Tuesday, March 31, 2015

NIYONZIMA KUUNGANA NA WENZAKE LEONiyonzima
Kikosi cha Yanga kimeendeleza kimbizakimbiza ya kusaka mbinu za kuimaliza FC Platinum ya Zimbabwe kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Jumamosi wiki hii baada ya jana na leo kuwa katika makamuzi makali.
Hata hivyo taarifa mbaya ni kocha Hans van Der Pluijm amemkosa kiungo wake, Haruna Niyonzima ambaye hajarudi kutoka kwao ambapo alikwenda kuitumikia timu yake ya taifa, Rwanda katika michuano ya kirafiki ya kalenda ya Fifa.

Kikosi cha Yanga katika mazoezi leo asubuhi, kwenye Uwanja wa Karume, Dar.

Akizungumza na Tanzania One leo baada ya mazoezi ya klabu hiyo kwenye Uwanja wa Karume, Dar alisema kiungo huyo anatarajiwa kutua leo ama kesho.
“Niyonzima huenda akawasili leo ama kesho ili kuungana na kikosi katika safari yetu ya kwenda Zimbabwe,” alisema kiongozi huyo.
Matokeo yoyote chini ya kichapo cha mabao 4-0 yataisongesha mbele Yanga kwenye hatua ya pili ya mtoano kabla ya kutinga katika hatua ya makundi kwani ina mtaji wa mabao 5-1 walioupata katika mchezo wa awali jijini Dar.POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...