Tuesday, March 31, 2015

WEMA, IDRIS MAHABA NIUE!

WAPENZI? Kwa mara nyingine Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu amesababisha kichwa cha habari kufuatia kunaswa ‘live’ usiku mnene akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan wakioneshana vitendo vya ‘nakupenda tu’ mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
NI ESCAPE ONE MIKOCHENI
Wawili hao walinaswa wakioneshana mahaba niue hayo usiku wa kuamkia Machi 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar walipokuwa wamekwenda kushuhudia shoo kali ya mpambano kati ya Bendi za The African Stars ‘Twanga Pepeta’ na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
PICHA LILIVYOANZA
Awali, paparazi wetu aliyeamua kulivalia njuga tukio hilo alimshuhudia Wema akiingia ukumbini humo akiwa sanjari na kampani yake, akiwemo shosti wake mkubwa kwa sasa, Aunt Ezekiel na mshauri wake  kikazi, Petit Man.
Walikwenda kukaa kwenye viti vilivyokaribiana na kuanza kufuatilia mpambano wa bendi hizo mbili kubwa nchini uliokuwa ukiendelea jukwaani kwa kishindo kikuu.
Idris akimweleza jambo Wema Sepetu.
PETIT AKAA NA MADAM
Kutokana na mpangilio wa watatu hao, Petit Man alikaa katikati ya Wema (kushoto kwake) na Aunt, lakini muda mwingi alikuwa akinong’onezana na Madam huyo huku wakionekana kuzungumza mawili matatu yahusuyo mpambano huo unavyoendelea.
IDRIS NDANI YA NYUMBA
Ndani ya dakika kama ishirini tangu Wema na msafara wake waingie ukumbini humo, Idris naye aliwasili akiwa ameongozana na mdogo wa hiari wa Wema aitwaye Bite pamoja na mtu mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Nao walikwenda walipokuwa wamekaa akina Wema.
ONA HII SASA
Kuonesha kwamba itifaki inazingatiwa, Idris alipofika mahali hapo, Petit alisogeza nyuma kiti chake na kuwafanya Wema na Idris waweze kukaribiana na kuzungumza kwa ujirani zaidi.

Wakipozi kimahaba.
WAANZA KUNONG’ONEZANA
Kitendo cha wawili hao kukaa karibu tu, fasta walianza kuongea kwa staili ya kunong’onezana kwa muda mrefu, wakati mwingine wakishikana mikono.Kuna wakati walikwenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kupapasana mapajani huku wakiendelea kuzungumza maneno ambayo hayakuweza kusikika kwa sababu ya sauti ya muziki ukumbini hapo kuwa juu.
WAFUTANA JASHO
Kama vile hiyo haitoshi, ilifika mahali Wema alionekana usoni kuvuja jasho kwa mbali, basi alichukua skafu ya Idris kutoka shingoni na kujifuta ambapo Idris naye alimsaidia na baadaye Wema naye alifanya vivyo hivyo pale mwenzake huyo naye alipotokwa na jasho.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
“Mh! Mwenzangu we acha tu. Hii ndiyo inaonesha sasa Wema na Idris kuna kitu, maana siku za hivi karibuni, kila alipokuwa anakwenda Wema, Idris naye alikuwa hakosi sasa leo hapa ndiyo full mahaba niue, hatari,” alisikika mpenda ‘ubuyu’ mmoja.
PICHA ZINAJIELEZA?
Baada ya paparazi wetu kuwafotoa picha kadhaa wawili hao, alimfuata Wema na kumuuliza ili kujua kama ameamua kujiweka ‘mazima’ kwa Idris au la! Wema alijibu kwa kifupi:“Bwana wee si kila unachokiona kinahitaji ufafanuzi, wewe si ushapiga picha inatosha, maswali ya nini sasa?”
IDRIS AGOMA KUZUNGUMZA
Jitihada za kuzungumza na Idris ziligonga mwamba kutokana na staa huyo wa BBA aliyejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani laki tatu (zaidi sh mil. 514) kutokuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na ukaribu wake na Wema ukumbini hapo.
Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
MUDA WA KUONDOKA WAFIKA, WAONDOKA PAMOJA
Wakati shoo ikielekea ukingoni, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiongozana  katika msafara mmoja na Aunt, Petit na Bite ambapo walitokomea kusikojulikana.

Stori imetayarishwa na Musa Mateja, Chande Abdallah na Deogratius Mongela.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...