Tuesday, March 31, 2015

WEMA, IDRIS MAHABA NIUE!

WAPENZI? Kwa mara nyingine Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu amesababisha kichwa cha habari kufuatia kunaswa ‘live’ usiku mnene akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan wakioneshana vitendo vya ‘nakupenda tu’ mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
NI ESCAPE ONE MIKOCHENI
Wawili hao walinaswa wakioneshana mahaba niue hayo usiku wa kuamkia Machi 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar walipokuwa wamekwenda kushuhudia shoo kali ya mpambano kati ya Bendi za The African Stars ‘Twanga Pepeta’ na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
PICHA LILIVYOANZA
Awali, paparazi wetu aliyeamua kulivalia njuga tukio hilo alimshuhudia Wema akiingia ukumbini humo akiwa sanjari na kampani yake, akiwemo shosti wake mkubwa kwa sasa, Aunt Ezekiel na mshauri wake  kikazi, Petit Man.
Walikwenda kukaa kwenye viti vilivyokaribiana na kuanza kufuatilia mpambano wa bendi hizo mbili kubwa nchini uliokuwa ukiendelea jukwaani kwa kishindo kikuu.
Idris akimweleza jambo Wema Sepetu.
PETIT AKAA NA MADAM
Kutokana na mpangilio wa watatu hao, Petit Man alikaa katikati ya Wema (kushoto kwake) na Aunt, lakini muda mwingi alikuwa akinong’onezana na Madam huyo huku wakionekana kuzungumza mawili matatu yahusuyo mpambano huo unavyoendelea.
IDRIS NDANI YA NYUMBA
Ndani ya dakika kama ishirini tangu Wema na msafara wake waingie ukumbini humo, Idris naye aliwasili akiwa ameongozana na mdogo wa hiari wa Wema aitwaye Bite pamoja na mtu mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Nao walikwenda walipokuwa wamekaa akina Wema.
ONA HII SASA
Kuonesha kwamba itifaki inazingatiwa, Idris alipofika mahali hapo, Petit alisogeza nyuma kiti chake na kuwafanya Wema na Idris waweze kukaribiana na kuzungumza kwa ujirani zaidi.

Wakipozi kimahaba.
WAANZA KUNONG’ONEZANA
Kitendo cha wawili hao kukaa karibu tu, fasta walianza kuongea kwa staili ya kunong’onezana kwa muda mrefu, wakati mwingine wakishikana mikono.Kuna wakati walikwenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kupapasana mapajani huku wakiendelea kuzungumza maneno ambayo hayakuweza kusikika kwa sababu ya sauti ya muziki ukumbini hapo kuwa juu.
WAFUTANA JASHO
Kama vile hiyo haitoshi, ilifika mahali Wema alionekana usoni kuvuja jasho kwa mbali, basi alichukua skafu ya Idris kutoka shingoni na kujifuta ambapo Idris naye alimsaidia na baadaye Wema naye alifanya vivyo hivyo pale mwenzake huyo naye alipotokwa na jasho.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
“Mh! Mwenzangu we acha tu. Hii ndiyo inaonesha sasa Wema na Idris kuna kitu, maana siku za hivi karibuni, kila alipokuwa anakwenda Wema, Idris naye alikuwa hakosi sasa leo hapa ndiyo full mahaba niue, hatari,” alisikika mpenda ‘ubuyu’ mmoja.
PICHA ZINAJIELEZA?
Baada ya paparazi wetu kuwafotoa picha kadhaa wawili hao, alimfuata Wema na kumuuliza ili kujua kama ameamua kujiweka ‘mazima’ kwa Idris au la! Wema alijibu kwa kifupi:“Bwana wee si kila unachokiona kinahitaji ufafanuzi, wewe si ushapiga picha inatosha, maswali ya nini sasa?”
IDRIS AGOMA KUZUNGUMZA
Jitihada za kuzungumza na Idris ziligonga mwamba kutokana na staa huyo wa BBA aliyejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani laki tatu (zaidi sh mil. 514) kutokuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na ukaribu wake na Wema ukumbini hapo.
Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
MUDA WA KUONDOKA WAFIKA, WAONDOKA PAMOJA
Wakati shoo ikielekea ukingoni, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiongozana  katika msafara mmoja na Aunt, Petit na Bite ambapo walitokomea kusikojulikana.

Stori imetayarishwa na Musa Mateja, Chande Abdallah na Deogratius Mongela.

