Friday, March 30, 2012

AIRTEL YAWATANGAZA WASHINDI WA PROMOSHENI YA "NANI MKALI"


Afisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi.
Jane  Matinde  akitanzanga washindi wa  promosheni ya Mkali nani kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) ambapo washindi wa siku
hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki
hujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kulia ni Afisa
mawasiliano wa kampuni ya Airtel Bi. Dangio Kaniki akishuhudia  tukio
hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini
Dar-es-Salaam.

 
Airtel yawatangaza washindi wa "Nani Mkali" promosheni

*         Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki atangazwa
29, March 2012 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma
nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewatangaza
washindi wa wiki hii ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo
washindi wa kila siku watakabidhiwa shilingi milioni moja kila  mmoja
na mshindi wa wiki ataondoka na shilingi milioni tatu. Washindi hao
wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Arusha,
Zanzibar, Dar es Salaam, Nzega - Tabora na Manyara
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel
Dangio Kaniki alisema" Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania
kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa
washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika
promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali.  Na leo napenda kuchukua fulsa
hii kuwatangaza washindi wa wiki hii ambao ni
KAANAEL LEMLE KANUYA

ARUSHA

50

          1,000,000.00

RAKESH MANSUR DEYAL

ZANZIBAR

34

          1,000,000.00

NAPEGWA DAVID MONGO

DSM

58

          1,000,000.00

MARIAM WAZIRI HAMISI

DSM

32

          1,000,000.00

GUVANTRAI SACHDEV SHANTILAL

ARUSHA

54

          1,000,000.00

YUSUPH NOHAI ANNAI

MANYARA

35

          1,000,000.00

YUSUPH  MATHIAS MANONI

NZEGA-TABORA

25

          3,000,000.00


Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha
washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya
kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu
yetu ya jisikie huru, aliongeza Dangio
 kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na
kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali
na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo
sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja
na kodi.                                                        

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...