Wednesday, July 24, 2013

NAY WA MITEGO ATANGAZA KUMPIGIA KAMPENI LOWASA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2015


Haya ni mashairi aliyoyaandika Nay wa mitego kwenda kwa mtoto wa Rais a.k.a Riz One akimtaka amwambie baba yake kuwa mtwara hawataki korosho, wanataka gesi na pia Lowassa asiache kugombea urais maana yupo tayari kumpigia kampeni-2015
----------------

MASHAIRI YAKE:
Naongea na Riz one hey Riz One, we si mtoto wa raisi Riz one. Mwambie dingi yako Masela hawamuelewi wamakonde wa Mtwara hawataki tena Korosho, wanaitaka ges si mtawaua na mkong'oto?! Nani rafiki wa Lowasa anifikishie salam 2015 nataka agombee uraisi nitamfanyia kampeni wananchi wampe nafasi,

VIJANA WAUANA JIJINI MBEYA WAKIGOMBANIA PENZI LA MSICHANA



Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni s/o Sandu, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na Tolo s/o Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu.

Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Tuesday, July 23, 2013

CANDY N CANDY RECORDS KUSAKA VIPAJI VYA BONGO FLEVA JUMAMOSI HII LAMADA HOTEL



Candy n Candy Records kutoka Kenya inakuletea tamasha la kusaka vipaji vya wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Ishu hiyo itafanyika Jumamosi hii,tarehe 27/7/013 ndani ya ukumbi wa  Lamada Hotel kuanzia majira ya saa 3 asubuhi hadi jioni. 
Majaji watakao simamia zoezi la utafutaji vipaji hivyo ni Tundaman,Mazuu, Mama Loraa na Joe mmiliki wa Candy n Candy Records kutoka Kenya.
Tamasha hili litakuwa ni bure yaani hakuna kiingilio chochote.


Mmiliki wa Candy n Candy Records Mr. Joe katika pozi

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA LUCY KOMBA KUHUSU NDIKUMANA, WAIGIZA PAMOJA FILAMU YA KWANINI NISIMUOE.



Lucy Komba na Hamad Ndikumana
Muigizaji maarufu Swahiliwood Lucy Komba amemsifia Hamad Ndikumana(Kataut) ambaye ameigiza nae katika filamu mpya ya "Kwanini Nisimuoe" kuwa ana kipaji cha uigizaji tofauti na alivyofikiria mwanzoni kuwa inaweza kuwa shida kidogo wakati alipomfuata kwa ajili ya utengenezaji wa filamu hiyo. Ndikumana ni msakata kambumbu maarufu akiwa mwenyeji wa Rwanda na alimuoa muigizaji maarufu nchini Irene Uwoya miaka michache iliyopita ingawa kwasasa wanadaiwa kutengana.

Akichonga na Swahiliworldplanet kutokea nchini Denmark alipo sasa Lucy Komba alisema "Ndiku ana kipaji kusema ukweli wakati namchukua kufanya nae kazi nilijua nitapata nae tabu sana lakini ni tofauti na nilivyofikiria ni mtu mmoja kichwa sana yaani msanii ni msanii tu alicheza mpaka mwenyewe nilifurahi kwa kifupi ana kipaji cha uigizaji, maelekezo kweli nilimpa na kumfundisha nilimfundisha lakini uchezaji wake ulikuwa juu zaidi"

Lucy Komba ameibua waigizaji wengi maarufu wanaotamba sasa wakiwemo Jackline Wolper, Mzee Chillo na Irene Uwoya hivyo usije kushangaa Ndiku akifanya kweli kwenye kiwanda cha filamu. Filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni muda sio mrefu

WALIOWAUA WANAJESHI WA TANZANIA WATAJWA.....NI KUNDI LA "JANJAWEED" LINALOUNGWA MKONO NA SERIKALI YA SUDAN



WAKATI miili ya wanajeshi saba ikiwa imeagwa jana katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, imeelezwa kuwa kundi la Janjaweed linaloungwa mkono na serikali ya Sudan ndilo lililowavamia na kuwaua askari hao nchini humo na kuwajeruhi wengine 17 .

Wanajeshi hao wa Tanzania ambao walikuwa ni sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), walifanyiwa unyama huo Julai 13, mwaka huu katika eneo la kusini mwa Darfur, nchini Sudan.

Kiongozi wa moja ya makundi ya wapiganaji la Sudan Liberation Movement (SLM), Minni Mannawi ameibuka na kuwatuhumu wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo na ametaka ufanyike uchunguzi wa kimataifa.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Sudan Tribune alipokuwa anahudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu namna ya kupata amani ya kudumu nchini Sudan uliofanyika jijini Geneva Uswisi wiki iliyopita, alikanusha kuwa kundi lake linahusika na shambulio hilo.

“Tuna uhakika shambulio lililofanywa dhidi ya walinzi wa amani wa Unamid liliandaliwa na kutekelezwa na Janjaweed, tuko tayari kutoa ushirikiano kwa chombo maalum cha kimataifa kitakachoundwa kufanya uchunguzi kuhusu tukio hili…Nashauri serikali (ya Sudan) isishiriki katika uchunguzi kwa sababu itaficha ukweli,” alisema Mannawi.

Aliongeza kuwa wanamgambo hao waliowashambulia wanajeshi wa kulinda amani hivi sasa wanakabiliwa na ukata wa hali ya juu na kukosa vifaa kwa sababu serikali haina tena uwezo wa kuwahifadhi, hivyo wameamua kufanya matukio ya uporaji kukidhi mahitaji yao.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Martin Nesirky alisema wameanza kufanya uchunguzi wao binafsi. Taarifa ya UN ilieleza juzi kuwa mashuhuda wamekuwa wakieleza mauaji hayo yamefanywa na kundi linaloungwa mkono na serikali ya Sudan.

Wakati huo huo, majeshi ya Nigeria yamejitoa kulinda amani Darfur. Hazikutolewa sababu za kufanya hivyo japokuwa UN imethibitisha.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...