Tuesday, February 21, 2012

 MAKAMU WA RAIS WA AIRTEL AFRIKA ATUA BONGO

Toka kushoto ni Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika kitengo maalum cha mawasiliano Michael Okwiri akipokelewa na Bi. Joyce Luhanga Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP (kati) mara baada ya kuingia katika ofisi kuu za IPP Mikocheni jijini Dar leo. Mwishoni ni kiongozi wa vipindi Radio One na Mtangazaji wa ITV, Bw. Isack Gamba akiwaongoza pia.
Bw, Isack Gamba ambae ni kiongozi wa vipindi Radio One na Mtangazaji wa ITV akiwaelezea jinsi wanavyofanya vipindi na kushirikisha wasilizaji live katika studio za Radio One Sterio Mikocheni jijini Dar.
Bw Wens Mushi ambae ni Kaimu Naibu Mhariri wa The Guardian akitoa maelekezo kwa Makamu wa raisi wa Airtel Afrika kitengo cha mawasiliano (alieshikilia gazeti) huku Bw Alexander Doll Mkurugenzi mkuu wa Hill+Knowlton Strategies (w apili toka kushoto) toka kampuni maalum ya Mahusiano ya Airtel Afrika akifuatilia kwa undani zaidi. Anaefuata ni Mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe Bw Jesse Kwayu pamoja na wadau wa Airtel nchini Tanzania.
Kulia ni Nasa Kingu Mkuu wa Vipindi wa East Afrika TV/ Radio akiwapokea na kutoa maelezo jinsi wanavyofanya shughuli za habari katika ofisi za East afrika TV/Radio.
------
• Apongeza juhudi za wanahabari nchini Tanzania
• Ahaidi Airtel itakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wanahabari katika mawasiliano

Makamu wa raisi wa Airtel Afrika katika kitengo maalum cha mawasiliano kwa umma leo amepongeza juhudi za wanahabari nchini mara baada ya kutembelea baadhi ya vyombo vya habari Tanzania ikiwemo IPP media na Mwananchi Communication ikiwa ni ziara ya siku mbili aliyojiwekea ili kujionea mambo mbalimbali katika ulimwengu wa Habari na Mawasiliano nchini.
Akiongea wakati wa ziara hiyo akiwa na wadau mbalimbali na wanahabari, Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika bw, Michael Okwiri alisema “Nimegundua Tanzania kunamaendeleo mazuri sana hasa ukiangali mitambo na vyombo vya habari kwa kweli vinaonyesha kupiga hatua kwa kiwango” Vile vile nawapongeza sana wanahabari (Journalists) kwa juhudi zenu za kutafuta habari na kuziwahisha kuzichapa kwa muda wa siku pamoja na mambo mengi, kwa kweli ni juhudi inayohitajika kukamilisha mambo haya mapema ili wasomaji wapate taarifa inayoendana na muda. Kwa upande wetu Airtel naomba niwashukuru wanahabari wote kwa ujumla nchini Tanzania hasa mnaoshirikiana nasi Airtel kuhakikisha huduma ya mawasiliano ya uhakika inawafikia wananchi kwa kupitia baadhi ya habari zinazochapwa na kusambazwa nchini na vyombo vyenu. Airtel tunaahidi ushirikiano wa kutosha katika mawasiliano ili tuweze kutimiza dhamira yetu ya Uhuru wa kuongea nchini kote” alimaliza kwa kusezema bw Okwiri.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...