Saturday, March 31, 2012

ANGALIA JINSI DIAMOND ALIVYOKUWA AMEJIANDAA KWA SHOO YA "DIAMOND ARE FOREVER" NA MASHABIKI ZAKE


UKIZUNGUMZIA shoo kali kumi zilizoteka mioyo ya mashabiki hapa nchini na ukaacha kuizubgumzia shoo iliyopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, basi utakuwa hufuatilii kwa makini burudani zinazofanyika Bongo.

Shoo ya “Diamond Are Forever”, iliyochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku wa Machi 30, mwaka huu ni funga kazi ambayo kwa hakika ni namba moja kati nyingi zilizowahi kufanyika hapa jijini Dar.

Shoo hiyo ilipigwa na Nasseb Abdul ‘ Diamond’ au ukipenda unaweza kumwita ‘Platinum’ ilianza majira ya saa nne usiku na kuhudhuriwa na baadhi ya mastaa wa Bongo, akiwemo mpenzi wa zamani wa Diamiond, Miss Tz mwaka 2006 na mcheza filimu,Wema Isaac Sepetu.

Diamond alidhihirisha kuwa ana jina na uwezo wa kujaza mashabiki zaidi ya elfu moja peke yake bila msaada wa msanii mwingine.

Pamoja na shoo hiyo kutawaliwa na vituko vya hapa na pale kutoka kwa Diamond na Wema bado mashabiki walipata fursa ya kufurahia na wengine kukubaliana na uwezo wa Diamond katika kulitawala jukwaa.




Mwanamitindo anayeitendea haki fani hiyo nchini, Martin Kadinda katika pozi, na huyu ndiye aliyemvalisha Diamond na wote unaowaona wamevaa vikoti kama hivi vyake.































































Mavazi yaliyotawala katika shoo hiyo ukiachilia mbali la Mchomvu na Baby wake, yamebuniwa na Mwanamitindo anayeshika kasi Bongo, Martin Kadinda aliye katika picha ya pili juu.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...