Friday, April 24, 2015

MAMA KANUMBA, MAMA LULU KIMENUKA!

Mwandishi wetu
Taarifa zilizotua kwenye dawati la gazeti hili zinadai kuwa, wale wamama wa mjini ambao walikuwa mashosti hadi kufikia hatua ya kusema ni kama ndugu, mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, sasa kimenuka!

Mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.
DALILI KUWA PAKA NA CHUI
Chanzo chetu cha kuaminika kilidai kuwa, dalili za wawili hao kuelekea kugeuka kuwa paka na chui zilianza muda mrefu lakini hali ikazidi kuwa mbaya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Kanumba, Aprili 7, mwaka huu alipokuwa akitimiza miaka mitatu kaburini.

CHANZO NI LULU
Ubuyu ulidai kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kunumba, Mama Kanumba alimtuhumu Lulu kutotoa ushirikiano na kufikia hatua ya kutoa maneno makali zaidi yaliyomkera mama Lulu.


Mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
MAMA KANUMBA NA SMS MBAYA KWA MAMA LULU
Ilidaiwa kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba, mama Kanumba alimtumia mama lulu sms mbaya ya kejeli (kuiandika hapa siyo busara) ndipo mama Lulu ‘alipofyumu’ na kuona kwa hali hiyo bora kama mbwai na iwe mbwai.“Ile sms mama Kanumba alimtumia mama Lulu siku ile (Aprili 7) majira ya saa 11:00 alfajiri.


HAIKUWA YA KIUNGWANA
“Kwa kweli ilikuwa meseji mbaya mno. Alikuwa akimuagiza mama Lulu amuamshe Lulu kwa ajili ya kwenda kaburini kwa Kanumba lakini haikuwa ya kiungwana.“Hata hivyo, ukweli mama Lulu alitumia busara kwa kutomjibu lakini akadhamiria kuchukua hatua za kisheria,” alidai mtoa ‘ubuyu’ huyo.Enzi za ushosti wao.
Ilizidi kudaiwa kwamba, wakati mama Lulu akitafakari sababu ya shosti wake huyo ambaye walikuwa wakitembea mjini kama kumbikumbi kumtumia sms hiyo, akashangaa kusoma tena kwenye gazeti mama Kanumba akimpa vipande vyake Lulu, jambo lililozidi kumchefua mama Lulu.
KUBURUZANA KORTINI?
“Kimsingi hali ni mbaya sana sasa hivi, inavyoonekana mama Lulu kamchoka mama Kanumba na anataka kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuburuzana kortini,” alidai sosi huyo.

MAMA LULU AFUNGUKA
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta mama Lulu ambapo alipopatikana alikiri kupokea ujumbe na kwamba hali ni mbaya sana.“Nimeumizwa sana na sms ya mama Kanumba lakini siwezi kuwapa kwa sababu nataka kuifanyia kazi,” alisema mama Lulu.

Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
MAMA KANUMBA VIPI?
Kwa upande wake mama Kanumba aliendelea kusisitiza kuwa yeye ataendelea kumlilia mwanaye na hana mpango na familia hiyo ya Lulu.“Mimi kwa upande wangu nitamlilia mtoto wangu mpaka siku ya kufa kwangu lakini kinachoniuma ni Lulu kufanya sherehe ya mdogo wake siku ya kumbukumbu ya mwanangu.

“Jamani hata kama mtu ana roho gani, hawezi kufanya hivyo,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu sms aliyomtumia mama Lulu na kwamba mama huyo yupo mbioni kumchukulia hatua za kisheria hakuwa tayari kuzungumza chochote.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...