Tuesday, February 24, 2015

KOMBE LA DUNIA 2022 SASA KUPIGWA KRISMASI

 Bado fukuto kubwa linazidi kujitokeza kuhusu fainali za Kombe la Dunia ya mwaka 2022, zitakazoandaliwa nchini Qatar na sasa imehamishiwa mwezi Novemba na Desemba, kwa mujibu wa kikosi kazi cha Fifa.
Wakurugenzi wa soka wamekutana huko Doha, Qatar kujadiliana mengi kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa fainali hizo kutokana na hofu ya joto kali nchini humo, ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa wachezaji na mashabiki watakaozifuata timu zao.
Inatajwa kuwa joto nchini Qatar, hukufikia sentgridi (40°C) wakati wa kiangazi, huku miezi ya Novemba na Desemba likishuka hadi 25°C.
Pendekezo lilotolewa leo Jumanne, linatarajiwa kuafikiwa na kamati kuu ya Fifa huko Zurich, kati ya Machi 19 na 20.
Bosi wa kikosi kazi cha Fifa, Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa aliongeza kuwa michuano ya 2022 kuna uwezekano wa kufupishwa kwa siku. Tayari tetesi zinadai kuwa fainali hizo zitafungua dimba Nov. 26 na kutamatishwa Des. 23, siku mbili kabla ya Sikukuu ya Krismasi.
Lakini Fifa tayari imesema kuwa haina mpango wa kufupishwa kwa michuano kutoka timu 32 au mechi 64 kama ilivyo ada ya michuano yenyewe.

            Kwanini Nov-Des?
Tarehe nyingine iliyotajwa kuwezekana kuhamishia ni Mei na Januari-Februari. Fifa imesema idadi kubwa ya mapendekezo yameangukia Nov-Des kwa sababu:
*Jan-Feb, michuano ingeweza kuingilia na michuano ya Olympiki.
* Mwezi Ramadan utaanza Aprili 2, 2022, pia Mwezi Mei kwenda Septemba ni majira ya joto jingi sana
Katibu Mkuu wa Fifa, Mbrazili, Jerome Valcke alisema: "Kulikuwa na mabaya na mazuri kwa kila pendekezo, lakini mwisho wa yote tumeona ni bora iwe Novemba na Desemba." 

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...