Monday, February 29, 2016

WIKI MBAYA KWA DIAMOND NA NAY WA MITEGO ILIKUWA HII HAPA!!


Diamond Platnumz akiwa kwenye pozi la huzuni.
MAJANGA! Wiki iliyopita mambo hayakuwaendea poa mafahari wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kila mmoja kupatwa na masaibu yake, Ijumaa Wikienda linakupa moja baada ya jingine.

TUKIO LA DIAMOND

Chanzo makini kilichoshuhudia sakata zima kilieleza kuwa, Jumanne iliyopita Diamond aliingia kwenye ‘tifu’ zito na kijana aliyefamika kwa jina la Salehe Hafidhi ‘Ans Ken’ baada ya kumharibia kamera yake aliyompa kwa lengo la kumfanyia kazi zake.

“Palichimbika, Diamond alimkabidhi Ans Ken kamera yenye thamani ya shilingi Mil. 12 kama kitendea kazi maana anafanya naye kazi. Sasa jamaa akaiharibu, Diamond alipohoji jamaa akajibu mbovu ndipo mtiti ulipoibuka.

“Ilikuwa ni mvutano mzito Diamond akimtaka kijana huyo amlipe kamera yake jamaa akawa analeta ubishi ndipo Dangote (Diamond) akaona isiwe shida bora akimbilie polisi Mabatini (Kijitonyama) kushtaki na jamaa akakamatwa na kuwekwa ndani,” kilisema chanzo hicho.

MTUHUMIWA AKANUSHA TUKIO

Baada ya mwanahabari wetu kunasa tukio zima, alimvutia waya mtuhumiwa (Ans Ken) ambaye aliachiwa kwa dhamana siku moja baada ya kuswekwa lupango ambapo alikanusha kuwa tukio la yeye kugombana na Diamond halikutokea.

“Kwanza mimi siitwi hayo majina uliyonitajia, sina tatizo na Diamond na wala sitaki kugombana naye siku si nyingi nimetoka naye South kufanya kazi,” alisema.

AZIDI KUJIKANYAGA

Alipohakikishiwa na mwanahabari wetu kuwa ana RB inayomuonesha kuwa yeye ni mtuhumiwa wa Diamond, Ans Ken kwa kujikanyaga alibadili kauli yake ya awali na kusema mtafaruku ni kitu cha kawaida katika kazi huku pia akiendelea kukanusha.

“RB si karatasi la kawaida tu, siyo kweli bwana. Hiyo siyo stori achana nayo, kwanza kwenye kazi kugombana mbona ni kitu cha kawaida si kila jambo litatangazwa, hajawahi kunifikisha polisi,” alisema kwa kujikanyaga maneno.

DIAMOND SASA

Kwa upande wake Diamond alipotafutwa simu yake iliita bila kupokelewa lakini Ijumaa Wikienda limenasa jalada la kesi hiyo aliyoifungua Diamond katika Kituo cha Poisi Kijitonyama iliyosomeka KJN/RB/2020/2016 KUHARIBU MALI.

Nay wa Mitego na gari lake lililovunjwa kioo.



TUKIO LA NAY SASA

Katika tukio jingine, Nay wa Mitego, alinusurika kifo baada ya kuvamiwa mara mbili kwa nyakati tofauti na watu wasiojulikana huku wakimuacha na maumivu ya kumvunjia vioo na taa za gari zake mbili.

TUKIO LA KWANZA

Akiwa katika Mitaa ya Kinondoni Manyanya, Februari 24, mwaka huu Nay alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuegesha gari lake aina ya Toyota Prado kandokando ya barabara ambapo alipoingia dukani na kurejea, alikuta limevunjwa taa ya upande wa kushoto na watu wasiojulikana.

MAJANGA ZAIDI

Kama hiyo haitoshi, usiku wa kuamkia Februari 27, mwaka huu akiwa mitaa ya Sinza-Kamanyola, Nay alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana ambao walimvunjia kioo cha nyuma cha gari yake Toyota Port aliyokuwa ametoka nayo usiku huo na kuigesha maeneo hayo.
Prado ya Nay wa Mitego kabla  ya kuvunjwa taa ya nyuma. 
MSIKIE NAY

Akizungumzia matukio hayo, Nay alisema hajawahi kukutana na mwaka wa misukosuko kama mwaka huu baada ya kuachia wimbo wake wa Shika Adabu Yako ambao ndani yake ‘amewa-diss’ mastaa kibao wa Bongo.

“Dah! Naweza kujikuta hata nikimfanyia mtu maamuzi magumu, juzi tu nimetoka kuvunjiwa taa ya gari yangu ile Prado, nikiwa niko kwenye hali ya kutafuta fedha ya kununua taa, leo tena nimevamiwa na watu nisiowajua na wamenivunjia kioo cha gari yangu hii Toyota Port.

