Friday, January 29, 2016

KHAAAA....KUMBE WEMA,NAJMA WANASHEA TENA PENZI KWA IDRIS!

Wema Sepetu na baba kijacho wake, Idris Sultan.


Ubuyu mpya kabisa uliotua kwenye meza ya dawati hili unadai kuwa, Mshindi wa Shindano la Big Brother 2014 ambaye anatajwa kuwa ndiye ubavu wa Wema Sepetu kwa sasa, Idris Sultan, anatoka pia na msanii anayefahamika kwa jina la Najma Dattan ‘Naj’.

Najma ni msanii wa muziki aliyewahi kuwa na uhusiano na Mr Blue kabla ya kuhamia kwa Diamond miaka kadhaa iliyopita.

Najma Dattan.

Kisikie chanzo
Chanzo chetu kilicho karibu na Najma kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, Idris na Najma wamekuwa wakitoka kwa muda mrefu na kwa ndugu wa binti huyo wala siyo siri.

“Unajua watu hawajui kuwa Idris yuko na Najma na mara kwa mara amekuwa akienda nyumbani kwao na hata ndugu wa Najma wanamjua.
“Kilichoibua taharuki ni juzikati Idris kudai ile mimba ya Wema ni yake, unaambiwa Najma anashangazwa na taarifa hizo,” kilidai chanzo hicho.

Wanaswa pamoja
Wakati madai hayo yakitua kwenye meza ya gazeti hili, mmoja wa mapaparazi wa Ijumaa hivi karibuni aliripoti tukio la Idris na Najma kunaswa pamoja kwenye hafla ya Clouds TV iliyofanyika pale Escape One, Mikocheni jijini Dar ambapo alisema:

“Mimi niliwaona pale Escape One, Idris alifika na kumchukua Najma na kumuingiza kwenye gari lake na kuondoka, alishuhudia Martin Kadinda, Steve Nyerere na mastaa wengine,” alisema paparazi huyo na kudai alikuwa akifuatilia ili kujua uhusiano wao.

Najma asakwa
Baada ya madai hayo kutua kwenye dawati la Ijumaa, jitihada za kumtafuta Najma kwa njia ya simu zilifanyika na alipopatikana alikiri kujuana vilivyo na Idris ila akagoma kuzungumzia uhusiano wao.

Ijumaa: Najma habari yako, unafahamiana na Idris? Je, ni mpenzi wako kwani kuna madai kuwa wewe unatoka na yeye kimapenzi na kwamba jamaa kakuzimia ile mbaya licha ya yeye kudai kampa mimba Wema, unalizungumziaje hilo?

Najma: Mh! Yaani nyie mmekosa la kuandika na udaku wenu, naomba nisiongelee lolote juu ya hilo.

Ijumaa: Tunachotaka kujua ni kama wewe na Idris ni wapenzi kweli, hilo tu.Najma: Niacheni jamani.

(Akakata simu)
Alipopigiwa tena hakupokea. Kwa upande wa Idris simu yake iliita weee, haikupokelewa, alipotumiwa sms pia hakujibu.

Ijumaa linaendelea kuwawekea mitego kwani kuna msemo wa Kiswahili usemao, mapenzi ni kikohozi, hawawezi kuficha uhusiano wao milele.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...