NIYONZIMA KUUNGANA NA WENZAKE LEO



Niyonzima
Kikosi cha Yanga kimeendeleza kimbizakimbiza ya kusaka mbinu za kuimaliza FC Platinum ya Zimbabwe kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Jumamosi wiki hii baada ya jana na leo kuwa katika makamuzi makali.
Hata hivyo taarifa mbaya ni kocha Hans van Der Pluijm amemkosa kiungo wake, Haruna Niyonzima ambaye hajarudi kutoka kwao ambapo alikwenda kuitumikia timu yake ya taifa, Rwanda katika michuano ya kirafiki ya kalenda ya Fifa.

Kikosi cha Yanga katika mazoezi leo asubuhi, kwenye Uwanja wa Karume, Dar.

Akizungumza na Tanzania One leo baada ya mazoezi ya klabu hiyo kwenye Uwanja wa Karume, Dar alisema kiungo huyo anatarajiwa kutua leo ama kesho.
“Niyonzima huenda akawasili leo ama kesho ili kuungana na kikosi katika safari yetu ya kwenda Zimbabwe,” alisema kiongozi huyo.
Matokeo yoyote chini ya kichapo cha mabao 4-0 yataisongesha mbele Yanga kwenye hatua ya pili ya mtoano kabla ya kutinga katika hatua ya makundi kwani ina mtaji wa mabao 5-1 walioupata katika mchezo wa awali jijini Dar.



MAAJABU YA DUNIA, MAMA AWAFUNGIA NDANI WANAWE 3 KWA MIAKA 10! WAZALISHANA

Na Haruni Sanchawa, Mafia
NI mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Kanga Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani wakimsindikiza mwandishi wa gazeti la Uwazi, Haruna Sanchawa (hayupo pichani) kuelekea nyumbani kwa Bi. Mwasiti Ally.
Uwazi lilipata habari hizi kupitia kwa wasomaji wake waishio Mafia na kuamua kufunga safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina yake. 
UWAZI LACHANJA MBUGA KUFUATILIA
Baada ya kufika Mafia mjini, Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa kilomita 40 kutoka mjini hadi kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.
UWAZI LAANZA NA JIRANI
Kabla ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi lilibahatika kuwapata majirani ambapo mmoja wao alisema watoto hao ambao ni baba mmoja, mama mmoja, walianza kuwa katika hali ya kushangaza kiakili mwaka 2001.
“Alianza mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo hilo liliishangaza familia na hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.
Bi. Mwasiti Ally akiwafungulia wanaye aliowafungia ndani kwa miaka 10.
MAMA MZAZI SASA
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili, hawako sawa. Nateseka nao sana.“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri. Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma. Nikashangaa ni nini? “Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”
Ally Juma ni mmoja kati ya watoto wa wanodaiwa kufungiwa ndani kwa miaka 10 na mama yao mzazi Mwasiti Ally (pichani). HISTORIA YAO FUPI
Mwanamke huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto saba, watatu ambao wote ni wakubwa ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili na wanne ambao ni wadogo wapo sawa na wameolewa wakiendelea na maisha yao ya ndoa.
AWATAFUTA WATU KUMSAIDIA
Akiendelea kuzungumza na Uwazi, mwanamke huyo ambaye ni mjane alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo alizunguka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao wamerogwa.
 
Bi. Mwasiti Ally akimnyanyua mwanaye Ally Jum.
“Nimehangaika sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu wana matatizo ya akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema mama huyo.
Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona imeshindikana na watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuwaogopa watu, kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia eneo la baharini.
WAJENGEWA KIJUMBA, WAFUNGIWA HUMO
Mwasiti alisema muda wote huo alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika mwaka 2005 aliamua kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao waweze kuishi humo wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi leo.
HALI ZAO NDANI YA KIJUMBA
Wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Lakini mama mtu anatoa sababu ya kuwafungia:“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.”
 
Ally Juma mwenye ugonjwa wa akili.
NINI KILITOKEA BAADA YA KUWAFUNGIA?
“Miezi ya hivi karibuni nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye kidogo bado anajiweza kinguvu.”Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).
 
