ambayo kwa mujibu wa mahakama, upelelezi umekamilika na itasikilizwa Julai 17, mwaka huu.
KWA UPANDE WAKE FLORA
Risasi Jumamosi lilimwendea hewani, Flora ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa upatanishi kati yake na mumewe, Emmanuel.
Huyu hapa: “Ongea na wakili wangu atakwambia kila kitu.” Ambapo majibu ya wakili yalikuwa: ”Ninachojua mimi ni kwamba Flora ameshamsamehe mumewe na yuko tayari kuanza ukurasa mpya.”
MBASHA SASA
Kwa upande wake, Mbasha alipozungumza na gazeti hili juzi alisema kurejea upya kwa ndoa yake ni jambo la kuupendeza moyo wake.
“Mimi sina neno nipo tayari, nimeshasamehe yaliyotokea, Flora ni mke wangu jamani, nampenda sana kutoka moyoni.”

Wednesday, June 25, 2014

KITU CHA "INSIDE" CHA MWANA MAMA JENNIFER KYAKA (ODAMA) KUACHIWA JUNI/10/2014

Sasa ile filamu iliyokuwa ikisubiliwa na Watanzania wengi ya INSIDE kutoka kwa Jennifer Kyaka (Odama) itakuwepo sokoni 10.07.2014. Filamu hii ambayo imechezwa katika  mazingira ya ofisini ikionyesha vituko vinavyofanyika maofisi na wafanyakazi na pia mabosi. Kama kawaida ya kampuni ya J-Film 4 Life ndio iliyohusika katika kutengeneza filamu hii ambayo ukiangalia utavutiwa na kujua mengi kuhusiana na vituko vya vinatokea  maofisini

Ndani ya filamu hii kuna vituko vya ajabu ukisingatia yumo Majuto, Beny, Dullah, marehemu Rachel Haule, Odama na wengine wengi kama unavyoona katika cover. Jipange mtu wangu kujipatia hii nakala ambayo mpya upate kuongeza siku zako za kuishi kwa kicheko.


Saturday, June 21, 2014

AJALI YA KUTISHA YATOKEA LUGALO DAR

Magari mawili aina ya Coaster yanayosafririsha abiria kati ya Mwenge, Tegeta na Mbezi jiijini Dar, yamegongana na na kuua abiria wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 10, ajali hiyo imetokea mchana huu eneo la Makongo. Mashahuda wa ajali hiyo wamesema kuwa uzembe uliofanywa na dereva wa daladala iliyokuwa ikitoka Tegeta ndiyo uliosababisha ajali hiyo, kwani alipita upande usiyo wake.

Kushoto ni gari ndogo aina ya Range Rover ambayo iligongwa na Daladala (kulia) iliyosababisha ajali hiyo


...Daladala hiyo inavyoonekana mara baada ya ajali…


Kushoto ni gari ndogo aina ya Range Rover ambayo iligongwa na Daladala (kulia) iliyosababisha ajali hiyo


...Daladala hiyo inavyoonekana mara baada ya ajali


Askari wa usalama akichukua maelezo eneo la tukio


...eneo la ajali linavyoonekana mchana huu.


Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Gari ndogo aina ya Range Rover ambayo iligongwa na Daladala.



Baadhi ya miili ikiwa kwenye gari Hospitali ya Lugalo.


Daktari akiendelea kutoa huduma ya kwanza ndani ya gari la wagonjwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Lugalo, Brigedia Jeneral, Josia Mekere.

Madaktari wa Hospitali ya Lugalo wakiendelea kuwahudumia majeruhi.

Ndugu wakilia kwa uchungu baada ya kutambua miili ya ndugu zao.


Mzee aliyefiwa na mwanae akilia kwa uchungu.


...Baadhi ya maaskari na wananchi waliokuwa wakitoa huduma ya kwanza eneo la tukio.


Mtangazaji wa Global TV Online, Gabriel Ng'osha akiwa eneo la tukio.

TAMASHA LA ATOSHA KISSAVA LASOGEZWA MBELE KUTOKANA NA MSIBA WA DEBORA SAID

Siku ya Jumapili 22/06/2014 ilikuwa ni siku ya kufanyika uzinduzi wa albamu ya Atosha Kissava katika kanisa la marehemu mama mchungaji Debora Said hapo Mabibo Extenal Ubungo jijini Dar es Salaam. Tamasha hili halitafanyika mpaka mtakapotangaziwa tena.
Tunawaomba radhi kwa yote yaliyotokea na tunasikitika sana na kifo cha mtumishi wa Mungu Debora Said

ASANTENI

Atosha Kissava


MOTO WAZUKA CHUO CHA UDOM USIKU WA KUAMKIA LEO

Moto ukiendelea kuwaka usiku wa kuamkia leo karibu na hostel za wasichana katika skuli ya sanaa na lugha (School of Humanities) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Wakaazi wa mji huo walisikia vingo'ra vya magari ya zimamoto yakielekea chuoni huko kwa kasi usiku wa manane.




RUMAFRICA INAWAPA POLE WATANZANIA KWA KIFO CHA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI DEBORA SAID


Hakika tumesikitishwa sana na kifo cha mama mchungaji Debora Said. Tumepungukiwa na moja ya nguzo kubwa katika kumtangaza Yesu Kristo.

Marehemu mama mchungaji Debora Said

Ni wakati mgumu sana kwetu kwa maana tumepungukiwa na mjumbe aliyekuwa akitupa Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji. Sisi tuliobaki tuzidi kumtumikia Mungu wetu kwa maana hatuji ni lini tutamfuata Debora Said.

