Saturday, March 31, 2012

DIAMOND ARE FOREVER BURUDANI MWANZO MWISHO!!!

Wanenguaji wa THT, wakiwa wamembeba juu Diamond wakati wa shoo hiyo.

Diamond akionesha uwezo wake katika kucheza.

UKIZUNGUMZIA shoo kali kumi zilizoteka mioyo ya mashabiki hapa nchini na ukaacha kuizubgumzia shoo iliyopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, basi utakuwa hufuatilii kwa makini burudani zinazofanyika Bongo.

Shoo ya “Diamond Are Forever”, iliyochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku wa Machi 30, mwaka huu ni funga kazi ambayo kwa hakika ni namba moja kati nyingi zilizowahi kufanyika hapa jijini Dar.

Shoo hiyo ilipigwa na Nasseb Abdul ‘ Diamond’ au ukipenda unaweza kumwita ‘Platinum’ ilianza majira ya saa nne usiku na kuhudhuriwa na baadhi ya mastaa wa Bongo, akiwemo mpenzi wa zamani wa Diamiond, Miss Tz mwaka 2006 na mcheza filimu,Wema Isaac Sepetu.

Diamond alidhihirisha kuwa ana jina na uwezo wa kujaza mashabiki zaidi ya elfu moja peke yake bila msaada wa msanii mwingine.

Pamoja na shoo hiyo kutawaliwa na vituko vya hapa na pale kutoka kwa Diamond na Wema bado mashabiki walipata fursa ya kufurahia na wengine kukubaliana na uwezo wa Diamond katika kulitawala jukwaa.

Wasanii kutoka THT Elias Barnabas (kulia) na Amini wakimpa sapoti Diamond.

Diamond akicheza juu ya meza aliyokuwa ameketii Wema na marafiki zake.

Q Chief, akiimba huku amekaa chini katika shoo hiyo muda mfupi baada ya kukaribishwa na Diamond.

… akikumbatiana na mama yake mzazi.

Wema Sepetu akishangalia wakati Diamondi akicheza.

Jokate naye akicheza kwa furaha.

Diamond akiserebuka na mmoja wa mashabiki zake.

Wema akimtunza Diamond, ambaye alikataa kupokea mkwanja wake

Wema akionesha hudhuni baada ya Diamond kukataa kupokea fedha zake na kurejea kwenye meza yao.

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiingia ukumbini hapo.

Wema Sepetu wakati akiingia Ukumbini.

Diamond, Mama yake Mzazi na Queen Doreen wakiwa katika pozi mara baada ya kuwasili ukumbini.

Diamond na Mama yake wakiwasili.

Ndugu na marafiki wa Diamond, wakihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili ukumbini.

Mwanamitindo Martin Kadinda akihojiwa mara baada ya kuwasili ukumbini hapo.

Diamodi akiimba huku amempigia magoti Aunt Ezekiel.

Baadhi ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo wakiserebuka.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...