Friday, November 30, 2012

AIRTEL TANZANIA YAANDA PART YA KUMPONGEZA BALOZI WAKE AMBWENE YESSAYA "AY" NYUMBANI LOUNGE LEO



Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya Channel O aliyoipata Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa ushindi alioupa pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam


Afisa Uhusiano wa Airtel akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya video bora, Katikati ni AY akifatiwa na DJ wake Athur Baraka
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya “ AY “ na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “ I don’t wanna be alone”
Akiongea na wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fursa hiyo kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
Naye Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii mbalimbali toka Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa kusherehekea ushindi huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu. Tunapenda pia kuchukua fursa hii kuwaalika watanzania na wateja wetu leo pale nyumbani lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa Mziki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY'



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...