Pia tunwapa pole ndugu na jamaa zake na marehem Debora Said

Mkurugenzi wa Rumafrica Rulea Sanga-RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

----------------------------
ANGALIA MAHOJIANO YA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI DUNIANI YALIYOFANYIKA NA RUMAFRICA KATIKA KIPINDI CHA RUMAFRICA ONLINE TV

Friday, June 20, 2014

HOW TO FIX DISABLE IPHONE, IPOD,IPAD

MUME WA FLORA MBASHA YUPO NJE KWA DHAMANA



Shetani mbaya! Wakati jana mumewe Emmanuel Mbasha (32) akipandishwa kizimbani kwa mara ya pili kwa soo la ubakaji wa shemejiye, mwimba Injili kinara Bongo, Flora Mbasha (31) amepitia katika hatua tatu za aibu, Ijumaa lina ripoti kamili.
Mwimba Injili kinara Bongo, Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha.

Mbasha ambaye naye ni mwimba Injili na mfanyabiashara alitarajiwa kupandishwa kizimbani jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Ilala, Dar akitokea mahabusu Keko akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Flora ambaye alihama nyumbani na kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza, Dar, kitendo hicho kilimuingiza staa huyo kwenye hatua ya tatu ya aibu na kujikuta akiwa katika masikitiko makubwa.

AIBU YA KWANZA
Kwa mujibu wa mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina, aibu ya kwanza inayomuuma Flora ni ile ya ndoa yake kuingia kwenye gogoro kisha kudaiwa kutengana na mumewe kinyume na kile anachokihubiri kupitia nyimbo zake zinazopendwa na wengi ndani na nje ya Bongo.

Binti wa miaka 17 anayedaiwa kubakwa na mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili Bongo Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha.

“Unajua lile neno la ‘mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’ (Mithali 14:1) linamfanya awe na aibu mbele za watu.
“Unaambiwa kanisani (anasali Kanisa la Ufufuo na Uzima la Mchungaji Josephat Gwajima kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar) anaona aibu hasa kwa waumini wenzake.

“Flora amedumu na Ima (Mbasha) kwenye ndoa kwa miaka 12 hivyo kutokea kwa kilichotokea ni aibu kwani tayari walikuwa wamekomaa tofauti na walipoona wakiwa na umri mdogo.
“Hebu fikiria, mtoto amekuwa mkubwa, anaposikia mama ana matatizo na baba si ni aibu jamani? Cha msingi tuwaombee wamalize matatizo yao, inaweza kusaidia kuifuta aibu hiyo kwani imeandikwa ‘Ndoa na iheshimiwe na watu wote...’ ( Waebrania 13 : 4 -),” alisema mnyetishaji wetu akisisitiza kuwa akitajwa gazetini ataonekana mvujishaji wa mambo ya siri ya wanandoa hao.

AIBU YA PILI
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa aibu ya pili inayomkabili Flora ni skendo ya yeye kudaiwa kuhamishia makazi kwa mchungaji wake, Gwajima.

Katika aibu hiyo, mumewe alinukuliwa na gazeti mama la hili, Uwazi akimlalamikia mchungaji huyo amwachie mkewe kwani yeye ndiye alisababisha sakarakasi zote hizo za ndoa yake.
Ilidaiwa kuwa kwa mke wa mtu achilia mbali mhubiri kwa njia ya nyimbo, kitendo cha kukumbwa na skendo nayo ni aibu pia.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.

“Kwa mtumishi kutajwa kwenye jambo kama hilo lisilo na mrengo wa kupendeza masikioni mwa watu, ni aibu kuu,” kilidai chanzo hicho.

AIBU KUU YA TATU
Ilisemekana kuwa achilia mbali ndoa, mambo ya mchepuko lakini aibu kuu ya tatu kwa Flora, ni kashfa ya ubakaji wa shemejiye inayomkabili mumewe Mbasha.
“Unajua usifikirie kwamba mume akipata aibu mke anaweza kuikwepa. Hawezi kwa sababu ‘wanazungumza lugha moja’ (yaani ni mwili mmoja). Ona sasa mume anapandishwa kizimbani kwa ubakaji.
Mwimbaji wa nyimbo za injili Bongo Flora Mbasha

“Pia usifikiri watu watasema kashfa ni ya Ima peke yake. Kwanza hata kutamka watu wanasema mume wa Flora. Ikumbukwe aibu ya mume ni ya mke pia. Ni vigumu mno kwa Flora kusema aibu ni ya mumewe pekee,” alitiririka mto habari huyo.

FAMILIA ZATOFAUTIANA
Wakati hayo yakiendelea, habari zinadai kuwa familia za pande zote zinatofautiana huku kila moja ikilaumu nyingine.

Ilidaiwa kuwa upande wa Mbasha unamlalamikia mama wa Flora kuwa anamuunga mkono mwanaye badala ya kusaidia kutuliza hali ya hewa.

Ilielezwa kuwa upande wa Flora wao wanamlaumu Mbasha kwa madai kuwa chanzo cha yote ni mgawanyo wa mali hasa baada ya kuona kuwa hakuna tena ndoa.
FLORA ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa juzi kwa njia ya simu, Flora alitoa la moyoni: “Kweli naumia sana tena sana. Kwa sasa kesi ipo mahakamani, siwezi kuizungumzia lakini ndiyo hivyo. Siyo siri nateseka sana.”
Mbasha anadaiwa kumbaka ndugu wa Flora ambaye ni yatima kati ya Mei 23 na 25, mwaka huu ambapo kesi yake inaendelea kuunguruma baada ya kukaa mahabusu ya Keko kwa siku kadhaa ambapo sheria ndiyo itakayoanika siri zote juu ya sakata hilo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...