Akiwa tayari amesaini mkataba na klabu hiyo, Samatta alikuwa anasubiri ‘taa ya kijani’ kutoka kwa bosi wa TP Mazembe Moise Katumbi ambaye mwanzoni alikuwa anaweka ‘kauzibe’ kutoa ruhusa kwa mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika kwenda kujiunga na klabu ya Genk.
Atakumbukwa na wana-Lubumbashi kwa kuisaidia timu yao kutwaa taji la ubingwa wa Afrika mwaka 2015 pamoja na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kuifungia timu yao mabao saba kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.
![]() |
Samatta |
Samatta ameshawasili nchini Ubeligiji tayari kwa ajili ya kuanza majukumu mapya kwenye klabu hiyo ya barani Ulaya.
Klabu ya Genk imeshawahi kuwatoa mastar wakubwa barani Ulaya wanaotamba kwenye vilabu vikubwa vya ligi maarufu duniani. Christian Benteke (Liverpool), Kelvin De Bruyne (Manchester City), Thibaut Courtois (Chelsea) ni baadhi ya majina ya mastar ambao wamewahi kupita kwenye klabu ya Genk.
No comments:
Post a Comment