Monday, January 25, 2016

SOMA HAPA HABARI YA KUSIKITISHA MAMA KUWAUA WANAE WAWILI


 Eliza Bugusi Steven (28),Mwanamke anayedaiwa kuwaua wanaye

MARA: Mwanamke mmoja Eliza Bugusi Steven (28), mkazi wa Kijiji cha Kamugegi, Kata ya Kamugegi, Wilaya ya Butiama mkoani Mara, ameelezewa jinsi alivyowaua kwa kuwanywesha sumu watoto wake wawili wa kuwazaa.
Nicholaus Steven (miaka 4)
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa Eliza alifanya tukio hilo Januari 7, mwaka huu, saa nne usiku akiwa nyumbani kwao, kwa kile kilichodaiwa kunyanyapaliwa na ndugu zake baada ya mwanamke huyo kurejea kuishi kijijini akitokea jijini Mwanza alikokuwa akiishi na mumewe.
Francis Steven (miaka 2)
Marehemu hao, Nicholaus Steven (4) na Francis Steven (2) walinyweshwa sumu hiyo iliyokuwa kwenye kikombe na baada ya kuhakikisha wamepoteza uhai, mwanamke huyo naye alikunywa iliyobaki, lakini akaokolewa muda mfupi baadaye baada ya kupiga mayowe ya kuomba msaada.
Waombolezaji siku ya msiba
Inadaiwa kuwa, Eliza ambaye mumewe alifariki dunia mwaka jana, tangu alipofika kijijini hapo amekuwa akinyanyapaliwa na mama yake mzazi pamoja na mdogo wake, ambao wamekuwa wakimtuhumu kuugua ugonjwa unaotokana na ngono.

Diwani wa Kata ya Kamugegi, Ikungura Charles, amesema: “Mdogo wa Eliza ambaye aligombana naye muda mfupi kabla ya tukio hilo, ametoweka nyumbani hapo.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji na jaribio la kujiua baada ya hali yake kutengemaa,” alisema kamanda huyo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...