Muhadia Juma mwenye ugonjwa wa akili, naye anadaiwa akufungiwa ndani mama yao mzazi kwa miaka 10.
SIKU YA KUJIFUNGUA
Inadaiwa kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia, familia ilishirikiana na uongozi wa kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo alijifungua salama.Baada ya kujifungua, Muhadia alirudishwa kijijini lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo.
Mzee Juma anayedaiwa kumpa mimba dada yake Muhadiya Juma, akiwakimbia wanakijiji walioongozana na mwandishi wa gazeti la Uwazi.
MJUMBE NAYE
Naye mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Seleman alipoulizwa kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli mjane huyo amekuwa akiishi na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka kumi sasa tangu walipoanza kupata matatizo.
Mjumbe wa nyumba 10 pamoja na Bi. Mwasiti Ally wakimuonesha mwandishi wa gazeti la Uwazi kaburi la mtoto wa Muhadiya.
“Watoto wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa ajili ya matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna mafanikio kama unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.
“Inawezekana wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini afya zao zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani, ikiwemo kujisaidia. “Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
Bibi wa watoto hao.
WITO
Kwa hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa serikali, taasisi na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo kuishi na watu wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado ni tatizo kwa eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani haionekani kama ni suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya sheria.
Ushahidi wa uduni wa elimu unaonekana hata kwenye kujua mambo muhimu. Mfano, mwanamke huyo hajui tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa mtoto wake hata mmoja kati ya watoto wote saba!

Monday, March 30, 2015

MWILI WA MAREHEMU ABDUL BONGO WAPELEKWA MORO KWA MAZIKO

Mwili wa Abdu Bonge ukitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwanyamala jijini Dar ili kuhamishiwa Muhimbili.

MWILI wa aliyekuwa mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdu Bonge, mapema leo asubuhi ulihamishwa kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala na kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Baada ya uchunguzi huo kukamilika ulichukuliwa na kupelekwa Magomeni Kagera kwaajili ya kuagwa na baadaye safari ya kwenda mjini Morogoro kwa shughuli za maziko yanayotarajiwa kufanyika kesho majira ya saa 7 mchana.

ANGALIA MATUKIO YA PICHA KWENYE SHOO YA LADY JAYDEE, ALI KIBA

DSC_0248
DSC_0035Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
DSC_0083
DSC_0078
DSC_0046
Umati wa mashabiki wa Machozi Band wakipata burudani kutoka kwa band hiyo inayoongozwa na Lady Jay Dee.
DSC_0048
DSC_0065
DSC_0066
DSC_0204
Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.
DSC_0217
Ali Kiba akiendelea kuwaburudisha mashabiki wake Machozi Band.
DSC_0219
Warembo walipagawajem sasa.
DSC_0253
Mrembo akijinafasi kwa Ali Kiba.
DSC_0275
#ChekechaCheketua.......Wadada wakichizika na mauno ya Ali Kiba na style yake mpya.
DSC_0283
Mwanadada hakukubali kabisa na kuamua kupanda jukwaani kulipiza mauno ya Ali Kiba.
DSC_0284
Picha inajieleza jinsi Ali Kiba alivyokonga nyoyo za mashabiki wake.
DSC_0296
Lady Jay Dee: Nimemkuta analia, kajilaza, sababu amechoka.....Mengi amevumilia, yalomkwaza, anataka kuondoka....ana siku ya pili sasa, hajarudi nyumbani kulala,...namuonea huruma sana, haya....mapenzi hayana maana
Lady Jay Dee: who the single girl.....who the single boy, Ali Kiba: i am a single boy.......Ali Kiba: who the single girl, .......Lady Jay Dee: i am a single girl.......Lady Jay Dee: who the single boy, Lady Jay Dee na Ali Kiba:....mi na we single boy.
DSC_0300
Tumefunika mbaya mtu wangu....ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.
DSC_0281
DSC_0256
DSC_0010
Binti mrembo binti kwenye kipaji Faraja wa Machozi Band akiwapa raha mashabiki wa Band hiyo Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani kiota cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge).
DSC_0142
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D akiwarusha mashabiki wake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0158
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D katika hisia kali za kuwapa raha mashabiki wake.
DSC_0144
Vijana wakijiachia vilivyo baada ya Reggae za Double D kuwakolea ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0170
Omirady wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa Band hiyo katika show inayopigwa mara moja kwa mwezi na kuwateka mashabiki wengi ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0015
Msanii Chiqitita wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa band hiyo (hawapo pichani).
DSC_0059
Mashabiki wa machozi band wakipata Ukodak.
DSC_0193
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Live Band uliofurika Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani ya M.O.G Bar & Restaurant kushuhudia show ya wakali wa muziki nchini Lady Jay Dee na Ali Kiba.
DSC_0001
Hawa jamaa ndio wanaohakikisha Lady Jay Dee anakuwa salama siku zote

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...