Wednesday, January 27, 2016

PROFESA JAY AGOMEA KUITWA MHESHIMIWA, AWATAKA WANANCHI WA MIKUMI WAMUITE MTUMISHI!

Mbunge wa jimbo la  Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay’. katika pozi.
Mbunge mpya wa Mikumi (Chadema) ambaye ni msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amewaambia wapiga kura wake kumuita Mtumishi badala ya Mheshimiwa, kwa sababu kazi yake ni kuwatumikia wananchi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Dodoma, Profesa Jay alisema alipoomba kura aliahidi kuwatumikia wapiga kura wake ili kufikia ndoto zao za maisha bora kwa kuondoa kero mbalimbali, hivyo hawezi kuifanya kazi hiyo kama atakubali uheshimiwa badala ya utumishi.
Mbunge mpya wa Mikumi (Chadema) Profesa Jay.
“Tuliahidi utumishi uliotukuka kwa wapiga kura, tumekuja hapa kuifanya kazi hiyo kwa kuisimamia serikali ili iondoe kero zote zinazowakabili wananchi, sasa ukiruhusu uheshimiwa, unaweza kujikuta unasahau wajibu wako, lakini kama kila mara utajikumbusha kuwa wewe ni mtumishi wao, hakika hautakuwa na muda wa kupoteza,” alisema mbunge huyo na msanii wa pili wa Hip Hop kuingia bungeni baada ya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ wa Mbeya mjini (2010).

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...