Thursday, April 23, 2015

WALALAMIKA KWA KUTOTAJWA KATIKA FILAMU YA FURIOUS 7

The Rock, Vin Diesel na Paul Walker ni baadhi ya majina ambayo yametajwa mwishoni mwa filamu ya kusisimua ya "Furious 7" iliyoingia sokoni hivi karibuni ... tatizo ni kwamba kuna baadhi ya watu ambao walishiriki kikamilifu kwenye matukio muhimu ya filamu hiyo ambao hawakupewa 'credit' mwishoni.
Sehemu ya matukio waliyoshiriki watu hao.
Vyanzo vya karibu na wazalishaji wa filamu hiyo vimeeleza kuwa watu hao walishiriki katika matukio muhimu ya filamu hiyo ikiwemo sehemu ya magari yenye parachuti na kukimbizana kwa magari maeneo ya milimani.
Mojawapo ya picha katika filamu ya Furious 7.
Kundi hilo la watu waliosahaulika limeeleza kuwa lilitoa jumla ya watu 25 ambao walihatarisha maisha yao katika filamu hiyo japo hawajatajwa mwishoni mwa filamu hiyo iliyojizolea umaarufu na kufanya vizuri sokoni ndani ya muda mfupi tangu itolewe.
Filamu hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza huko Australia Aprili 2, 2015, na baadaye kuzinduliwa nchini Marekani Aprili 3, 2015, na baada ya hapo iliachiwa kimataifa katika mfumo wa 3D.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...