“Najua wanaonifanyia haya ni wajinga wachache ambao wanataka kupambana na mimi baada ya kuachia wimbo wangu wa Shika Adabu Yako, sasa kuanzia sasa itabidi niongeze zaidi umakini maana maadui wameongezeka japo nina RB ya kujihami,” alisema Nay.

TUMEFIKAJE HAPA?
Siku chache baada ya kuuachia Wimbo wa Shika Adabu Yako ambao ‘uliwachana’ mastaa wenzake kisha baadaye wimbo huo kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Nay amekuwa akipokea vitisho mbalimbali kutoka kwa watu asiowajua licha ya kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Kimara-Mwisho, jijini Dar.

Sunday, February 28, 2016

BANANA ZORRO APAGAWISHA UZINDUZI WA JOZI LOUNGE!

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Jozi Lounge,  Dismas  Massawe, akikata utepe kuashiria shughuli ya uzinduzi wa klabu hiyo.

 STAA wa muziki wa Bongo Fleva anayeupiga kwa njia ya bendi, Banana Zahir Zorro, usiku wa kuamkia jana aliwapagawisha vilivyo  mashabiki wake kwenye uzinduzi wa klabu mpya ya burudani ya Jozi Lounge iliyopo Msasani Village karibu na shule ya msingi Msasani jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo uliokatwa utepe na mmiliki wa klabu hiyo, Dismas Massawe, ulifanyika usiku mnene huku ukishuhudiwa na mamia ya mashabiki wa burudani ambao walijitokeza ambapo Banana  kupitia timu yake ya B-Band alisongesha burudani.

Akifanya makamuzi  muda mfupi tu baada ya  uzinduzi kufanywa, Banana  alitangaza kuwa kila siku ya Jumamosi bendi yake itakuwa ikifanya makamuzi hapo, hivyo akawataka mashabiki wajitokeze kwa wingi ili  kupata burudani ya kipekee.

“Nimefurahi sana leo kukutana na mashabiki wangu kwenye tukio hili la uzinduzi hivyo nitumie fursa hii pia kuwatangazia kwamba tutakuwa tukitumbuiza hapa kila siku ya Jumamosi, hivyo naomba mashabiki wangu wote tuwe tunakutana hapa kupata muziki mzuri na vinywaji safi kwa bei poa,” alisema Banana Zorro.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Banana Zorro, akitoa burudani muda mfupi baada ya uzinduzi wa klabu hiyo.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria uzinduzi huo wakiingia ndani ya klabu hiyo baada ya kuzinduliwa.
Mbunifu wa mavazi nchini,  Rhemtulah (kulia) akiwa na jamaa zake kwenye uzinduzi huo.
Baadhi ya waalikwa  kwenye uzinduzi huo wakiwa katika pozi.
Mtangazaji maarufu Tayana (kulia), akiwa katika pozi na wenzake.
Mashabiki wakiwa ndani ya Jozi Lounge.
Wadau wa klabu hiyo wakiwa katika pozi.
Tayana akiwa kwenye pozi.
Wadau wa Jozi Lounge wakiwa kwenye zulia jekundu (red carpet).
Dismas Massawe (kulia, akipozi mbele ya kamera.
Wageni Red Carpet.
Baadhi ya warembo waliohudhuria uzinduzi huo wakiwa kwenye pozi.
Mapozi yalitawala kwa mashabiki waliofika hapo.
Wadau wa ‘mastarehe’ wakiwa kwenye pozi.
:  Waalikwa wakiingia ndani ya Jozi Lounge muda mfupi baada ya uzinduzi huo kufanyika.

Saturday, February 27, 2016

Angalia matukio mbalimbali ya Bethidei ya Efm Sports Headquarters ilivyo fana!

Mkurugenzi wa EFM Radio, Frances Siza 'Majay' (kulia), akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye baada ya kumkabidhi zawaidi ya kikombe chene jina lake na nembo ya EFM kwenye hafla ya kusherehekea mwaka mmoja wa kipindi cha Sports Headquarters.

KIPINDI cha EFM Sports Headquarters kinachosikika kupitia Radio ya Efm usiku wa kuamkia leo kiliadhimisha mwaka mmoja tangu kianze kurushwa ambapo pati yake ilifanyika katika Ukumbi wa Sports Lounge, Posta jijini Dar.
Kipindi hicho cha Sports HQ ambacho kinazungumzia michezo mbalimbali hapa nchini na nje kilianzishwa mwaka jana Februari 27, ambapo kinaongozwa na mkuu wa kitengo cha michezo redioni hapo Maulid Kitenge na msaidizi wake, Omari Katanga.
Pati hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika bethidei hiyo ambayo ilianza majira ya saa 12 jioni na kumalizika usiku.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Nape alisifia uwezo wa watangazaji wa kipindi hicho licha ya kuwa na muda mfupi kwa kuwa na uwezo wa kuhoji maswali ambayo yamekuwa na tija.
































POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...